Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Kwa hiyo kuboresha Uwanja wa Ndege wa Musoma, alikozaliwa Mwalimu sio kumuenzi? Mwendazake alifanya unafiki mkubwa kwa kutoanzisha mradi wowote mpya mkoani Mara, japo alikuwa anajifanya anamuenzi Mwalimu. Mradi pekee aliowazuga watu wa mkoa wa Mara ni kukamilisha (sio kujenga) mawodi mawili matatu ya akinamama wajawazito na watoto kwenye hospitali ya Kwangwa, Musoma zaidi ya hilo hakuna. Hata mradi wa maji wa Bunda aliukuta ukiwa unaendelea tangu enzi za Kikwete. Mama kaamua kutengeneza airport ili kufungua njia nyingine za kiuchumi ikiwemo utalii maana wazungu wakishuka Musoma ni rahisi kwenda Serengeti
Kwa hiyo hoja yako ni nini ? Ni Samia vs Magufuli ? Au Samia + Magufuli ?