Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aanatarajiwa kuzungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Nchini, leo Jumanne Januari 3, 2023.

Mazungumzo haya yanafanyika Ikulu, Magogoni - Dar es Salaam.


VIONGOZI WAWASILI
Viongozi mbalimbali wa vyama wameshawasili ukumbini, wakiwemo Freeman Mbowe na John Mnyika (CHADEMA), Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), Abdulrahman Kinana na Daniel Chongolo (CCM), Profesa Lipumba (CUF), Hashim Rungwe (CHAUMMA), John Cheyo (UDP), Joseph Selasini (NCCR Mageuzi).

KUMBUKUMBU KIKAO KILICHOPITA
Kumbuka kuwa Rais Samia alishakutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Dodoma, Desemba 2021 katika mkutano wa vyama na wadau wa siasa lakini vyama vya CHADEMA na NCCR-Mageuzi viliususia.

MAZUNGUMZO BAADA YA KUKUTANA NA MBOWE
Mazungumzo haya yanafanyika zikiwa zimepita siku mbili baada ya Rais Samia kuzungumza na Mbowe, mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, ikiwa ni wakati huohuo Rais Samia alipokuwa akipokea taarifa ya maridhiano baina ya CCM na Chadema yaliyodumu takriban miezi minane.
Hivi mbona anagoma kwenda Dodoma!??
 
Viongozi mbalimbali wa vyama wameshawasili ukumbini, wakiwemo Freeman Mbowe na John Mnyika (CHADEMA), Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), Abdulrahman Kinana na Daniel Chongolo (CCM), Profesa Lipumba (CUF), Hashim Rungwe (CHAUMMA), John Cheyo (UDP), Joseph Selasini (NCCR Mageuzi).
Hamna kitu humo... Washalamba asali hao.
 
Mbowe kwa sasa anaeleweka sana, kaonyesha ukomavu wa kisiasa ila tatizo bado genge lililo mzunguka hawataki kubadilika!!! wanadhani siasa ni uadui!
wanadhani siasa ni ukorofi na kupwayuka!!

Mbowe anao wajibu wa kuwaelimisha walio mzunguka.

wanasiasa hawapaswi kulazimisha mambo wanayo yataka wao bali wanapswa wakubali pia hoja za chama kinacho tawla.
Kama sio uadui kwanini watu wanapigwa risasi wengine wanatekwa na kupotezwa... fahamu siasa zetu ni vita kwasababu watu hawataki kutoka kwenye mamlaka kwa maslai yao.
 
TangaZo mbona haliko sawia Sasa mbona atujulishwi kama Rais nae kaisha fika?
 
huu ndio utamaduni wa watanzania.
siasa sio uadui bali siasa ni kushindanisha hoja kwa wananchi.
pia sio sahihi kulazimisha hoja yako ndio ikubalike isipo kubalika unasusa!! huko ni kutokukomaaa kisiasa.
 
HUYU MAMA YETU HUYU... YAANI WATU HAWANA HATA HABARI NAE YANI... TANGAZO LINALOMHUSU HATA HALISISIMUI... ZAIDI YA KUZIDI KUTIA HASIRA TU...

KWA SABABU HATA UKISEMA UKAMSIKILIZE ATASEMA NINI... HAKUNA LA MAANA.
 
Hauwezi kutumia nguvu kushindana na mwenye nguvu. CCM wameshika mpini, wapinzani wameshika makali, so wapinzani (walioshika makali) wakilazimisha kuvutana na CCM (walioshika mpini) ni wao wapinzani ndio watakaochanika mikono.

Cha kufanya ni kwenda hivi hivi mdogo mdogo huku wanarekebisha dosari ndogo ndogo.

Usiamini sana katika vurugu maana utaishia kuumia au kufungwa jela. Hata uhuru kuna nchi ambazo zilidai uhuru bila kumwaga damu, watu walikaa chini waka negotiation wakakubaliana uhuru ukapatikana.

Siasa za kukimbizana na mapolisi barabarani zimeshapitwa na wakati. Watu wanahitaji kutafuta suluhu kwa njia za amani ili nchi iendelee kuwa na amani, umoja na mshikamano.
Umeongea ukweli mtupu🤝

Hata wale wanaombeza Mheshimiwa Mbowe aliyeyakubali Maridhiano hayo na kuyaendeleza, niwaulize swali Moja tu, je chama Cha Chadema kilipotangaza UKUTA, wakati ule, ni wangapi walijitokeza mabarabarani Ili wapigwe virungu na Jeshi la Polisi?😎
 
Hivi mbona anagoma kwenda Dodoma!??
kufanya nini Dodoma kikifanyika dar kuna ubaya gani tambua bado dar ili umuhimu mkubwa sana rais kuwa pale karibu benk kuu ipo pale bandari ipo pale wafanya biashara wakubwa wapo dar viwanda vikubwa vipo pale hivyo mikutano muhimu ya uchumi pale ni muhimu dodoma vikao vya vyama na bunge sawa
 
Kete zinasukumwa kama zilivyotarajiwa mkuu?

Sent from my SO-01J using JamiiForums mobile app
Ndio,zinasukumwa pole Pole!!

Naona maridhiano yataleta katiba Mpya Muda SIO MREFU!

HALAFU makubaliano ya kutokuwa na uchaguzi 2025 Hadi katiba ipatikane!! Nadhani ni ajenda pia ya maridhiano japo covid-19 Ndio inatesa Mwenyekiti hadi SASA!

Lazima waone Namna ya KU dump hii ishu na kuifufua tena!

Tunaekea pazuri!
 
"Wakati mnanikabidhi kuongoza taifa hili busara zilinituma jinsi nilivyolipokea taifa hili kwamba ipo haja ya kufanya taifa liwe kitu kimoja" "Nikasema ili taifa liwe moja lazima tuwe na maridhiano na kwenye maridhiano sisi vyama vya siasa tunawawakilisha wananchi wa Tanzania ndio wenye sauti zao nikasema tuwe na mazungumzo ndani ya vyama vya siasa".- Ameongeza Rais - Rais Samia Suluhu Hassan

Katika mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya maridhiano ilikua ni Kufunguliwa kwa mikutano ya hadhara ambapo kwa sasa marekebisho ya sheria yanafanyiwa kazi ili kuwa na muongozo sahihi.

Lakini leo niko hapa kutangaza Mikutano ya Hadhara ni haki ya vyama vya siasa kwahiyo uwepo wangu mbele yenu leo ni kutoa ruhusa, kuja kutangaza kuwa lile tangazo la kuzuia mikutano ya Hadhara linaondoka.

Jukumu la Serikali ni kutoa ulinzi na nyinyi nendeni mkafanye siasa za kistaarabu, Sisi tuko tayari kukoselewa.
 
Awamu ya tano ilizuia mikutano ya kisiasa kwakuwa ilijaza madomo zege ndani ya chama, watu wasioweza kujenga hoja na kujibu hoja makini za vyama vya upinzani.
 
Back
Top Bottom