Rais Samia anasema 'hili tunalichukua'. Hayati John Magufuli aliamua pale pale jukwaani

Umeandika kwa mahaba makubwa sana uliyonayo kwa RIP Magufuli na unayo haki ya kuwa na maoni haya.
Tatizo lako umekurupuka huko na kimawazo chako finyu ukataka kuja kukileta hapa kuharibu image ya Rais Magufuli .

Kwa taarifa yako Magufuli ndio Rais wa pili wa Taifa hili kujulikana huko vijijini baada ya Nyerere.
 
Pole sana mkuu. Ninamheshimu Magufuli lakini haitonizuia kutoa maoni yangu kadri navyoona inafaa.
 
Tuseme sifa za “ujasiri” na “uthubutu” za JPM zimeshapoteza maana kwa mtazamo huu mpya?
Ujasiri na uthubutu haziwezi kuwa ni sifa zinazopitwa na muda. Japo zingetumika vyema zingeweza kuwagusa walio wengi kuliko zilivyowagusa nyakati za uhai wa JPM.
 
Mkuu, sifa hizo zilikuwa zijivumishwa kwa Magufuli bila “qualifications” zozote. Watoaji walikuwa wakiongeza “admiration” yao kwa kiongozi yule jinsi alivyokuwa na “msimamo usioyumba kwa kile anachoamini” bila ufafanuzi zaidi. Ndivyo makada wa CCM walivyokuwa wakimtukuza Magufuli.

Sasa naona msimamo wa Rais unapewa ufafanuzi wa kifalsafa na kimantiki kama ulivyoandika hapa. Ule ujasiri na uthubutu wa Magufuli unatolewa kasoro - kwamba unaweza kuwa ulikuwa na makosa katika baadhi ya nyakati. Hiyo ni qualification ya msingi.

Ukweli usemwe kuwa ule “ujasiri” na “uthubutu” wa Magufuli ulikuwa ni synonym ya UDIKTETA, period. No need to philosophize about the obvious. Haikuwa sifa ya uongozi makini. A clear line should be drawn between Magufuli and Samia instead of fuzzy elaborations. Unless they are the same.
 
hata haya ni maoni yako wewe binafsi, bora mwanaume aharibu kuliko mwanamke kwangu mimi
Yanabakia kuwa maoni yako binafsi pia. Mama Thatcher aliongoza Uingereza pengine wewe ulikuwa bado unaishi viunoni mwa Baba yako.

Ujerumani inaongozwa na mwanamke huu ni muhula wa pili na uchumi umetulia kama enzi za Kohl, badilika achana na mtazamo duni uliofilisika.
 
huwezi fananisha huko na Tanzania ndugu yangu, ina maana kuishi kwako kote hapa duniani...umeamua kufananisha inchi ya huko na hii ya hapa kwetu kiasi kwamba uamini mwananmke anaweza tawala hapa hadi akastawisha nchi?...kuwa makini sana inawezekana unataka ujaribu kuficha ukweli hadharani
 
Mwanamke anatawala hivi tunavyoandika, wewe unasema hawezi kutawala!. Tulia mkuu naona unajipatia maumivu ya kichwa yasiyo na ulazima.

Rais wa Burundi katoka kwao kaja kumuona, wewe unapiga makelele jamii forum!. Ndio tunae mpaka 2025 ikiwezekana ni mpaka 2030.
 
ndio akili zenu zilipoishia hapo, Kaja kuangalia fursa apige hela huyo. Mwanamke hakuna lolote na watakuja sana kujipigia hela hapa. hata akikaa maisha akae tu....ila hakuna kitu pale
 
Anapopiga hela wewe unaumia moyoni?. Yaani na akili zako timamu unaumia sana mwenzako anapopiga pesa?.Akili zile zile za kilofa za kiafrika. Riziki ya mwenzio usiilalie mlango wazi, sijui kama msemo huo ulifundishwa shuleni au ulikuwa bado haujazaliwa.

Mama ni mjanja sana, kitu kizuri anakijua vyema. Katoa ruhusa mgodi wa Kabanga Nickel uanze kuchimbwa, ni jukumu letu watu wa Ngara kuanza kushughulika na mradi. Na ipo miradi mingine mingi anayotoa kibali ianze kuzalisha mali.

Wewe unaendekeza dharau za kipuuzi zisizo na kichwa wala miguu hapa Jamii Forum.
 
Kuna hasara nyingi sana za kuhukumu hapo hapo endapo tu jambo hilo halina haja na ulazima wa kuhukumu hapo hapo.

Kuhukumu hapo hapo kuna madhara makubwa kwa sababu mara nyingi mtu anahukumu kwa utashi na kufurahisha kundi fulani na pengine ukamkosesha haki mtu mwingine.

Mama samia alipojibu hoja ya chato kuwa mkoa alijibu kwa hekima sana kwamba vitaangaliwa vigezo kama vitakidhi basi chato utakuwa mkoa.

Hekima iliyoje kwa mama yule,pale alijua fika kwamba akijibu moja kwa moja chato kwamba itakuwa mkoa atawafurahisha sana wana chato msibani na angewafariji zaidi,lakini jibu halikuwa na ulazima wa kutolewa pale pale kwa sababu baadae utakuja kuonekana muongo.

Hivyo mama yetu raisi haoni haja ya kuhukumu hapo hapo kwa sababu kwanza kesi nyingi ambazo zinahukumiwa hapo hapo hazina ulazima wa kuhukumiwa,lakini pia zinakuwa na hukumu za mihemko mara nyingi hivyo mama anaona bora ajiepushe nazo.

Hekima na kufikiria kwanza kisha ndipo unajibu.
Tabia ya magufuli ya kuhukumu hapohapo aliambukizwa Lukuvi kwenye kutatua migogoro ya ardhi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Ipo tofauti nimeiona ndani ya miezi saba tangu JPM aage dunia na Rais Samia apewe nchi. Tofauti ya uwezo wa kusikiliza na kufanya maamuzi yenye mizania sahihi. JPM hakubarikiwa busara za utatuzi wa matatizo mengi ya kiutekelezaji japokuwa alikuwa na sifa ya utatuzi huo. Hayati JPM alipenda kuamua suala pale pale jukwaani yaani muda ule ule alipokuwa ndio kwanza kalifahamu.

Rais Samia anaukwepa huu mzigo wa lawama ya wananchi. Hana pupa ya maamuzi na hutumia busara ya kusema 'mimi na wasaidizi wangu hili tunalichukua na tunakwenda kulifanyia kazi'. JPM aliamua muda ule ule, matokeo yake baada ya siku kadhaa kupita yale maamuzi yanakuwa yakifahamika kuwapendelea baadhi ya watu na kuwaumiza wengine. Baada ya siku kadhaa kupita inakuja kujulikana kuwa maamuzi yameegemea upande mmoja badala ya kuwa ni ya haki. Hulka hii ilisababisha baadhi ya watendaji serikalini kumuogopa Hayati JPM.

Na wengine hawakumuogopa bali walianzisha tabia ya kuharibu kazi makusudi ili wamuachie ofisi ateue watu wengine anaoona wanafaa kupewa ofisi. Rais Samia anakubali kutumia muda mrefu kupata utatuzi wa matatizo akijiridhisha na maamuzi yatakayofikiwa baada ya kulitazama suala husika kwa pande zote mbili. Unaweza kudhan ni udhaifu kumbe ni sifa ya uongozi, kuepuka kuleta mifarakano miongoni mwa watu wako wa karibu.

Kwani udhaifu wa tabia ya maamuzi ya jukwaani ni kiongozi kuwa wapendwa zaidi wanaoaminiwa na yeye na wapendwa wa kawaida tu. Watu wasioogopa wala kuona aibu ya kuwaharibia wenzao walio wengi kwa sifa ya muda mfupi tu.

Rais Samia ameonyesha utulivu wa kufanya maamuzi. Hajaonyesha pupa wala hasira pale anapochokozwa, mfano alichokifanya Baba Mchungaji Gwajima kingeweza kabisa kuiamsha hasira ya Samia lakini akatulia kama hakuna linalotokea. Aliweza kuonyesha ukomavu wa kiuongozi kwa kuweza kuistahimili misukosuko ya kisiasa kwa utulivu mkubwa.

Hayati JPM alipendwa kwa kusimamia haki za wananchi lakini upande mwingine wa sifa hiyo ulimpatia maadui haswa miongoni mwa wale waliokwazwa. Rais Samia ameweza kueleweka pale anaposema 'hili tunalichukua'. Hataki kufanya maamuzi halafu yakaleta msingi mbaya (precedent) wa siku zijazo.
Uzi huu hutamwona kipara kipya,p mayalla,wala bia yetu.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Uongozi ni kuamua tu kuchukua njia unayopita, unapita unaenda zako bila ya kujali kelele za kutoridhika au vigelegele vya kuridhika.....,miaka yenyewe mingapi ya uongozi ya kuridhisha wote!!

Maamuzi ya papo kwa papo yana uwezekano mkubwa wa kukosea kunakotokana na kukosa taarifa sahihi na mwisho wa siku mtu anaonewa (nina uhakika katika kila maamuzi natano ya papo kwa papo, mawili yanakuwa sivyo). Faida ya hii ni kuwa watu ni kweli wanakuogopa na hujitahidi kuwa 'sio wao' ili kubaki salama

Style ya mama ya 'kulichukua' ina uwezekano wa kutenda haki lakini ina shida ya kuchelewa na......nchi ni kubwa sana yatachukuliwa mangapi miaka yenyewe mitano au 10 tu!

Suluhisho: nenda tu na unachoamini ni sahihi!
Wewe siyo kiongozi,naamini kama unafamilia basi itakuwa hovyo sana hiyo familia.

Nchi haijengwi na mtu mmoja wala na awamu moja tu.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Wote wanaweza kuwa sawa..
Wote wanaweza wasiwe sawa..
Mmoja anaweza kuwa sawa na mwingine hapa.

Taifa la Tanzania na watu wake kuna mahala linamtaka Marehemu JPM na hulka yake ileile..
Hii nchi kuna baadhi ya watu wajinga sana, narudia tena wajinga sana na ndio wanasababisha hii nchi iwe hapa kwa sasa..

Wakati huu Taifa linahitaji mtu kama marehemu atuvuruge sana na tukija kukaa sawa miaka mingi mbele ndio waje viongozi aina hii ya Mama , pamoja na JK... Style ya uongozi wa mipango na kuamini watu inafaa sana kwenye mataifa yaliyoendelea tayari lakini sio kwa Taifa kama hili lenye baadhi ya watu primitive na wajinga...
Aina ya kiongozi wa kutuvuruga kujenga mbili zinazoelekea upande mmoja, Hiyo ni akili?

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Sio tu kutumbuliwa hadharani, bali kuna watu wanahitaji viboko kabisa...
Unajua watanzania tuna shida sana hivi Huyu mama kwa akili hawa wapuuzi isiyochambua mambo akiwaambia wakusanye mabango atayafanyia kazi maana yake nini? Yaania aliyesababisha tatizo kama la kula hela za kituo cha afya au shule ndo anaambiwa akusanye mabango atayafanyia kazi! Mama huyu yupo tu kikatiba ila uwexo mdogo!
 
Usimpambe, uwezo huo wa kufanya maamuzi yenye tija na sahihi kwa muda mfupi Samia hana! Magu ni namba nyingine, usijaribu kulinganisha na photocopy iliyoishiwa wino!

Back
Top Bottom