Rais Samia Ataishi na huu ukweli kwa maisha yake yote yaliyobakia hapa duniani

Mtu yupo hai na ana uwezo wa kurekebisha anapokosea ila akishindanishwa na marehemu bado marehemu anashinda πŸ˜‚
Correcting a wanton massacre of citizens? Then grabbing state power with impunity! That's quite a high bar. I really don't see her (or anyone, in that case) overcoming that - short of a heartfelt public confession, begging for mercy (self-humiliation) as well as submitting oneself to appropriate legal authorities for due process and penalty. A sure suicide move on her part.

Very sadly, she's at the point of no-return. Whoever pushed her there had sinister motives, for sure. I keep wondering who that person could be?!! And, most important, what's their endgame?
 
hizo ni thoughts zako binafsi
 
Alichaguliwa wa jeshi kwa % kubwa + wahuni waliopewa cheo kwenye kitume cha kihuni cha uchaguzi na wananchi wachache sana wenye matatizo ya akili
Basi kamtoeni mumuweke Kitima au Pengo 🀣🀣🀣
 
Mkuu, binafsi nipo Bongo lakini sijui Samia ameleta maendeleo gani Tanzania tangu aingie madarakani.

Zaidi ya yote naona ameongeza utekaji, utesaji na mauaji..

Ameongeza deni la Taifa kutoka 57 trillion mpaka 107 trillion.

Katka utawala wake amesababisha Mfumko wa Bei... Kabla yake kipande Cha sabuni kilikua 200 lakini saivi ni 700 Tsh.

Anyway huenda nina roho ya chuki na wivu ndiyo maana sioni maendeleo aliyo yaleta...

Unaweza angalau kutaja miradi miwili ya maendeleo aliyo izundua? Kabla ya ile iliyo achwa na mwenda zake?
 
Ameongeza mabango ya mama mikoa yote
 
HUNA akili. Utaona impact ya alichokifanya ndio utajua maana ya amiri jeshi.

Unadhani imeesha ? Akili ni kitu muhimu sana
Impact ya alichokifanya imesababisha kuonyesha kuwa Tanzania ni imara na haiwezi kucgezewa na vikaragosi walioko nje wanaolipwa na Ford Foundation.
 
Acha kumpangia ratiba Rais, wewe ni nani?
 
Sasa hivi wote washindwa kuamua ama wamuachie Tundu Lissu na kama kumwachia ni kwa namna ipi. Pia hata kama akina Humphrey Polepole bado wapo hai ni vigumu kuwaachia hivihivi kwa aibu na uoga.

Wamejiweka wenyewe katika mtego mgumu.
 
Kama aliyeandika haya ni PhD holder, basi nchi ina wasomi utumbo wasio na mfanowe. Rais anayewabadilishia mfumo wenu wa elimu wa kikoloni ulioleta graduates wengi wasio na ujuzi unaohitajika mtaani na kuwawekea mfumo wa elimu ujuzi kivipi hafai. Rais huyo ndiye aliyemaliza ujinga wa "second selection" kwa watoto wenu kwenda secondari kwa kuwajengea shule mpya 400, na madarasa ya kisasa maelfu kwa ma elfu. Ukitoa mkoloni na Nyerere kidogo, hakuna Rais aliyewajengea madarasa yenye huduma zote za unadhifu. Leo anakuwaje incompetence?

Rais aliwajengea shule za kisasa za vipaji kwa wanawake 26. Idadi kubwa ya shule za aina hiyo kuwahi kujengwa Tanzania tangu Uhuru. Huyu anakuwaje incompetence?

Samia ndiye Rais pekee kujenga vyuo vikuu au kampasi nyingi kwa wakati mmoja kuliko Rais yoyote? Mikoa ya Kagera, Tanga, Sumbawanga, Katavi, Kigoma, Lindi ambayo kwao chuo kikuu ilikuwa ni kwa picha sasa wanapata vyuo vyao vikuu vya Serikali. Huyu anakuwaje Rais wa hovyo Dr?

Tuna ukanda wa bahari takribani km 1424, ni Rais Samia pekee aliyefikiri vizuri kutumia fursa hiyo kwa kujenga bandari kubwa na ya kisasa ya uvuvi ili kutumia fursa ya bahari. Tangu Uhuru, hakuna Rais aliyejenga skimu za umwagiliaji za hekta nyingi kumzidi yeye kwa miaka yake minne. Ni Rais Samia ndiye aliyeboresha mifumo na vifaa vya kisasa katika hospitali hadi ngazi ya wilaya kuliko yeyote.

Kwa miaka nenda, Dar es Salaam imekuwa na kero kubwa tatu (umeme, maji na mafuriko ya jangwani). Amemaliza Stiglers Gorge, anajenga Daraja la Jangwani na Daraja la Mzinga kule Mbagala na pia anajenga Bwawa la Kidunda kwa ajili ya kurekebu kiwango cha maji ya mto Ruvu ili kufuta mgawo wa maji Dar kipindi cha kiangazi.

Tangu Uhuru, hakuna Rais aliyesomesha madaktari wengi kwa pamoja kuliko yeye kupitia Samia Scholarships.

Kwa miaka mingi, Barabara ya Morogoro hadi Dodoma imekuwa haipitiki kipindi cha masika. Ni Samia huyu amekenga maeneo korofi na kuinua maeneo yaliyokuwa na changamoto hiyo (kutoka Gairo hadi Dodoma). Huyo anakuwaje incompetence kwako?

Ni Rais Samia ndiye atakayeandika historia ya mapinduzi ya kilimo ya kutumia maji ya mto Rufiji kupitia ujenzi wa Mabwawa mawili ya umwagiliaji (Nyerere Annexes) unaoendelea huko Rufiji. Haya ni mbali ya Bwawa la sasa la Mwalimu Nyerere.

Tangu Uhuru, Tanzania imejenga uwanja mmoja tu wa kisasa wa michezo. Samia anakuwaje incompetence kwa kujenga viwanja vitatu vya kisasa kwa pamoja?

Rais anayejenga upya madaraja yote yaliyojengwa tangu mkoloni kwa Barabara ya Dar es Salaam Lindi anakuwaje incompetence?

Rais aliyerudisha makali ya bandari ya Tanga kiasi cha sasa hivi kupokea Melissa kubwa kubwa anakuwaje incompetence kwako?

Rais anayetaka kuifanya TAZARA irudi kwenye ubora wake, anakuwaje mbaya kwenu? Na kumbuka, haya yote yanafanyika bila kuharibu maisha ya watumishi wala wafanyabiashara wa kweli. Waathirika wakubwa wa uongozi wa Samia ni wenye wivu na chuki tu, si vinginevyo.

Kuhusu ya October 29, hayajafikis hata robo ya January 27 2001 kule Pemba. Kule kulikuwa ni habari nyingine, kiasi kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tulitengeneza wakimbizi kutoka Tanzania.

NB: Ukiwa msomi halafu ukiwa jealous unakuwa mpumbavu square.
 
Sasa jiulize kwanini wote walisema hakuna kuandamana na vitisho vya mazoezi ya majeshi juu.
Wakati wa JPM watu walitii hawakujitoa muhanga.
Wakati wa SSH hawakutii waliojitoa muhanga walijua watapigwa, watafungwa au watauwawa?
TUMIA AKILI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…