Rais Samia atakumbukwa kwa kujenga uchumi unaowagusa Watanzania

Acheni pambio, Mama anatuweka kwenye hali mbaya zaidi deni lenyewe tu ndani ya mwaka mmoja linatisha na bado anadai mitano tena miradi mkakati inasuasua ilikuwa sasa hivi bwawa limemalizika na Maji yanajazwa, reli inasuasua.
Watu hawampi ukweli hali mbaya manunguniko ni mengi. Kama ana mizania namshauri asihangaike na mitano tena.
 
Mpongeze wewe na ukoo wako inatosha.!
Mimi na ukoo wangu na watanzania wengi tunaendelea kumpongeza mh Rais wetu kwa kazi kubwa anayofanya, huku niliko tayari mbolea ya Ruzuku umeshapika, huku Ni pongezi tu kwa mh Rais wetu
 
Namba ya simu umesahau
 
Deni ni shilingi ngapi? Kwa bahati nzuri Rais wetu Ni mkweli katika kuongoza nchi yetu, watanzania tunajuwa kilichokopwa na kazi kilichofanya, Ndio maana tunaendelea kumuunga mh Rais wetu mpendwa, Angalia mfano jinsi mh Rais alivyo Jenga shule nzuri na vituo vya Afya vizuri utazani ulaya huku akiajiri na watumishi wa umma kwenda kuwahudumia na kuwatumikia watanzania kutokanaa na Fedha ambazo tulikuwa tumezipata

Mh Rais wetu anaendelea kugusa maisha ya watanzania kwa kutusogezea huduma karibu na makazi yetu
 
Mimi naweka Yale mazuri aliyofanya mh Rais wetu na namna watanzania wanavyoendelea kumuunga mkono mh Rais, huku niliko wakulima wanasema watafanya kazi ya kumpigia kampenii mh Rais ili asihangaike kuzunguka,

wamefurahishwa na namna mbolea za Ruzuku zilivyo wahi kufika hata kabla ya kuanza msimu mpya, wanasema hakika mh Rais Ni msikivu na amesikia kilio chao na kugusa maisha yao
Weka kwanza utanishukuru Badae
 
Mkuu sijui labda mi sijui. Je unajua Mama mtizamo wake hasi juu ya Dkt Magufuli umelighalimu hili taifa kwa kuwa na maisha magumu? Hiyo ni yake yeye Mama kama yeye. Sijui labda hapo baadaye. Ila kwa sasa Mama hajaleta unafuu zaidi ya kufanya bei ya mchele kubakia zaidi ya 2400 kwa kilo.
 
Unatia huruma na kinyaaa eti "mh rais wetu'" unajinyenyekesha kwa binadamu mwenzio, kuliko ata muumba wako ovyo kabisa
 
Unatafuta kazi au afu kumbuka unafiki ni dhambi
 
Chawa katika ubora wake
 

Wakulima sio watu wa kuwaamini sana

Wakati wa Jk alisifia Kilimo kwanza, wakati wa magu walisifia Sana na wakasema hakuna kama yy

Now wanasema mama ndio kila kitu

Usiwaamini sana
 
Hakuna ruzuku inayowekwa ila ni aina ya kutafuna pesa za walipa kodi kwa kisingizio kisichoaminisha chochote, ulaghai mtupu
 
Hata mbwa ula makombo ya bosi wake 🦮🦮🦮
 
Hata mbwa ula makombo ya bosi wake 🦮🦮🦮
Kazi anayoifanya mh Rais Ni kubwa Sana, Anastahili pongezi zetu , Anastahili kuungwa mkono, Anastahili kupewa faraja, Ameliheshimisha Taifa hili, amejenga umoja wa kitaifa, amewaleta watanzania kwa pamoja, amevunja uadui wa kivyama, ameijenga misingi ya kuelewana na kuaminiana,

Amefanya kila mtu ajisikie Anayo nafasi katika ujenzi wa nchi hii, Najivunia kuongozwa na mh Rais mama Samia suluhu Hassani Kama Rais wa nchi, Kama kijana na Kama mwananchi panapo majaliwa ya mwenyezi Mungu mtoa njia na maarifa, anayetoa uzima na kumjalia mtu Afya njema nitakuja kuwasimulia watu juu ya ushupavu wa uongozi wa mh Rais wetu aliouonyesha tangia aliposhika na kuapishwa katikati ya majonzi ya kuondokewa na Rais aliyekuwa madarakani na namna alivyoibeba nchi katika mabega yake bil kuteteleka,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…