Rais Samia atakumbukwa kwa kujenga uchumi unaowagusa Watanzania

Rais Samia atakumbukwa kwa kujenga uchumi unaowagusa Watanzania

Yani ni Umaku asee
Kuongoza nchi siyo sawa na kuongoza kondoo,,inahitajika hekima busara upendo na akili kubwa ya kimkakati na kujuwa ufanye Nini kuwainua watu kiuchumi, hiki ndicho afanyacho mh Rais wetu katika juhudi za kuyainua maisha ya mtanzania licha ya uchumi ulio yumba Dunia nzima
 
Kumlalamikia SSH ni kutudhihilishia uwezo mdogo wa kufikiri... yaani kuna la ajabu lipi unasetemea mama ataweza kufanya.... ni wa kumuonea huruma na kumwombea
 
Ndugu zangu, wanasema uchumi mzuri Ni ule unao gusa maisha ya watu wengi, ukimfuatilia vizuri mh Rais wetu utagundua kuwa Anajenga uchumi wenye kumgusa kila mtanzania.

Kwanza mh Rais ametambua kuwa kilimo ndio secta iliyo ajiri watanzania wengi wa makundi tofauti tofauti, Hivyo juhudi zozote za kuujenga uchumi wetu Ni sharti ukipe kipaombele kilimo, Ndio maana unaona ongezeko la bajeti katika wizara ya kilimo Na hata utoaji wa Ruzuku takribani billioni 150, hii inakwenda kuchochea uzalishaji, lakini pia kundi kubwa linakwenda kuguswa kupitia mipango hii ya Rais wetu mpendwa.

Mh Rais wetu Amedhamilia kuhakikisha kuwa katika kujenga uchumi wetu Hakuna mtu au kundi lolote linaloachwa nyuma au kusahaulika, Hali hii inajidhihilisha kwa namna anavyojenga miradi mbalimbali inayogusa maisha ya watu hasa wanyonge, ndio maana unaona miradi Kama shule, vituo vya Afya,zahanati,huduma za maji na umeme vikitamalaki kila Kona ya nchi hii.

Rais wetu pia anajitahidi kuhakikisha kuwa mfumuko wa Bei unaoikumba Dunia unapunguzwa kwa kuweka Ruzuku kwenye mafuta ambayo Ni injini ya uchumi wetu, ndio maana unaona akitoa karibu billioni Mia moja kila mwezi.

Rais Samia mama yetu Atakumbukwa Sana akimaliza uongozi wake 2030 kwa kujenga uchumi unaogusa watanzania hasa wakipato Cha chini, kazi ya serikali Ni kusaidia watu kunyanyuka kiuchumi, kazi ambayo mh Rais wetu anaifanya vyema Sana.

Mama hakika yupo kazini, Tunamuhitaji mama aendelee kututumikia Hadi 2030, ndio tutajuwa tufanye Nini akitufikisha hapo, kikubwa tunaendelea kumuombea uzima na Afya njema.
Poyoyo kazini.
 
Hii awamu hata ipewe miaka 100 haina maarifa ya kuifikisha tz ktk maendeleo zaidi inazidi kuiporomosha tz kiuchumi na kiumasikini, hata muipambe vip muisifie kwa nyimbo na mapambio hii awamu imefeli mazima... Itaishia kusema NA HILI MKALITIZAME
 
Naona

Naona umeishiwa hoja umeanza matusi, hata hivyo Mimi nawaheshimu hata ninao tofautiana nao mtazamo maana Naheshimu utu wa mtu, wewe Kama binadamu unastahili heshima na siyo kudhalilishwa utu wako

Mungu akupe hekima na moyo wa upendo, Mimi hata unitukane vipi siwezi nikafungua mdomo wangu Wala kuandika matusi hapa juu yako, Sina kisasi Wala chuki nawe, nitaendelea kuheshimu michango yako hata Kama sikubaliani nayo nitaichukulia Kama maoni yako binafsi
Uko vizuri
 
Ndugu zangu, wanasema uchumi mzuri ni ule unao gusa maisha ya watu wengi. Ukimfuatilia vizuri Mh. Rais wetu utagundua kuwa anajenga uchumi wenye kumgusa kila mtanzania.

Kwanza Mh. Rais ametambua kuwa kilimo ndio sekta iliyo ajiri watanzania wengi wa makundi tofauti tofauti. Hivyo juhudi zozote za kuujenga uchumi wetu ni sharti ukipe kipaumbele kilimo.

Ndio maana unaona ongezeko la bajeti katika wizara ya kilimo na hata utoaji wa ruzuku takribani billioni 150. Hii inakwenda kuchochea uzalishaji, lakini pia kundi kubwa linakwenda kuguswa kupitia mipango hii ya Rais wetu mpendwa.

Mh. Rais wetu smedhamilia kuhakikisha kuwa, katika kujenga uchumi wetu hakuna mtu au kundi lolote linaloachwa nyuma au kusahaulika. Hali hii inajidhihilisha kwa namna anavyojenga miradi mbalimbali inayogusa maisha ya watu hasa wanyonge.

Ndio maana unaona miradi kama shule, vituo vya afya, zahanati, huduma za maji na umeme vikitamalaki kila Kona ya nchi hii.

Rais wetu pia anajitahidi kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unaoikumba dunia unapunguzwa kwa kuweka ruzuku kwenye mafuta ambayo ni injini ya uchumi wetu. Ndiyo maana unaona akitoa karibu billioni mia moja kila mwezi.

Rais Samia mama yetu Atakumbukwa sana akimaliza uongozi wake 2030, kwa kujenga uchumi unaogusa watanzania hasa wakipato cha chini. Kazi ya serikali ni kusaidia watu kunyanyuka kiuchumi, kazi ambayo Mh. Rais wetu anaifanya vyema sana.

Mama hakika yupo kazini, tunamuhitaji mama aendelee kututumikia hadi 2030. Ndio tutajuwa tufanye nini akitufikisha hapo, kikubwa tunaendelea kumuombea uzima na afya njema.
Nzuri Sana hii
 
Kipi unachoona nilichozungmza ambacho hajakifanya mh Rais, hivi unafuatilia uchumi wa Dunia inavyokwenda, hivi unafuatilia Hali ya kimaisha katika nchi nyingine, hivi unajuwa ugonjwa wa Corona pamoja na Vita vya ukraein vimeathiri Sana uchumi wa Dunia, hivi umefuatilia hatua zinazochikuliwa na wakuu wa nchi na serikali mbali mbali duniani, hivi umeona Hali zilivyo hata kwa majirani zetu,

hakika Kama umefuatilia hayo yote niliyokuuliza Basi Kama huna kinyongo na mh Rais wetu naamini utampongeza kwa hatua alizozichukua katika kunusuru uchumi wetu na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja
Hivi huo uchumi wa dunia unawaathiri Watanzania wa huku bara tu na si wale Watanzania wa visiwani?

Kwa nini bei ya mafuta, kwa mfano, iwe ndogo huko Tanzania visiwani ikilinganishwa na huku Tanzania bara?
 
Huyu mama ataendelea kujua rangi za Watanzania,akitoka madarakani,nadhani hakujifunza kwa Magu.Kama JPM alipondwa vile na alikua vile,huyu mama itakuaje?Aisee.

JPM alipondwa na wanga.

hakuna mtu timamu alimponda au anamponda jpm.
 
Ni bora ungefanya kautafiti kadogo sana kujua 'feelings' za wenzako kuhusu mweleko wa nchi kuliko kuandika kwa mihemko!
 
Uchumi wa watanzania wengi unategemea secta ya kilimo ambako huko utakuta mh Rais ameweka mkono wake wa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini ili mkulima amudu Bei za mbolea, hii itamsaidia mkulima kukuza kipato chake na uchumi wake kwa kuwa uzalishaji utaongezeka

Hapo Kama ana mtoto akienda shule anakuta Elimu bure kwa kuwa mh Rais ni Rais mwenye huruma anayetaka kuona watoto wa wananchi wanyonge nao wanapata fursa ya Elimu bila shida,sasa hapo hajasaidia au unataka Rais wetu afanye Nini ndio ulizike wewe.
Hakuna alichokifanya yeye binafsi maana kuhusu elimu imetajwa kwenye ilani ya chama chake sasa kwanini unampamba mtu ambaye anatekeleza maelekezo ya mdhamini wake na sio matakwa binafsi ya kisiasa
 
Nyie kunguni ndio mnatuharibia nchi.
Samia hizi sifa hata anashangaa zimekujaje? Na hajafanya lolote.

Fanyeni kazi achwni kujikomba
 
Aisee sio bure utakuwa umetumwa na kama hujatumwa nenda kajitafakari vizuri
 
Ndugu zangu, wanasema uchumi mzuri ni ule unao gusa maisha ya watu wengi. Ukimfuatilia vizuri Mh. Rais wetu utagundua kuwa anajenga uchumi wenye kumgusa kila Mtanzania.

Kwanza Mh. Rais ametambua kuwa kilimo ndio sekta iliyo ajiri watanzania wengi wa makundi tofauti tofauti. Hivyo juhudi zozote za kuujenga uchumi wetu ni sharti ukipe kipaumbele kilimo.

Ndio maana unaona ongezeko la bajeti katika wizara ya kilimo na hata utoaji wa ruzuku takribani billioni 150. Hii inakwenda kuchochea uzalishaji, lakini pia kundi kubwa linakwenda kuguswa kupitia mipango hii ya Rais wetu mpendwa.

Mh. Rais wetu smedhamilia kuhakikisha kuwa, katika kujenga uchumi wetu hakuna mtu au kundi lolote linaloachwa nyuma au kusahaulika. Hali hii inajidhihilisha kwa namna anavyojenga miradi mbalimbali inayogusa maisha ya watu hasa wanyonge.

Ndio maana unaona miradi kama shule, vituo vya afya, zahanati, huduma za maji na umeme vikitamalaki kila Kona ya nchi hii.

Rais wetu pia anajitahidi kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unaoikumba dunia unapunguzwa kwa kuweka ruzuku kwenye mafuta ambayo ni injini ya uchumi wetu. Ndiyo maana unaona akitoa karibu billioni mia moja kila mwezi.

Rais Samia mama yetu Atakumbukwa sana akimaliza uongozi wake 2030, kwa kujenga uchumi unaogusa watanzania hasa wakipato cha chini. Kazi ya serikali ni kusaidia watu kunyanyuka kiuchumi, kazi ambayo Mh. Rais wetu anaifanya vyema sana.

Mama hakika yupo kazini, tunamuhitaji mama aendelee kututumikia hadi 2030. Ndio tutajuwa tufanye nini akitufikisha hapo, kikubwa tunaendelea kumuombea uzima na afya njema.
Aisee ungekuwa upo karibu yangu hata sijui ningekufanya kitu gani.
 
Anaweza kuwa sahihi na anaweza asiwe sahihi. Yeye ni mtanzania acha aseme.

Pinga hoja kwa hoja,matusi mwiko
 
Mimi na ukoo wangu na watanzania wengi tunaendelea kumpongeza mh Rais wetu kwa kazi kubwa anayofanya, huku niliko tayari mbolea ya Ruzuku umeshapika, huku Ni pongezi tu kwa mh Rais wetu
Endelea kupongeza hadi ukiguswa kota lako ndo utashtuka
 
Back
Top Bottom