Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kumekuwa na mfululizo wa mashambulizi makali ya maneno ya kisiasa kutoka kwa Rais Samia na wasaidizi wake wa karibu dhidi ya mtangulizi wake marehemu Magufuli.
Binafsi sifurahishwi nayo kwa kuwa yamemlenga mtu aliyekufa (Magufuli) na yanasemwa na waliokuwa wasaidizi wa marehemu Magufuli, ambao waliibuliwa na kubebwa kwa 100% na Magufuli mwenyewe. Kumkana sasa Magufuli na siasa zake kabla ya kuwaomba radhi watanzania waliomizwa na utawala wa Magufuli huku Samia akiwa msaidizi na mshauri mkuu wa Magufuli, ni jambo la fedheha sana.
Yaani mabaya yote ya utawala wa Magufuli (kama ubabe, unyanyasaji, utesaji, wizi) wanasema yalikuwa ya Magufuli mwenyewe, lakini mema yote ya Magufuli (kama ujenzi, miradi, usimamizi, uwajibikaji) wanasema yalikuwa ya wote kwa umoja wao! Huu ni unafiki mkubwa.
Sote tunajua kuwa uchaguzi wa 2015 ulichezewa ili Magufuli aingie madarakani, na uchaguzi wa 2020 ulichezewa na Magufuli mwenyewe kwa 100% ili aendelee kukaa madarakani. Na Magufuli aliyafanya hayo yote kwa maslahi yake binafsi, maslahi ya CCM na maslahi ya wasaidizi wake. Leo hii watu wale wale kumkaanga Magufuli kisiasa ni jambo la ajabu sana.
Kwanini hawakusema hayo wakati Magufuli akiwa bado hai?
Kwanini hawakukaa hata pembeni ili kukwepa kushiriki dhuluma aliyotendwa na Magufuli?
Yaani leo hii Magufuli amegeuzwa na CCM ya mama Samia kuwa dampo la kufichia uchafu wote wa kisiasa unaonuka wa CCM uliofanywa na CCM na serikali yake tangu 2015-2021. Hii hatari sasa.
Ilitosha sana kwa mama Samia na CCM yake kuja kwanza hadharani kuwaomba radhi watanzania kwa utawala mbovu wa Magufuli uliokosa aibu, utu na haki, kisha kutafuta maridhiano ili ukurasa mbovu wa utawala wa Magufuli ufungwe milele katika taifa letu.