Rais Samia atua Tanzania, aongelea mafanikio ya safari yake Marekani

View attachment 2203337

Akizungumza baada ya kurejea Nchini Tanzania kutoka Marekani, amesema Watanzania wategemee matunda kutoka Filamu ya TheRoyalTour na Nchi ijitayarishe kupokea wageni wengi

Amesema Fedha za kutengeneza Filamu hiyo zimetokana na michango ya Wafanyabiashara mbalimbali Ndani na Nje ya sekta ya Utalii iliyoanguka kidogo kutokana na mlipuko wa COVID19

Aidha, Rais Samia amesema akiwa ziarani amezungumza na Serikali ya Marekani na kunyoosha pale palipokuwa na changamoto, akisema "Sasa tupo vizuri, tunaenda nao vizuri sana"

Mambo zaidi aliyoongea Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan:
Uhusiano wa Tanzania na Marekani umetimiza miaka 60 mwaka 2021. Zamani tulikuwa zaidi kunyoosha mikono, tunaomba hiki na kile

Lakini sasa tumekubaliana pamoja na kwamba hayo yatakuwepo, uhusiano mkubwa ni Uwekezaji na Biashara

Rais Samia: Tulifanya mazungumzo na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa (Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani), tumekubaliana vizuri

Fedha kama ile tuliyoleta na kuipeleka kwenye Vituo vya Afya na Madarasa, tunatarajia kuna nyingine itakuja iende kwenye maendeleo

Rais Samia: Kuna kundi lilienda kufanya Mkutano na Meya wa Jiji la Dallas, na matokeo ya Mkutano ule ni kwamba wenzetu wamekubali na wana hamu wafanye undugu na Miji yetu

Tunaangalia uwezekano wa kuwa na ndege zitakazotoka moja kwa moja Dallas mpaka Tanzania kuleta wageni

Rais Samia: Katika mazungumzo yetu na Wafanyabiashara wa Marekani tumesaini mikataba ya makubaliano ya miradi ya kuja kuwekeza Tanzania, thamani tuliyopiga ilifikia Trilioni 11.7

Kazi ni kwetu kuwapokea hawa watu bila usumbufu na kufanya uwekezaji wao uwepo Tanzania
Naona kama maneno matupu mepesi mepesi tu. Au nyie mnaonaje ndugu zangu?
 
Baadhi ya approach za mama zinahitaji muda kumuhukumu. Muda ni mwalimu mzuri , kama italeta tija tutaona matokeo.
 
Ukweli wko ni upi? Halafu huyu ni Rais wa nchi mpe heshima yake. Tuwe na ustaarabu ktk kutumia Uhuru wa maoni ndugu yangu. Siyo sahihi hicho ulichokiandika yaani kina kera.🙏🙏🙏
Acha ukereke, kwani nikisema maza wewe unaelewa nini inamaana Tz kuna maza mmoja? shame on you
 
Baadhi ya approach za mama zinahitaji muda kumuhukumu. Muda ni mwalimu mzuri , kama italeta tija tutaona matokeo.
Hata mimi niko kama mawazo yako yalivyo, kuna tabia ya kutaka kuwa na Taifa la kupandikizana chuki bila kukosewa kitu na mtu.

Kwanza mpaka dakika hii mama amerudisha uhuru wa Watanzania kwa kiasi kikubwa na shughuri za kisiasa zinarudi, mengine apewe muda, binafsi namuona mama ni muungwana sana.
 
Acha ukereke, kwani nikisema maza wewe unaelewa nini inamaana Tz kuna maza mmoja? shame on you
Unajuwa wewe ni fala sana, hii thread inamuhusu nani, na nani ametowa ahadi na wewe ukasemaje?

Some people are alive because is crime to shoot them, just stupid like you.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
View attachment 2203337

Akizungumza baada ya kurejea Nchini Tanzania kutoka Marekani, amesema Watanzania wategemee matunda kutoka Filamu ya TheRoyalTour na Nchi ijitayarishe kupokea wageni wengi

Amesema Fedha za kutengeneza Filamu hiyo zimetokana na michango ya Wafanyabiashara mbalimbali Ndani na Nje ya sekta ya Utalii iliyoanguka kidogo kutokana na mlipuko wa COVID19

Aidha, Rais Samia amesema akiwa ziarani amezungumza na Serikali ya Marekani na kunyoosha pale palipokuwa na changamoto, akisema "Sasa tupo vizuri, tunaenda nao vizuri sana"

Mambo zaidi aliyoongea Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan:
Uhusiano wa Tanzania na Marekani umetimiza miaka 60 mwaka 2021. Zamani tulikuwa zaidi kunyoosha mikono, tunaomba hiki na kile

Lakini sasa tumekubaliana pamoja na kwamba hayo yatakuwepo, uhusiano mkubwa ni Uwekezaji na Biashara

Rais Samia: Tulifanya mazungumzo na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa (Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani), tumekubaliana vizuri

Fedha kama ile tuliyoleta na kuipeleka kwenye Vituo vya Afya na Madarasa, tunatarajia kuna nyingine itakuja iende kwenye maendeleo

Rais Samia: Kuna kundi lilienda kufanya Mkutano na Meya wa Jiji la Dallas, na matokeo ya Mkutano ule ni kwamba wenzetu wamekubali na wana hamu wafanye undugu na Miji yetu

Tunaangalia uwezekano wa kuwa na ndege zitakazotoka moja kwa moja Dallas mpaka Tanzania kuleta wageni

Rais Samia: Katika mazungumzo yetu na Wafanyabiashara wa Marekani tumesaini mikataba ya makubaliano ya miradi ya kuja kuwekeza Tanzania, thamani tuliyopiga ilifikia Trilioni 11.7

Kazi ni kwetu kuwapokea hawa watu bila usumbufu na kufanya uwekezaji wao uwepo Tanzania
nchi inamadini gesi mito maziwa bahari mbuga za wanyama aridhi bora kwa kilimo lakini cha kusikitisha imelaniwa kuwa na viongozi omba omba,
 
Mama Samia aache utapeli wa kijinga, wageni watakuja kwakuwa ugonjwa wa Covid ni kama umepita, pia kwa sasa tunakwenda kwenye miezi ya high season. Hivyo bila hata hiyo royal tour bado wageni wangekuja. Isije ikaonekana wageni wanakuja watake kutembelea humo humo kuwa ni sababu ya royal tour. Wangalau wageni wakivuka 3m@year tunaweza kushawishika kuwa ni sababu ya royal tour.
 
Hata mimi niko kama mawazo yako yalivyo, kuna tabia ya kutaka kuwa na Taifa la kupandikizana chuki bila kukosewa kitu na mtu.

Kwanza mpaka dakika hii mama amerudisha uhuru wa Watanzania kwa kiasi kikubwa na shughuri za kisiasa zinarudi, mengine apewe muda, binafsi namuona mama ni muungwana sana.
Unachosema linaweza kuwa kweli Ila pia utakua na mapenzi nae binafsi.

Hadi sasa sijawa impressed kwa kuwa anadeal na petty issues tu, na pia maneno matamu ni mengi bila progress yoyote
 
Mama Samia aache utapeli wa kijinga, wageni watakuja kwakuwa ugonjwa wa Covid ni kama umepita, pia kwa sasa tunakwenda kwenye miezi ya high season. Hivyo bila hata hiyo royal tour bado wageni wangekuja. Isije ikaonekana wageni wanakuja watake kutembelea humo humo kuwa ni sababu ya royal tour. Wangalau wageni wakivuka 3m@year tunaweza kushawishika kuwa ni sababu ya royal tour.
Kabla ya covid walikua wanakuja wangapi hiyo high season!?...ili tujue Kama royal tour imetulipa
 
Unachosema linaweza kuwa kweli Ila pia utakua na mapenzi nae binafsi.

Hadi sasa sijawa impressed kwa kuwa anadeal na petty issues tu, na pia maneno matamu ni mengi bila progress yoyote
Ni sekta ipi inayoingizia nchi fedha nyingi ikiwa utalii ni pety!?...
 
Back
Top Bottom