Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,465
- 5,672
Kuna mengi makubwa na magumu sana ya kurekebisha.Sasa hivi wote washindwa kuamua ama wamuachie Tundu Lissu na kama kumwachia ni kwa namna ipi. Pia hata kama akina Humphrey Polepole bado wapo hai ni vigumu kuwaachia hivihivi kwa aibu na uoga.
Wamejiweka wenyewe katika mtego mgumu.
Dhambi ya kumwaga damu kiasi kile ni kubwa sana. Hakuna namna ya kusahihisha hilo kosa na kurejea hali iliyokuwepo kabla. Lazima hatua kubwa za “Kimapinduzi” (a radical move) zichukuliwe kuponya nchi.
Kwa sisi Wakristo, muuaji wa kwanza, Kaini, alipomuua ndugu, yake, Habili, Mungu alimuondoa mahali pake na kumtupa atangetange duniani kote!
Vivyo hivyo wote waliohusika na damu ya Oktoba 29+ hawana budi kuwajibika na kuondoka kabisa kwenye utawala na uongozi wa nchi. Lazima mabadiliko makuu yafanyike.
A TOTAL RESET is essential and necessary. Devoid of that, we’d continue living in a DOOMED and DAMNED country. We’ll soon join the wretched of the earth.