Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

Bwawa la Nyerere halikuwemo katika mipango yake. Environmental Impact Assessment iliposema halina tija akaliweka pembeni. Kama ambavyo walivyofanya marais watatu waliomfuata.

Amandla...
 
Bwawa la Nyerere halikuwemo katika mipango yake. Environmental Impact Assessment iliposema halina tija akaliweka pembeni. Kama ambavyo walivyofanya marais watatu waliomfuata.

Amandla...
Nani huyo?
 
Halafu atakuaa anatua hapo? Vipi wa Chato ushaisha phase II?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Nchi haina dira, viongozi wanajenga miradi isiyo na tija kisa kufurahishana
 
anataka kujenga uwanja wa kuanikia mahindi, na mtama au? sijaelewa
 
Kwa kuendeleza na kuufanyia maboresho uwanja huu nakupongeza maana, nikirudisha kumbukumbu zangu nyuma alipofariki Nyerere ndege nyingi zilishindwa kutua katika kiwanja kile hakika utakuwa umeacha alama kwa wana Mara na Wana musoma kwa ujumla.

Kuhusu kile chuo kilichopelekwa butiama sijajua kwanini hadi sasa hawajaanza fanya udahili
 
Hii mradi kanda ya ziwa tu,,mikoa ya mbeya iringa njombe songea ccm wanawaona mapimbi sana
Huu ni muda wa kuifuta ccm mikoa ya nyanda za juu
Nyanda za juu nyie sio watanzania halisi sijajua kwanini hamkuangukia kwenye nchi za jirani zetu
 
Tanzania kamwe hatutaendelea hivi karibuni ikiwa hatuna mwelekeo wala dira katika uongozi wa nchi. Kila rais ajaye anabuni mambo yake. Baya zaidi ni mambo haya ya kujitakia sifa. Uwanja wa ndege ni huduma/kitega uchumi, haujengwi kwa sababu ya kmuenzi mtu, yeyote. Sidhani kama kuna mtaala wowote uliofanywa juu uwanja huo utarudisha vipi pesa za watoa kodi. Inaelekea pesa za Watanzania zaamuliwa na mhumuko mmoja tu na mapenzi ya mtu! Nchi itaendelea vipi hivyo?
Natoa mfano wa Rwanda: kwa miaka 20 tu iliyopita Rwanda imepiga hatua kubwa sana ya kuigwa. Bila shaka sababu kuu ni kuwa kuna mwelekeo, dira na uongozi usobadilika badilika kama kinyonga.
Pili: Kwa nini kajiwanja kama haka kajengwe na Wachina? Jamani. Inadhi sana. Si muagize vyombo tu msivyonavyo? Mainjinia chungu nzima wapo. Walieni tu nusu ya mnavyowalipa Wachina watafanya kazi zaidi ya Wachina. Mbona Waafrika hatujiamini hivi?
 
SERIKALI NDIO IMETOA FEDHA NA SIO SAMIA.

HAJATOA KWENYE AKAUNTI BINAFSI BALI KITOKA HAZINA YA JMT [emoji1241]
 
Najua vijana wengi wa sasa hamjui . Miaka ya nyuma kuna kiwanja cha ndege cha kimataifa kilitakiwa kujengwa sehemu moja inaitwa Nyansurura. Baada ya Nyerere kuondoka madarakani mpango huo ukafanyika hadi leo. Ilikuwa kumuenzi vizuri ilikuwa kujenga huo kuliko ukarabati wa huo.
 
Uwanja unajengwa sio kukarabatiwa, Palikuwa na vumbi tu pale
 
Huyu Samia ni tajiri sana kumbe.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…