Rais Samia anasema 'hili tunalichukua'. Hayati John Magufuli aliamua pale pale jukwaani

Umejidhalilisha sana uliposema Jiwe alikuwa anajua idadi ya samaki, ajue idadi ya samaki ila hajui hata marais wa nchi maarufu.
Hii chuki mliyonayo kwa JPM kwahakika itawa haunt maisha yenu yote...Hivi kwanza hamuoni kuwa ni laana kugombana na maiti? Mtu anaweza dhani mlimloga daah, mbona mnajichora hivi?
 
Kama hili hulijui basi wew siyo mfatiliaji wa siasa za Tanzania. Acha uvivu tafuta maarifa mwenyewe mimi nimkupa hints tu.
Unajidharirisha kwa kuja na ushahidi usio na reference, sio tu kwenye siasa za Tanzania, kwenye kila jambo ulimwenguni ukiweka accusations or any sort of concerns just make sure to clarify your tales, otherwise zinakuwa ni story za kwenye kahawa, wasomi wanalijua hilo lakini, conclusively, you have helped me to imagine what kind of person I’m dealing with.

Sidhani kama magazeti na habari kwenye television zingekuwa zinapewa attention endapo zingekuwa zinatoa hints tu kama hizi zako. Anyways, huna tofauti na wasoma vichwa vya habari as if hiyo habari ipo sokoni inauzwa.
 
Reactions: Ame
Tuseme sifa za “ujasiri” na “uthubutu” za JPM zimeshapoteza maana kwa mtazamo huu mpya?
Madhara ya ujasiri yamekuja kuonekana baadae. Watu wameumizwa kwa maamuzi hayo yaliyowafurahisha watu jukwaani na wakaishia kushangilia.

Kumekuwepo na uonevu na makundi mawili yasiyokuwa na sababu wala umuhimu.
 
Kuna dada fulani alikuwa akipigwa na mumewe mara kwa mara bila hata kosa la msingi. Baadaye yule mume akabadilika akaona mambo yale ya ugomvi siyo mazuri, akabadilika akawa mtu mwenye hekima, anayesikiliza, na kutoa maamuzi ya busara, yenye maoni na mapendekezo kuliko kipigo na ugomvi. Yule dada akawa anashangaa kila siku zilivyosonga mbele, na mwishoni akamwuliza muwewe "Hivi mume wangu siku hizi kwa nini hunipendi kama zamani?"

Kwanini hunipigi tena" Hii stori ni ukweli mtupu, na nimeona imefanana na uzi huu hapo juu. Watu walishazoea uongozi wa ukali, maamuzi ya haraka na makali- Hiyo ni style ya uongozi ambayo ilikuwa na faida zake, ila pia kuna style nyingine za uongozi ambazo nazo ni nzuri tu hata kama zinachukua muda kutoa maamuzi. TUWE WAELEWA
 
Alijenga hulka ya kuogopwa ambayo ni mbaya kwa taifa lenye watu wasio na mazoea ya kujiamini wakati wanajenga hoja.

Alitengeneza spirit ya hasira iliyomnyima ukuaji wa nafsi yake mwenyewe kwa kuwa na tabia ya kupandisha hasira mara kwa mara.
 
Hoja ya uzi ni maamuzi yanayochukuliwa baada ya kiongozi kujiridhisha kwa kuyalinganisha na yale ya pale pale jukwaani. Yapi ni bora na yenye uwezekano wa kuwa na faida zenye kudumu kwa muda mrefu.
 
Madhara ya ujasiri yamekuja kuonekana baadae. Watu wameumizwa kwa maamuzi hayo yaliyowafurahisha watu jukwaani na wakaishia kushangilia.

Kumekuwepo na uonevu na makundi mawili yasiyokuwa na sababu wala umuhimu.
It was important by then kwakua tulishakuwa watu ambao hatutimizi wajibu zaidi ya kupenda kupiga na kufanya uvivu kisha tukaombe kwa wafadhili......
 
Alijenga hulka ya kuogopwa ambayo ni mbaya kwa taifa lenye watu wasio na mazoea ya kujiamini wakati wanajenga hoja.

Alitengeneza spirit ya hasira iliyomnyima ukuaji wa nafsi yake mwenyewe kwa kuwa na tabia ya kupandisha hasira mara kwa mara.
Kiongozi wa nchi lazima aogopwe na aheshimiwe at the same time, laiti kama umeshawahi kufanya kazi na Wazungu walio/ wanaoitawala dunia (Germany, Uk, USA) jinsi wanavyotengeneza fear kufanya mambo yao yaweze kwenda vizuri, kwa haraka na kwa viwango, jinsi wanavyoweza kumfukuza mzembe bila huruma sidhani kama ukajiuliza kwanini wako mbele yetu.

Wanafuatia Wachina na Wahindi, sisi wa mkiani bado tunataka kurembana rembana kama maharusi, tutabaki nyuma kama makalio mpaka kiama… maybe ndio position tunayoipenda anyways….
 
Idadi ya samaki hahaha, mkuu umemalizia kwa kichekesho ulichokiandika kwa umakini kama kina ukweli wowote ule.

Alikuwa ana hasira za haraka zinazomnyima busara kama alivyomtukana yule mkurugenzi mbele ya hadhara.

Unapotoa maamuzi ya hapo hapo ni lazima ujiridhishe na taarifa na usahihi wake kwa asilimia angalau tisini na tano. Unasema alikuwa anajiridhisha na taarifa alizokuja nazo kikaoni, vipi kama kuna tukio limetokea baada ya yeye kuwa na taarifa hizo?.
 
Kama hujaogopwa uwe na usahihi wa taarifa unazopewa, vinginevyo cheo chake kitakujengea chuki kwa unaowaongoza.

Vipi kama ni taarifa zinazoegemea kwenye majungu kuliko uhalisia?.
 
Hoja ya uzi ni maamuzi yanayochukuliwa baada ya kiongozi kujiridhisha kwa kuyalinganisha na yale ya pale pale jukwaani. Yapi ni bora na yenye uwezekano wa kuwa na faida zenye kudumu kwa muda mrefu.
Yote ni bora ila context matters...Msikariri tu,kuna maamuzi hayahitaji hata kusubiri, kuna ambayo yanahitaji confirmation na kuna ambao yanahitaji muda ili yachunguzwe.

Sasa msimsingizie hayati bure, alikuwa anapewa briefing kila siku kusema kuwa alikuwa anafanya maamuzi papo kwa papo hakuna anayeweza thibitisha.

Contrary basi ziara zake zote zilikuwa well planned na alishafanya assignment yake kabla ya kufika hapo sehemu. Ukwlei tunaoujua JpM alikuwa anasoma sana taarifa kwahiyi kuja na general and sweeping statement ni furahisha genge tu nyie wachuma janga waty mliojaa majungu na unafiki wa kiwango cha lami.

Hasira zenu zipelekeni kwenye kuiendeleza nchi, yeye amesha pumzika hangaikeni na yenu huku, hana sehemu tena katika maisha haya.

Rest in Power Dr. John Joseph Pombe Magufuli...Because of you am proud of being a Tanzanian!
 
Tatizo lako Ame ni la watanzania wengi tu. Kudhani kuwa kumkosoa JPM ni kuwa upande unaomchukia, you are very wrong.

Maamuzi ya haraka siku zote yanazo hasara nyingi tu. Mfano ni pale alipokuwa anawatumbua watu halafu wanaendelea kuwa ni sehemu ya pay roll ya serikali wakipata haki na stahiki zile zile wanazopata wafanyakazi wengine.

Maamuzi mengine ya haraka ni kupeleka pesa ya sherehe za uhuru za mwaka 2016 kujengea barabara ya Morocco halafu baada ya miaka michache inabomolewa na kujengwa upya kwa pesa nyingine!. Kwanini ujenzi usifanyike wote kwa mara moja?.
 
Kama hujaogopwa uwe na usahihi wa taarifa unazopewa, vinginevyo cheo chake kitakujengea chuki kwa unaowaongoza.

Vipi kama ni taarifa zinazoegemea kwenye majungu kuliko uhalisia?.
Majungu yapo sikatai, lakini lisemwalo lipo, ukisubiri kamati za uchunguzi kwenye kila takataka ndani ya nchi kubwa hii sidhani kama miaka 10 inatosha kufanya Maendeleo mbalimbali, kila kauchochoro kuna kero, wengine wasilalamikiwe ulalamikiwe wewe mpaka raisi anafika hujatafuta suluhu utegemee akuache wewe asiwasikilize mabosi wake.

Samia aliyakataa mabango lakini nasikia saizi kaanza kuyakubali, huo ndio wajibu wake, kufanya maamuzi ya papo kwa papo, ya muda mrefu pia.

Hivi tujiulize, pale uingereza umeshawahi shuhudia maswali na hoja mbalimbali kwa waziri mkuu wao, lazima majibu yakina yapatikane, sasa si kila hoja angekuwa anasema tutaenda kulijadili na kurejesha majibu, unaenda kujadili na nani? Hicho ndio kipimo cha competency yako.
 
Kwa aina ya watu tulionao kwenye utumishi wa umma, sekta binafsi zenye kushikilia kiuchumi, na wananchi wa kada nyingi tulihitaji uongozi wakariba ya Hayati JPM watu wetu wengi tunawaongoza wanahitaji kusukumwa kwa nguvu ukiwapa nafasi ya kujisimamia wanaujinga mwingi kuliko unavyo weza kufikiria. Mtu ambaye anatoa malalamiko kuhusu aina ya uongozi wa JPM hajawahi kuongoza... sisi ambao ambao tumeongoza taasisi na makundi makubwa ya watu tunajua namna watu wetu waliovyo.. ukilegeza kamba kidogo jiandae kulaumiwa..

Watu wanawaza wizi na utajiri wa kupindukia wanawaza rushwa kwa makusudi, hawana mipango ya kufanikisha malengo ya taasisi, wanasababisha urasmu ili kuweka mazingira ya kupewa kitu, angali taasisi za uma zenye mamlaka ya utoaji leseni, vibali mbali mbali wanavyo tekeleza majukumu yao kuna mambo hayapo sawa ni watendaji wachache sana wenye kusimamia haki. Angali mahakama, polisi, uhamiaji na vyombo vingine vinavyo simamia sheria, ukiwa ni mtu ambae umehudumiwa na makundi haya kwa haki bila usumbufu au mazingira ya rushwa una haki ya kukataa aina ya uongozi wa JPM.

Kwa eneo kubwa mama ni mtu laini sana kuweza kusimamia nchi yenye watu wa aina yetu, hakuna kitakacho fanyika kwa kizingatia muda na gharama halisi ( Inflation kila kona) , kila siku ataishia kutueleza yeye ni mpole asiye fokea watu nk. Si mlaumu maana mazingira alikotokea na aina ya maisha aliyopitia hii kwake ni zali la mentali..... Lakini watamwangusha sana kwa hilo ninauhakika kwa kuwa nayashuudia kila siku.

Wafanyabiashara duniani kote ni watu wanaobanwa kulipa kodi na kudhitiwa kwenye mfumuko wa bei, ukiwaachia wanakuchezesha maana mstari kati ya wahalifu wa wafanyabiashara ni mwembamba sana. Swali la kujiuliza ni kwa hawa wamachinga wanaolalamikiwa kukwepa kodi..(Kuchafua mazingira naliacha kwanza) Je machinga ni nani ... trade dealer, peddler au mchuuzi yaani ni mtu anaeuza end products to be used with last consumer.. Sio Distributor, sio whole seller sio muagizaji, kama hivyo ndivyo serikali inashindwaje kukusana kodi yake? Maana yake wafanyabiashara wakubwa wana watumia machinga kukwepa kodi... sasa leo Dar wameanza kuwaondoa ngoja tuone makusanyo kama yataongezeka! Petrolium products zinapanda kila kukicha, bidhaa za chuma kila siku juu, mafuta ya kula nk Bila kuwa na mtu wa kuwafinya wafanyabiashara wananchi wa kawaida ndio wana beba mizigo yote na mwisho umasikini kuisha kwao ni ndoto ya alinacha.​
 
So Rais anafanya maamuzi based on taarifa za kusikia kwa wananchi bila kujiridhisha! Vp kama wanamdanganya au ni chuki zao? Refer yule mama tapeli.
Wewe acha ushamba,ukiona Rais anakwenda sehemu kuna watu wametangulia miezi 3 mbele, hivyo Rais akiwa sehemu anatarifa zote, ndio maana Magufuri alikuwa akiwaumbua wasaidizi Wake adharani, Rais ni tasisi kubwa sio Mtu mmoja.
 
Unakwenda kujadili na serikali yako ili mje na majibu ya kina na yatakayodumu miaka mingi ijayo. Uingereza ni dunia ya kwanza yenye teknolojia ya juu sana ya kutatua matatizo mbalimbali.

Majibu ya pupa huwa na madhara ya kudumu na ya muda mrefu ujao. Pia unajenga tabia ya kuogopwa na mfumo mzima, kila mtu anataka kukimbia ili aende na kasi yako, nani kakudanganya kuwa kasi yako ndio sahihi kulinganisha na za wengine?.
 
Ni ujuha kuamini kuwa JPM alienda sehemu na kusikiliza kesi bila information zozote. Kuna mengi aliyajua kabla ya kufanya ziara na maamuzi yake.
 
Raisi sio diwani au balozi wa nyumba kumi bro, litambue hilo vizuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…