Mkuu GTL, hapa sina wasiwasi wowote kuhusu lililpo tatizo. Huyu muunda kamati anavyo vyombo vyote vinavyompa taarifa kuhusu matatizo mbalimbali kwenye wizara zake na kwingine kote.Mkuu, yaani unahisi kwamba wewe utakua unayajua mambo na taarifa nyeti za kila wizara kuliko RAIS wa Nchi?
Kwanini huwa mnalitaka Jeshi la polisi lisijichunguze lenyewe dhidi ya tuhuma zinazolihusu?
Kwanini tusisubirie Report baada ya uchunguzi?
Kuunda Kamati kuchunguza Wizara ni ufujaji wa pesa, hakuna zaidi ya hapo.
Kwa hiyo, wewe mkuu GTL umeona kamati ndiyo sahihi kuchunguza tatizo kwenye wizara hiyo siyo?
Basi niambie, wizara ngapi zina matatizo, tena makubwa sana hata kuliko hiyo inayoundiwa kamati.
Kwa maana hiyo basi, nipendekeze kwako, na kwa huyo mteuzi, aunde kamati za kuchunguza, hata vyombo vinavyoshindwa kumpa Mteuzi wa Kamati taarifa sahihi zinazohusu serikali yake!
Sasa sijui hapo utasemaje mkuu wangu.
Pengine itabidi pia iundwe Kamati kuchunguza "Muunda Kamati" mwenyewe.
Lakini ukitaka kujua ushauri wangu wa bure kwake ni kwamba, hiyo wizara husika apewe mtu toka Visiwani aiendeshe, kama si hivyo, basi wizara iondolewe kwenye Muungano, kila upande uwe na wizara yake, ili tumalize muungano haraka.