Rais Samia apokea Ripoti za CAG na TAKUKURU za Mwaka 2021/2022
Zamani kidogo hizo report ingezikuta jamiiforumu hata kabla ya kuwasilishwa kwa Rais , jamiiforumu ya sasa mpaka muda huu ni donoa donoa tu report full hakuna.

Mwenye nayo aweke hapa

USSR
Hizo zamani ni lini?
 
Hakuna kitu, hiyo imesha toka. Wezi wanaambiwa ' watupishe, hawafai'! Zaidi ya Rais Mwinyi alie jiuzuru wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani, nani mwingine? Hatuna utamaduni huo. Vinginevyo wizara inayo miliki uwanja wa mkapa kwa tukio la jana leo waziri husika angesha achia ngazi. Wizi wa pesa za umma ni jadi ya taifa la jamhuri ya kambale.
 
Kuna vitu vingine unasoma huku unaumia sana moyo

Pesa za Walipa kodi zinaliwa tu HOVYO na serikali ipo

Sioni sababu ya Raia wa nchi kuwaacha hawa wote waliohusika na upotevu wa fedha zote hizi

Nchi imekuwa shamba la bibi

Sasa Rais Samia Suluhu Hassan atumie makali yake hapa tumwone.
 
Hakuwa akijua wezi wa tanzania wasivyo na soni wala haya ya uso.
Mbongo ana uwezo wa hata kuiba mafuta ya gari ya rais wakiwa katika msafara mikoani.
Siku moja waibe lisimame njiani wafuate na kidumu.😂️😂️😂️😂️
 
Back
Top Bottom