Rais Samia aunda kamati kutathmini utendaji kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Rais Samia aunda kamati kutathmini utendaji kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Hizi pesa za walalahoi zinatumika vibaya. Hawa marais wakiwaona watu ambao wanafahamiana nao hawana cha kufabya ndo huo upuuzi huwa wanaanzisha. Haaaa kalaghe .Magu alimtoa nduki uk maana alikuwa kama hayupo
 
Kuna watumishi pale wako very demotivated sababu ya utolewaji upendeleo katika kutolewa vyeo.

Mpaka ujulikane na Rais au ujipendekeze sana apewe jina ndio upande cheo hasa cha ubaloziii.
 
Watu walosomea Na kubobea kwenye maswala ya diplomas hawapewi vyeo wanapewa watu baki wanasiasa ambao hata ukiwauliza what is diplomacy hawajui! [emoji848]
 
Anaweza kutolewa mtu huko alomleta anakojua akawa na cheo lakini wenyeji wanaachwa.

Hii inafanyika kwenye taasisi za Umma nyingi sana siku hizi tangu enzi za Mwendazake.

Inarudisha nyuma utendaji.

Unapomleta mtumishi mgeni hata akiwa kiongozi maana yake aanze moja kujifunza Na kuielewa organizational culture ya hiyo taasisi husika,
Itamchukua miaka kadhaa kuielewa panda 2-3 Kisha kuanza kuielewa na kuanza kufanya kazi ziendelee.

Hili linachelewesha utendaji kwa kiasi kikubwa.
 
Kwanini ulete watu au CEO mgeni toka mbali kuja kwenye taasisi ya umma?

Je hiyo taasisi haina watumishi wenye sifa na uzoefu?

Kwanini msifanye interview kupata watumishi toka taasisi husika?

Hao wanaoletwa wenyewe sasa ?!
 
Hiyo ya kujiamulia kupeleka watumishi taasisi mbalimbali inapelekea watoto wa Viongozi kufanya kazi popote wanapotaka,

Watu wanachomekea watu wao!

Na fitina na kuhamisha wengine walioko ndani ili wawapishe walioko nje ya taasisi waingie.

Yaani ni mbilingembilinge tu ilimradi!
 
Niliposoma mara ya kwanza hii mada ilivyowekwa, akilini mwangu wizara ya kwanza ilikuwa ni hiyo hiyo inayohusu Tanesco.

Huyu anazo sababu zake. Wanaovuruga huko kwenye hii wizara ya Mambo ya Nje, ni hao hao watu wa aina yake muunda kamati, na anajua hivyo.
Tatizo linafahamika linakotokea, tume ni ya nini tena kama siyo kufuja pesa.
Nadhani kuna jambo fulani halipo sawa ndio maana Mheshimiwa Rais SSH ameunda hii kamati. Labda nikumbushe tu, juzi kwenye mabadiliko ya Makatibu wakuu wa wizara aliyekuwa Katibu Mkuu wa hii Wizara Balozi Sokoine aliwekwa kando bila kutoa maelezo yeyote.
 
Back
Top Bottom