Rais Samia aunda kamati kutathmini utendaji kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Mkuu, yaani unahisi kwamba wewe utakua unayajua mambo na taarifa nyeti za kila wizara kuliko RAIS wa Nchi?

Kwanini huwa mnalitaka Jeshi la polisi lisijichunguze lenyewe dhidi ya tuhuma zinazolihusu?

Kwanini tusisubirie Report baada ya uchunguzi?
Mkuu GTL, hapa sina wasiwasi wowote kuhusu lililpo tatizo. Huyu muunda kamati anavyo vyombo vyote vinavyompa taarifa kuhusu matatizo mbalimbali kwenye wizara zake na kwingine kote.

Kuunda Kamati kuchunguza Wizara ni ufujaji wa pesa, hakuna zaidi ya hapo.

Kwa hiyo, wewe mkuu GTL umeona kamati ndiyo sahihi kuchunguza tatizo kwenye wizara hiyo siyo?

Basi niambie, wizara ngapi zina matatizo, tena makubwa sana hata kuliko hiyo inayoundiwa kamati.
Kwa maana hiyo basi, nipendekeze kwako, na kwa huyo mteuzi, aunde kamati za kuchunguza, hata vyombo vinavyoshindwa kumpa Mteuzi wa Kamati taarifa sahihi zinazohusu serikali yake!
Sasa sijui hapo utasemaje mkuu wangu.

Pengine itabidi pia iundwe Kamati kuchunguza "Muunda Kamati" mwenyewe.

Lakini ukitaka kujua ushauri wangu wa bure kwake ni kwamba, hiyo wizara husika apewe mtu toka Visiwani aiendeshe, kama si hivyo, basi wizara iondolewe kwenye Muungano, kila upande uwe na wizara yake, ili tumalize muungano haraka.
 
Sikujua kuwa jamaa amekwishawekwa kando. Asante kwa taarifa.
 
Wakati anateuliwa mulamula mlisema ni bingwa wa diplomasia, huyu alipoteuliwa mlisema pia bingwa wa diplomasia. Nilichoona sasa hivi kuna timu ipo kwa ajili ya hii kazi
 
Unamaanisha Togolani na polepole wanajua diplomasia ya uchumi? Hii nchi hii kweli hasara

Hao wenyewe kina mulamula na huyo Tax wakati wanateuliwa mlisema hivyohivyo
 
Kama vipi apewe tu Uwaziri wa heshima JK wa Msoga au arudishwe yule jamaa yetu aliyetaka kuwa Rais bwana Membe... Ikishindikana kabisa nipewe mimi Mh Nangu Nyau ila ofisi ya wizara itakuwa pale Manhatam.
Warudishwe ili tatizo liongezeke? Tatizo sisi huwa ni wasahaulifu sana, hata haya Sasa turasahau pia
 
Unamaanisha Togolani na polepole wanajua diplomasia ya uchumi? Hii nchi hii kweli hasara

Hao wenyewe kina mulamula na huyo Tax wakati wanateuliwa mlisema hivyohivyo
Hao sio Wana biashara,hao niliowataja wameonesha Tija sana tuu kwenye maeneo Yao.

Akina Tax na huyo Mulamula ni maofisa wa Ofisini tuu..
 
Mabalozi wengi waliteuliwa bila kuwa na sifa,Balozi nyingi hazina sifa ya kuwa Balozi

Wafanyakazi wengi wa Balozi zetu hawajaelimika

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Unafikiri tatizo ni kuwa na sifa ya ubalozi? Ukweli kabisa wengi wanayo hiyo sifa

Tatizo letu sehemu zote ni moja tu hatuna nidhamu. Hapo ndio kila kitu kitaanzia hapo, kuanzia upigaji hadi ujinga mwingine
 
Utaweka sana watu kando lakini kama yeye mwenyewe sio msimamizi mzuri basi ni kazi bure
 
Kamati inaundwa ili kuchunguza utendaji kazi. Ni kichekesho hiki

Swali langu mara nyingi kwa mama samia huwa kwa nn anachagua sana maeneo ya kufanya haya? Kuna wizara ambazo alipaswa pia kufanya haya lakini huwa anakaa kimya
 
Hii kamati ikitoa tathmini mnistue
 
Unafikiri tatizo ni kuwa na sifa ya ubalozi? Ukweli kabisa wengi wanayo hiyo sifa

Tatizo letu sehemu zote ni moja tu hatuna nidhamu. Hapo ndio kila kitu kitaanzia hapo, kuanzia upigaji hadi ujinga mwingine
Hili swala la nidhamu itabidi tuanze nalo shule ya msingi
 
Hao sio Wana biashara,hao niliowataja wameonesha Tija sana tuu kwenye maeneo Yao.

Akina Tax na huyo Mulamula ni maofisa wa Ofisini tuu..
Swali langu hebu nieleze tija aliyoonyesha togolani na polepole?

Tatizo tunaangalia sana nani anapost nini
 
Unafikiri tatizo ni kuwa na sifa ya ubalozi? Ukweli kabisa wengi wanayo hiyo sifa

Tatizo letu sehemu zote ni moja tu hatuna nidhamu. Hapo ndio kila kitu kitaanzia hapo, kuanzia upigaji hadi ujinga mwingine

Kwa hiyo wenye nidhamu ni hao wanasiasa wa kuokoteza?
 
Sasa hii kamati itasaidia nini?Kujua utendaji mpaka kuundiwe kamati?Hii nchi kwa kweli.
 
Hili swala la nidhamu itabidi tuanze nalo shule ya msingi
Fikiria tu mfano yule balozi aliyefariki, alikua na CV kubwa mno na mbobezi wa kwenye eneo hilo. Jiulize ilikuwaje akapata ile kashfa ya ubakaji ofisini?
 
Fikiria tu mfano yule balozi aliyefariki, alikua na CV kubwa mno na mbobezi wa kwenye eneo hilo. Jiulize ilikuwaje akapata ile kashfa ya ubakaji ofisini?
Ndo maana narudi pale pale kuwa tuanzie majumbani kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…