Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Mkuu kwenye siasa uwongo na kweli havikwepeki

Kuna muda ukweli unaweza kufanya damage kubwa kuliko uwongo, hapo ndio kuna umuhimu wa kupotezea kuliko kusema
Bora kuwa mkweli siku zote utakuweka huru, atamsifia magu alipofanya vizuri lakini alipokwanga wacha amnange kisawasawa, damage ya kusema ukweli itachukua muda mduchu sana uongo ndio utakuathiri milele
 
Mambo mengine ni uwezo binafsi.

Swala hapa ni kutomuexpose na situations kama hizo.

Yaani wasaidizi wake wawe wajanja kumkwepesha na mazingira kama hayo. Itokee very rare kuwa anahojiwa na vyombo vikubwa kama hivyo.

Huko mbele watu wako ahead of us kwa karne kadhaa. Uwezo wao wa kufikiri ni mkubwa sana.
 
serikali kuwa organised haimaanishi wote muwe na mawazo yanayofanana kama Mayai

kutofautiana misimamo haimaanishi serikali haina umoja
Ruksa kutofautiana ndani sio kuyabwaga nje
Tofauti zenu za mawazo mnatakiwa kuzimaliza huko ndani sio Marekani

Mfano ukiwa mwandishi wa habari unaandika habari za kikao cha chama.Kwenye hicho kikao wajumbe wakagawanyika makundi mawili yanayopingana wakaanza kuporomosheana matusi ya nguoni kila upande kiasi mwenyekiti akashindwa kudhibiti kikao kikavunjila bila muafaka mwenyekiti akasema tukutane tarehe ingine ikakubalika

Ukienda kutangaza au kuandika mwandishi wa habari unatakiwa uripoti hivi kuwa kikao kilikuwa kizuri ambapo mwenyekiti alitoa uhuru kwa kila upande kutoa hoja kwa uwazi kadri ulivyoweza. Baadaye ilikubalika tarehe ingine ya kikao kingine .Huandiki kuwa walitukanana na kutaja matusi waliyoporomosheana

Anyway jibu la mama Samia limekosa hata hekima tu ya kiutu uzima tukiachana na uraisi wake
 
Mahojiano ya jana ya Rais Samia na Gazeti la New York Times alinukuliwa akisema alipata wakati mgumu kufanya kazi na Hayati Magufuli kutokana na msimamo wa Magufuli juu ya Covid-19.

Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.

Kwa wanaoangalia mahojiano ya viongozi na waandishi wa habari wa nchi za 'mbele' wanajua jinsi waandishi hao wanavyokuwa aggressive, mnakumbuka Tundu Lissu mwenyewe alivyobanwa na mwandishi wa BBC hadi kujikuta ametamka atawapa mashoga haki zao...! Baadae akaja kukana hakumaanisha hivyo, ila sikumlaumu maana unabanwa kwelikweli.

Sasa kwa mtu kama Rais ambaye ana wasaidizi wengi smart walitakiwa ku-anticipate maswali ambayo angeulizwa Rais, na Rais angekua namna ya kuyajibu kabla, kuna maswali mengine unaya-dodge tu badala ya kutoa majibu direct ambayo yataleta utata, ndivyo wanasiasa hufanya.

Wasimuache kama anaenda kuhojiwa TBC.

Nadhani hili halitajirudia tena.
tusilaumu wasaidizi, yeye ni smart kiasi cha kuelewa namna ya kujibu maswali ya waandishi?

kikeke juzi hapa kamsumbua tena mahojiano ya kiswahili kabisa, kaanza kusema wa mitandaoni sio watanzania!
nadhani tukubali tumepigwa, bibi sio smart upstairs
 
ndio utuambie alitakiwa aseme vipi ?
Mfano hilo suala la Covid angejibu mbinu za kukabiliana na Covid ni suala lenye ubishi dunia nzima, ikiwemo Marekani yenyewe, na ndani ya serikali ya Magu walichukua zile hatua nyepesi kama za kunawa mikono, distance n.k
Huku wakifanya utafiti zaidi kabla ya kuchukua hatua zenye kuathiri

Hii haina utata wowote
 
tusilaumu wasaidizi, yeye ni smart kiasi cha kuelewa namna ya kujibu maswali ya waandishi?

kikeke juzi hapa kamsumbua tena mahojiano ya kiswahili kabisa, kaanza kusema wa mitandaoni sio watanzania!
nadhani tukubali tumepigwa, bibi sio smart upstairs
Samia yupo smart sana, kuna marekebisho mengi anayafanya ya kuisadia nchi ambayo ilikuwa ikiharibika kipindi cha mtangulizi wake
 
Jibu alilojibu raisi linaonyesha Serikali haikuwa organized .Raisi kivyake makamu kivyake utafikiri Serikali ya Sudan kusini kati ya Raisi Salva Kiir na makamu wake Riech machar!! Hakukuwa na unit of command and purpose

Swali je sasa Serikali ya Mama Samia iko organized from bottom to the top? Hilo swali kawaachia homework wamarekani wafanye analysis wenyewe!!
Nje ya Mada Mkuu;

Vipi hali ya usalama kwa wageni Sudan Kusini? Kuna dogo kapata kazi huko ila muda wa kuripoti bado, ndio anawaza aende au asiende?
 
Wamarekani wenyewe wanaomba yasije kuwakuta kama yaliyotukuta Tanzania Biden akafa yule mama akachukua nchi kwani wanajua madhara ya mwanamke kua kichwa cha nchi.

Mwanamke ni mwanamke tu.
Uingereza, Ujerumani, New Zealand, Liberia, hata wahafidhina kama Pakistan waliongozwa na wanawake ambao walifanya vizuri kuliko wanaume wengi tu
 
Mkuu tanzania bado hakujakuwa na ujasiri huo ama utamaduni huo kwamba ukishindwa kufanya naye mtu kazi wa juu yako ukae pembeni ni vile unabaki na matumaini tu na kuendelea sio kwa mama samia tu hata nyerere alikuwa mtumwa kwa wazungu

Muacheni mama awagonge zile sehemu zenu zenye maumivu, Sasa mumeona mama mwanamke wa kizanzibari alivyopiga hatua kuliko mwendazake mnakosa amani na usingizi., Mama bado yupo sana.
mkuu, amepiga hatua gani huyu bibi?
 
Sio kosa lako, umeathiriwa na matatizo ya kusema uongo ili kulinda hadhi fulani. Tatizo la kutokusema ukweli ndio limetufikisha watanzania hapa tulipo. Mama kaulizwa 2+2 kasema ni 4, ulitaka aseme ni 5 kama tulivyozoeshwa hapa nchini?
Mkuu ushawahi ku deal na siasa practically ukiachana na hiza za kwenye keyboard na vijiweni? Iwe upinzani au CCM?

Kama ulishawahi ungejua kuwa kuna muda huwezi kuongea kila kitu kwa public, kwa faida yenu wenyewe na kwa faida ya public
 
Mambo mengine ni uwezo binafsi.

Swala hapa ni kutomuexpose na situations kama hizo.

Yaani wasaidizi wake wawe wajanja kumkwepesha na mazingira kama hayo. Itokee very rare kuwa anahojiwa na vyombo vikubwa kama hivyo.

Huko mbele watu wako ahead of us kwa karne kadhaa. Uwezo wao wa kufikiri ni mkubwa sana.
Naunga mkono hoja uwezo wake kukabiliana na Press mdogo mno hatofautiani na marehemu Magufuli!! Yuko below standard achape tu kazi kama Magufuli watu wa mu judge tu kwa kazi zake.

Lakini kwenye vyombo vya habari Magufuli alikuwa dhaifu na mana Samia mdhaifu mno pia wote ujenzi hoja kwenye Press Hawako vizuri
Wasaidizi wa mama Samia wa take note huo ushauri wako
 
Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.

Kwa wanaoangalia mahojiano ya viongozi na waandishi wa habari wa nchi za 'mbele' wanajua jinsi waandishi hao wanavyokuwa aggressive, mnakumbuka Tundu Lissu mwenyewe alivyobanwa na mwandishi wa BBC hadi kujikuta ametamka atawapa mashoga haki zao...! Baadae akaja kukana hakumaanisha hivyo, ila sikumlaumu maana unabanwa kwelikweli.

Sasa kwa mtu kama Rais ambaye ana wasaidizi wengi smart walitakiwa ku-anticipate maswali ambayo angeulizwa Rais, na Rais angekua namna ya kuyajibu kabla, kuna maswali mengine unaya-dodge tu badala ya kutoa majibu direct ambayo yataleta utata, ndivyo wanasiasa hufanya.
“One of the mistakes which some political analysts make is to think their enemies should be our enemies,” he said which was met by applause. “Our attitude towards any country is determined by the attitude of that country to our struggle. Yasser Arafat, Colonel Gaddafi [and] Fidel Castro support our struggle to the hilt. There is no reason whatsoever why we should have any hesitation about hailing their commitment to human rights as they’re being demanded in South Africa. They do not support [the anti-apartheid struggle] only in rhetoric; they are placing resources at our disposal for us to win the struggle. That is the position.” Nelson Mandela
 
hayo majibu unajibu kama upo kibarazani kwako unakunywa kahawa sio mbele ya beberu unaemtomasa akupe pesa urudi nazo
Mfano hilo suala la Covid angejibu mbinu za kukabiliana na Covid ni suala lenye ubishi dunia nzima, ikiwemo Marekani yenyewe, na ndani ya serikali ya Magu walichukua zile hatua nyepesi kama za kunawa mikono, distance n.k
Huku wakifanya utafiti zaidi kabla ya kuchukua hatua zenye kuathiri

Hii haina utata wowote
 
Siyo siri kwamba mahusiano yetu na Marekani yalivurugika kipindi cha utawala uliopita ambao Rais wa sasa alikuwa sehemu yake kwa ngazi za juu kabisa. Kutegemea aende Marekani na kuondoka bila kuulizwa haya maswali au kuyajibu, kana kwamba kila kitu kilikuwa sawa, tuendelee tulipoishia 2010, ni kujidanganya. Haya maswali alitegemea kukutana nayo na sioni namna gani nyingine tofauti angeweza kuyajibu.

It is what it is
 
Mkuu ushawahi ku deal na siasa practically ukiachana na hiza za kwenye keyboard na vijiweni? Iwe upinzani au CCM?

Kama ulishawahi ungejua kuwa kuna muda huwezi kuongea kila kitu kwa public, kwa faida yenu wenyewe na kwa faida ya public

Mkuu narudia tena, umeathiriwa na hizo siasa unazosema hapa, ndio maana unapata tabu kwenye baadhi ya mambo. Si kosa lako bali ni makuzi.
 
Ni majibu fair lakini. Halafu wenyewe wanajua anayofanya Samia , interview moja sidhani kama ndio kipimo cha kumpima
hayo majibu unajibu kama upo kibarazani kwako unakunywa kahawa sio mbele ya beberu unaemtomasa akupe pesa urudi nazo
 
Back
Top Bottom