Rais Samia Atoa milioni 100 kwa ajili ya Ukarabati kanisa la Katoliki Manyara

Serikali haina dini ila watu wake wana dini.
 
Endelea kuweka neno mkuu.
Rais Nyerere alijitambulisha kama Mkatoliki. Alipokuwa Dar es salaam, kila siku asubuhi alikuwa akisali kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay. Tuliokaa Oysterbay tulimuona. Si Jumapili tu, kila siku.

Alipewa shutuma kwamba anapendelea Wakatoliki.

Akasema serikali yake hata haijui mawaziri ni wa madhehebu gani, anajua tu wanavyoapa wanatumia kitabu gani. Alisema serikali haina haja ya kujihusisha na mambo ya dini. Alisema hata kwenye kuhesabu watu, serikali haikusanyi idadi ya watu gani ni wa dini gani, na kama mtu anatafuta habari hizo, aende kwenye taasisi za dini.

Nyerere hakuwahi kutoa hela za serikali hivi kwenye taasisi za dini, kwa sababu alielewa mipaka ya serikali na dini.

Nyerere hakuwahi hata kupanda mbele kwenye altare kanisani kusema neno kanisani kama rais.

Rais Mkapa naye alikuwa anakwenda kanisa la St. Immaculata Upanga, hakuwahi hata kupanda madhabahuni kutoa neno kama rais. Alielewa mipaka ya serikali na dini, separation of church and state/ religion.

Sasa hawa viongozi wetu wa sasa wanaosema wanamuenzi Nyerere, mbona tunawaona wanaondoka kwenye misingi ya Nyerere ya kukataa kuchanganya mambo ya serikali na dini?
 
Saa 100 ni mfano wa rahisi asiyependa kuumiza kichwa kabisa na anaona njia ya rahisi yeye kujipatia ummarufu ni hiyo ya kugawa psa za wananchi hivyo hovyo Laiti kama angekuwa na uwezo wa kuzitafuta angeziheshimu
 
Politics...
 
Maelewano gani kwani kulikuwa na kutoelewana kati ya Rais Samia na kanisa? Kupinga uuzwaji wa bandari haikumaanisha ugomvi wa kanisa na raisi

Sent from my Infinix X660C using JamiiForums mobile app
 
Tafadhali tumpe tina la EDITHA au MATILIDA. 😊😊
Mpenzi wangu FaizaFoxy nitambatiza na kumpa jina la kikristo wakati wa ufunguzi wa hilo kanisa….! Naomba mmuchagulie jina πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mgema ukimsifia sana pombe huitia maji.

Na kweli pombe imewekwa maji mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…