Rais Samia anasema 'hili tunalichukua'. Hayati John Magufuli aliamua pale pale jukwaani

Kuna kukosoa na kum demonize...Ni vitu viwili tofauti...Umesema kweli tatizo langu ni la watanzania wengi, kwakua watanzania wengi walimkubali JPM kuwa alikuwa na dhamira njema kwa taifa lake, hilo tu linatosha kumwona hafai kufanyiwa hayo mnayotaka kuyafanya
 
Si kweli..ama hujui au ulikuwa haufatilii ziara za Jiwe. Mara nyingi Jiwe alifanya ziara akiwa na timu ya viongozi mbalimbali na hata kama hatokuwepo kwenye msafara kiongozi basi ikiibuka hoja inayohusu sekta fulani basi kiongozi atapigiwa simu huko huko alipo.

Magufuli alipenda kusikiliza kero za watu. Mama toka siku ya kwanza alitangaza hataki mabango.

Magufuli alikuwa na uwezo wa kupewa changamoto akaichambua kwa vifungu vya sheria na kanuni na akapambana kwa hoja na viongozi wake. Na inapobidi anatuma watu wake kama ilivyotokea yule mama kule mbeya aliposema aliyembaka mtoto wake kule tunduru aliachiwa huru, magufuli alituma watu wake na siku iliyofuata alimpa mrejesho kuwa yule mtu yupo ndani.

Sote ni mashahidi. Kuna wakati magufuli aliwatoa nishai walalmikaji kwa kuwaambia wafuate sheria. Na hakutatua matatizo peke yake, ilikuwa lazima ashirikishe mamlaka husika na ikibidi mlalamikaji anakabidhiwa kwa wahusika.

Kutatua matatizo papo kwa papo inahitaji uwe na uwezo wa kufatilia taarifa na kujua sheria na kanuni. Tukubali tu kuwa si kila kiongozi anaweza hilo. Wengi huwa wanaishia kusema nalichukua nitalifanyia kazi. Kisha imeisha hiyo.
 
Bado kitambo kidogo, tutaweza kubadili upepo,maana kuimba kwa midundo ya mpiga ngoma imesha kuwa jadi yetu ingawa muda ni mwalimu mzuri
 
Kum demonize umekwenda mbali sana mkuu. Mwanasiasa anadumu miaka na miaka baada ya kifo chake kwa kuyaweka hai yote aliyoyafanya.

Viongozi kama Sokoine na Lumumba wapo hai mioyoni mwa watu kwa sababu yale waliyoyafanya ndio yanayoendelea kuwahukumu. Dhamira njema kwa taifa ni suala moja na udhaifu wake wa maamuzi ni suala jingine tofauti kabisa.
 
Mkuu nilifuatilia sana ziara za Jiwe nchi nzima. Nilichokiandika ninakifahamu na ninao uhakika nacho. JPM alipenda kushiriki kila kitu kinachoendelea nchini, ni mpaka siku zake chache za mwishoni kuelekea kifo chake alikuwa bado anawapigia simu wasaidizi wake akifanya kazi.

Huko kupenda kuwa sehemu ya maamuzi iwe ni nyeti au ya kawaida ndio ilikuwemo tabia ya maamuzi ya haraka yanayokuja kupingwa baadae.
 
Bora uchelewe lakini utende haki, kuliko kuwahi na utende dhulma.

Suala ni kuongeza washauri na kupanua taasisi. Ni uongo kudhani kuwa Mtu mmoja "Rais" atatatua kero za watu milioni 60 kama ulivyokiri mwenyewe kuwa nchi hii ni kubwa.
 
Mama hana huo ujinga
 
Mama mtu mkweli mpenda haki asiyeyumbishwa
 
Yaani yule kayafa alikuwa anavuruga bajeti haheshimu mipango anakurupuka Ili tuu afurahishe wajinga,stupid na robo.
 
Hii chuki mliyonayo kwa JPM kwahakika itawa haunt maisha yenu yote...Hivi kwanza hamuoni kuwa ni laana kugombana na maiti? Mtu anaweza dhani mlimloga daah, mbona mnajichora hivi?
Chuki gani yule mtu wenu alikuwa mwehu? Si ajabu tumeambiwa Tzn kuna wagonjwa wengi wa akili mfano ndio huo wa huyo Mwendazake..
 
Ulitaka nae awe mlalamikaji au asubiri michakato.? Yawezekana ni wewe uliyekuwa haupendezwi na maamuzi ila zile nyomi zilizokuwa zinajaa barabarani zilikuwa zinafurahishwa namna matatizo yanavyomalizwa papo kwa papo ama basi mchakato wa kuyashughulikia uwe wa uhakika badala ya kusubiri michakato.

Kuna vitu havihitaji michakato mzee.
 
Umejidhalilisha sana uliposema Jiwe alikuwa anajua idadi ya samaki, ajue idadi ya samaki ila hajui hata marais wa nchi maarufu.
Hilo swali mwulize Kikwete hapa kuanzia dakika ya 11
 
Mwulize Kikwete hapa kuanzia dakika ya 11

 
Ni indicator ya kiongozi kuwa informed na kuwa effective katika maamuzi yake...Wengi ni wavivu, hawasomi, hawatafuti taarifa wanasubiri zije mezani kwao na husingizia ushirikishwaji...Kwnai sote si mashaidi zile ngonjera za njoo kesho rudi Juma fulani si ziliisha? Why? Kwakua alikuwa mfano hai wakutolaza cases za watu bila kuzishughulikia...Wengi wa watanzania wanapenda umangi meza ndiyo sababu wanaona alikuwa hajui afanyalo
 
Nadhani ulikuwa humfahamu Magu vizuri wewe,ile style yake ndio inafaa zaidi na yenye matokeo kwenye taifa linalokuwa kama hili.

Kwanza mpe heshima yake kama kiongozi mwenye ujasiri wa kusimama popote pale hasa vijiji vya njiani kusikiliza kero za wananchi na mkutano kwenda live Tanzania nzima ambapo shida za kijiji hicho inaweza kuwakilisha matatizo ya vijiji kama 10000 Tanzania hii.
Na ambalo hulikuwa hulijui ni kuwa huyu mzee alikuwa anatembea na viongozi wa ngazi zote kuanzia mkoa mpaka kijiji na kabla ajatoa hukumu alikuwa anaitisha viongozi wote ambao walipaswa kuwajibika kwenye hiyo kadhia.

Nenda youtube kapitie kesi moja ya kisima cha maji huko wilaya ya kongwa Dosoma ya mheshimiwa aweso uone jinsi viongozi wenye dhamana walivyo wazembe mpaka ikamlazimu mheshimiwa waziri atoe hukumu pale pale mbele ya wananchi maana inatia hasira ukiangalia jinsi wananchi wanavyokosa huduma ya msingi kwa uzembe wa kipumbavu wa watu wachache waliokabidhiwa dhamana hiyo.

Mwisho najua umeandika hili kuwafurahisha mabwana zako kumendea teuzi ila sijapenda kumlinganisha hayati Magufuli hapa,nikukumbushe kusimama kusikiliza,na kutatua kero za watu ambao sio hata ndugu zako huo ni wito sio kila binadamu au kiongozi anazaliwa nao,usikute hata wewe mtoa mada kukaa na ndugu zako kusikiliza shida zao pasi na kuwasaidia kifedha hata kuwapa ushauri tu mawazo courage hiyo huna sasa tukikupa uongozi utaruhusu watu wapenye ofisini kwako waje walie shida zako.

Kama hukunufaika na uongozi wa Magufuli basi kuna maskini na wanyonge huko ndani ndani walipitiwa na baraka zake mpaka leo ndio hao wanamkumbuka na kumuombea huko aliko kwa sasa sema tu uwezo wa kuingia hapa Jf na kutoa ushuhuda hawana.

Uongozi wa kusikiliza na kutatua shida za wananchi wanyonge ni wito,na huu wito ni inborn character mtu anazaliwa nao.
 
Umeandika kwa mahaba makubwa sana uliyonayo kwa RIP Magufuli na unayo haki ya kuwa na maoni haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…