Ni Rais pekee ambae watanzania wamemkataa wazi wazi.
Sio kwa sababu ya Udini( tuliwahi kuwa na rais waislam na hakukuwa na shida yoyote) , Ukabila au Jinsia kama inavyoenezwa kwa propaganda.
Wengi wamemkataa Samia kwa kigezo cha Competency na Uzalendo. Watanzania wanaamini nchi yao ipo kwenye majaribio na kwa sasa nchi inaendeshwa na WAHUNI, huo ni ukweli mchungu.
Huu ni ukweli ambao Samia ataingia nao kaburini.
1. Hakuwahi kuchaguliwa na wananchi kwa ridhaa yao kwa awamu zote mbili
2. Samia ni rais pekee ambae amebeba historia mbaya ya Tanzania , ni historia ya kipekee tangu TZ iumbwe na mbaya zaidi ameiandika hii historia kipindi cha technology and digital transformation, in the near future …. Hata familia yake itaathirika na hii historia
3. Ni Rais pekee ambae baada ya mauti yake, nyuma ataacha vitabu, documentary hata movies zitakazoelezea ubaya wake na ukatili ambao kwa asilimia kubwa umechangiwa na INCOMPETENCY , : sidhani kama ataipenda hii historia.
I feel so sad for her - Sidhani kama alitamani iwe ilivotokea. It is all about incompetency, smart leaders would never let that happen. Unawezaje kufanya massacre kwa wananchi unaowaongoza ….. very strange. Akili ni kitu muhimu sana
The worst part ni kwa miaka 4 iliyobaki ( kama mungu atampa kibali cha pumzi zaidi) hakuna atakachoweza kufanya cha kuleta maendeleo, kwa sasa ni anazuga zuga tu hakuna maendeleo atakayofanya kwa sasa , watanzania wamemkataa, na wataendelea kumkataa : now yupo kwenye survive of the fittest, it is sad but true ….: ni rais pekee atakaekuwa amekaa madarakani bila maendeleo yoyote.
4. Samia amekwenda kusafisha historia ya JPM na kumfanya kuwa the best president in our history, ni Rais pekee within 5 years amefanya mambo ambayo watanzania akiwemo na Samia wanaendelea kunufaika nayo, that was prophetic kwa kweli.
Dr. Megalodon Mushi
Ottawa, Canada
Rue 52
Kama aliyeandika haya ni PhD holder, basi nchi ina wasomi utumbo wasio na mfanowe. Rais anayewabadilishia mfumo wenu wa elimu wa kikoloni ulioleta graduates wengi wasio na ujuzi unaohitajika mtaani na kuwawekea mfumo wa elimu ujuzi kivipi hafai. Rais huyo ndiye aliyemaliza ujinga wa "second selection" kwa watoto wenu kwenda secondari kwa kuwajengea shule mpya 400, na madarasa ya kisasa maelfu kwa ma elfu. Ukitoa mkoloni na Nyerere kidogo, hakuna Rais aliyewajengea madarasa yenye huduma zote za unadhifu. Leo anakuwaje incompetence?
Rais aliwajengea shule za kisasa za vipaji kwa wanawake 26. Idadi kubwa ya shule za aina hiyo kuwahi kujengwa Tanzania tangu Uhuru. Huyu anakuwaje incompetence?
Samia ndiye Rais pekee kujenga vyuo vikuu au kampasi nyingi kwa wakati mmoja kuliko Rais yoyote? Mikoa ya Kagera, Tanga, Sumbawanga, Katavi, Kigoma, Lindi ambayo kwao chuo kikuu ilikuwa ni kwa picha sasa wanapata vyuo vyao vikuu vya Serikali. Huyu anakuwaje Rais wa hovyo Dr?
Tuna ukanda wa bahari takribani km 1424, ni Rais Samia pekee aliyefikiri vizuri kutumia fursa hiyo kwa kujenga bandari kubwa na ya kisasa ya uvuvi ili kutumia fursa ya bahari. Tangu Uhuru, hakuna Rais aliyejenga skimu za umwagiliaji za hekta nyingi kumzidi yeye kwa miaka yake minne. Ni Rais Samia ndiye aliyeboresha mifumo na vifaa vya kisasa katika hospitali hadi ngazi ya wilaya kuliko yeyote.
Kwa miaka nenda, Dar es Salaam imekuwa na kero kubwa tatu (umeme, maji na mafuriko ya jangwani). Amemaliza Stiglers Gorge, anajenga Daraja la Jangwani na Daraja la Mzinga kule Mbagala na pia anajenga Bwawa la Kidunda kwa ajili ya kurekebu kiwango cha maji ya mto Ruvu ili kufuta mgawo wa maji Dar kipindi cha kiangazi.
Tangu Uhuru, hakuna Rais aliyesomesha madaktari wengi kwa pamoja kuliko yeye kupitia Samia Scholarships.
Kwa miaka mingi, Barabara ya Morogoro hadi Dodoma imekuwa haipitiki kipindi cha masika. Ni Samia huyu amekenga maeneo korofi na kuinua maeneo yaliyokuwa na changamoto hiyo (kutoka Gairo hadi Dodoma). Huyo anakuwaje incompetence kwako?
Ni Rais Samia ndiye atakayeandika historia ya mapinduzi ya kilimo ya kutumia maji ya mto Rufiji kupitia ujenzi wa Mabwawa mawili ya umwagiliaji (Nyerere Annexes) unaoendelea huko Rufiji. Haya ni mbali ya Bwawa la sasa la Mwalimu Nyerere.
Tangu Uhuru, Tanzania imejenga uwanja mmoja tu wa kisasa wa michezo. Samia anakuwaje incompetence kwa kujenga viwanja vitatu vya kisasa kwa pamoja?
Rais anayejenga upya madaraja yote yaliyojengwa tangu mkoloni kwa Barabara ya Dar es Salaam Lindi anakuwaje incompetence?
Rais aliyerudisha makali ya bandari ya Tanga kiasi cha sasa hivi kupokea Melissa kubwa kubwa anakuwaje incompetence kwako?
Rais anayetaka kuifanya TAZARA irudi kwenye ubora wake, anakuwaje mbaya kwenu? Na kumbuka, haya yote yanafanyika bila kuharibu maisha ya watumishi wala wafanyabiashara wa kweli. Waathirika wakubwa wa uongozi wa Samia ni wenye wivu na chuki tu, si vinginevyo.
Kuhusu ya October 29, hayajafikis hata robo ya January 27 2001 kule Pemba. Kule kulikuwa ni habari nyingine, kiasi kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tulitengeneza wakimbizi kutoka Tanzania.
NB: Ukiwa msomi halafu ukiwa jealous unakuwa mpumbavu square.