Rais Samia arusha dongo kwa Lissu, asema kashfa na matusi kwenye mikutano ya hadhara ni kwasababu ya kuzungumzwa hakuna

Sasa mmejibiwa tu mjue tu kuwa sheria zipo aliyekamatwa na kuachiwa kwa dhamana ni kwa kuwa alikuwa amevunja sheria na sio politically motivated kwa hio kama mkuu anawakumbusha wanasiasa wenzake wafanye siasa na sio kuvunja sheria .
Alivunja sheria gani?

Ukiitaja sheria Aliyovunja kikatiba na kutumilia vocha ya 10000.
 
Sasa mmejibiwa tu mjue tu kuwa sheria zipo aliyekamatwa na kuachiwa kwa dhamana ni kwa kuwa alikuwa amevunja sheria na sio politically motivated kwa hio kama mkuu anawakumbusha wanasiasa wenzake wafanye siasa na sio kuvunja sheria .
Na yeye asitumie mitutu ya bunduki kujibu hoja
IMG-20200121-WA0012.jpg
 
Sasa mmejibiwa tu mjue tu kuwa sheria zipo aliyekamatwa na kuachiwa kwa dhamana ni kwa kuwa alikuwa amevunja sheria na sio politically motivated kwa hio kama mkuu anawakumbusha wanasiasa wenzake wafanye siasa na sio kuvunja sheria .
Kuna mtu ambaye hajui kwamba sheria ipo?hao anaowakumbusha ndio waalimu wa sheria wenyewe anawakumbusha nini?
 
By the way hao wanaosikiliza wanasikiliza nini ? (Ukimya)

Na matusi ni subjective unachosema matusi kwako huenda mwingine anaona unaambiwa ukweli.., Binafsi kwangu mimi matusi na kashfa ni kuambiwa mtu anaupiga mwingi wakati kiuhalisia mambo sio mambo (Hawa watu kwangu mimi wana-insult my intelligence)
Yeye mbona ni mtukanaji mzuri tu,alimwambia Professor Mkenda nonsense
 
"Tumeruhusu mikutano ya hadhara tukiwa na nia vyama vya siasa vizungumze, wananchi wasikie sera zao, mipango yao, mada zao ili vyama vikue na virudishe wale waliowapoteza. Viweze kurudisha, vyama visimame viwe madhubuti tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha na ndio maana ya kutoa fursa hii ya mikutano ya hadhara.

"Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashifu, watu wakasimame kuchambua dini za watu, lakini sishangangai kwanini haya yanatokea kwasabbu ya kuzungumzwa hakuna!.

"Tulianza oh na katiba, tukaenda ikakatika katikati... bandari, imeenda ah sasa imerudi tena katiba, inapokuwa hakuna na unalazimisha lazima ufanye jambo utazungumza yasiyokuwepo au yasiyo katika muelekeo huo." -
Rais Samia
Leo nikiwa kijiweni kwa fundi viatu nimesikia Wamasai wameamua kurudi kwao na kama mbwai iwe mbwai tu
 
wana kura nyingi kiasi gani? CCM iliwahi kuwambia wasomi wote waende huko na vitisho vyao,wakaenda na ikashinda
wakaja walimu, wakaambia kura zao wanaweza kumpa yeyote wanayemtaka, wakaenda na ikashinda
wakaja madaktari,ikla kwao
wachagga ikala kwao
masai ndio nani sasa?
 
Sasa mmejibiwa tu mjue tu kuwa sheria zipo aliyekamatwa na kuachiwa kwa dhamana ni kwa kuwa alikuwa amevunja sheria na sio politically motivated kwa hio kama mkuu anawakumbusha wanasiasa wenzake wafanye siasa na sio kuvunja sheria .
Kwa hiyo kuuza bandari za Tanganyika na kuacha za Zanzibar siyo kuvunja sheria?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kule ngorongoro mliongelea mafuta?
Kwani walienda? Kila mahali na hoja zake kwa kuwa kuna matatizo yanauma zaidi sehemu fulani kuliko sehemu nyingine. Ukienda Loliondo zungumza sera zinazowahusu, ukienda dsm zungumza sera za jiji. pia kuna yanayohusu nchi nzima kwa ujumla.
Mimi namshauri Rais kuwa asihangaioke nao, sisi wananchi tunaowasikiliza tutawahukumu sisi wwenyewe, yeye ashughulike na kutekeleza sera za Chama
 
Kuna mtu ambaye hajui kwamba sheria ipo?hao anaowakumbusha ndio waalimu wa sheria wenyewe anawakumbusha nini?
Hata mwalimu kuna wakati na yeye anakumbushwa afate kile anachofundisha asijisahau akadhani ni kwa ajili ya wengine tu
 
Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashifu, watu wakasimame kuchambua dini za watu, lakini sishangangai kwanini haya yanatokea kwasabbu ya kuzungumzwa hakuna!.
Hivi wanaovunja sheria na hao wanafisadi raslimali za nchi au wale wanaopinga ufisadi huu?
Sidhani kama kuambiwa ukweli ni dhambi! Mwizi aitwe mwizi na muungwana aitwe muungwana.
 
"Tumeruhusu mikutano ya hadhara tukiwa na nia vyama vya siasa vizungumze, wananchi wasikie sera zao, mipango yao, mada zao ili vyama vikue na virudishe wale waliowapoteza. Viweze kurudisha, vyama visimame viwe madhubuti tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha na ndio maana ya kutoa fursa hii ya mikutano ya hadhara.

"Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashifu, watu wakasimame kuchambua dini za watu, lakini sishangangai kwanini haya yanatokea kwasabbu ya kuzungumzwa hakuna!.

"Tulianza oh na katiba, tukaenda ikakatika katikati... bandari, imeenda ah sasa imerudi tena katiba, inapokuwa hakuna na unalazimisha lazima ufanye jambo utazungumza yasiyokuwepo au yasiyo katika muelekeo huo." -
Rais Samia

Chadema imeitwa ni MIJITU
 
Back
Top Bottom