Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa


Kwa hiyo hoja yako ni nini ? Ni Samia vs Magufuli ? Au Samia + Magufuli ?
 
CCM mpaka mpate akili itachukua muda mrefu sn, hizi ni pesa za umma na siyo mali ya mtu binafsi
 
Hii mradi kanda ya ziwa tu,,mikoa ya mbeya iringa njombe songea ccm wanawaona mapimbi sana
Huu ni muda wa kuifuta ccm mikoa ya nyanda za juu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kanda ya juu kusini, kazi tunayo mbona.
 
Nyerere haenziwi kwa kujenga viwanja vya ndege bali kwa kuheshimu

Wewe tunajua kuwa ndiwe bi kidude mwenyewe unajisifia kwa majina bandia kwenye mitandao
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa hizo pesa Mwaka jana za fidia nani alitoa mkuu
Ni serikali na huo mradi ulianza tangu enzi za Kikwete katika mpango wake wa kuboresha viwanja vya ndege vya Songwe, Kigoma, Kagera na Musoma, jiwe akawa anaukwepa kwepa, fidia zililipwa kwa sababu tu ilikuwa kwenye mpango lakini plani ya ujenzi haikuwepo kabisaaaaaaaa
 
Angeuacha tu. Wenyeji wa mkoa wa Mara hawathamini mkoa wao ndiyo maana hata mwl aliongoza miaka 24 na akauacha kama mnavyouona.

Pia walikuwa viongozi kibao wa kitaifa lakini hakuna chochote walichokifanya. Mwingine aliishia kujisifia kula vichwa vya watu na kukata mauno.
 
Pesa za kuanza ujenzi wa uwanja wa Musoma, Msalato, Mbeya, Geita (Chato) na Mtwara zilitengwa katiba Bajeti ya mwaka 2017 au 2018 hivi. Process ya Ujenzi inaendelea kwa miaka kama minne au mitano hivi, na mpaka sasa viwanja vyote havijakamilika sawasawa, ingawa kile cha mbeya nadhani kimetangulia kufuatia na cha Chato au Msalato.
Mkuu sami huo uwanja kaja kukamilisha tu mradi umeanza enzi za jiwe maan ata fidia watu wamelipwa wakat wake
Utakuwa na nguvu sana kubishana na CM 1774858 katika swala lolote linalohusu Samia! Account hiyo imefunguliwa miezi sita tu iliyopita ila tayari ina posts zaidi 2200 ambapo 98% ya posts zote hizo ni kuhusu Samia.
 
Safi sana Mama Samia. Kale kauwanja kalikuwa kanatia aibu. Na itasaidia Sana mkoa wa Mara kiuchumi kupitia utalii hususani mbuga ya Serengeti. Mtalii akishashuka atafika kirahisi na kuingia Serengeti kupitia lango la Lamadi au Mugumu kwenye hifadhi wanyama za Grumeti au Ikoma. Pia itakuwa ni short cut ya kwenda Mkoa wa Simiyu kwa wilaya za Busega na Bariadi ambayo ndii makao makuu ya mkoa.
 
Uwanja huu ulihitaji ukarabati siku nyingi naujua. Msiingize siasa kwenye hili sio kumpaka Mwl Nyerere mafuta kwa mgongo wa chupa. Musoma walihitaji huu uwanja siku nyingi kwanza wapo karibu zaidi na mbuga ya Wanyama ya Serengeti kuliko Mwanza na Arusha. Hoteli za kitalii zilitakiwa zijengwe Musoma sio Mwanza wala Arusha tu. Serikali iitazame Musoma kama sehemu ya utalii sio eti Nyerere acheni siasa kwenye vitu hivi. Nisieleweke vibaya kuwa nampuuza Mwalimu hapana nilimuheshimu na naheshimu legacy zake.
 
Sio vitu vya kulazimisha kujenga uwanja wa kimataifa Chato na kuanzisha mbuga ya wanyama kwa nguvu na wanyama wenyewe sijui wapo au walishavuka mpaka kwenda Rwanda? Tutumie hela za wananchi kwa umakini sio kutafutia kiki za kisiasa hata Mwalimu asingetaka hizi kauli.
 
Unajenga uwanja wa ndege kumuenzi Mwalimu? Sio kuhudumia wananchi na biashara zao?

Amandla....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…