Rais Samia awaapisha Wakuu wa Mikoa. Afanya mabadiliko madogo, Kafulila apelekwa Simiyu, Mongella aletwa Arusha

 
Amehofia huyo Kafulila angeirudisha Chadema madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao, au!!

Kwa hali hii, Katiba Mpya haikwepeki! Yaani unamteua mtu leo, kesho unamtengua/kumhamisha juu kwa ju, na hakuna wa kukuhoji!!

Only in Tanzania!!
Kwani ccm watashinda tena jimbo lolote tena 2025 lililo mjini?

Tuendelee kuwepo
 
Si amesema anaenda kuongea nao kwenye kikao cha kazi .
 
Mkuu ile kitu haichagui, maana mateso ni kwetu sote.

Gharama za business na maisha zinabadilika sana hali ya umeme ikiwa tete mkuu.

Hili la umeme naomba maza akopi kwa Magu aisee.
Hapana mkuu, mama na Magu ni watu tofauti, kwani we huoni kelele hizi zinzopigwa humu ili kupinga mama wasifanane kwa lolote na Magu?
 
Tulizoezwa vibaya si kila shughuli lazima kiongozi ahutubie halafu praise team wafanye ufafanuzi
 
Unauliza jibu

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Habari za wapi Yakheee!!! Kikwajuni, kibanda maiti au mchamba wimaaa!!! Rais wenu tuliye waazimisha kutoka Bara, anaendeleaje Yakheee?

Naona huyu mliyetuletea kutoka huko Yakhee anazinguaaa!! Yaani anateua leo, kesho anabadili!! Yaani hatumuelewi kabisa Yakheee!! Yaani kama anapika urojo Yakheee!! Kama vipi kila Nchi imchukue Rais wake Yakheee!!! Twaona nyie mwafaidi zaidi na huu mbadilishano Yakheee!!

Au unaonaje Yakheee!!
 
Wala haina tatizo kubadilisha for good!

Ndiyo maana kuna continuous improvements kwenye modern management style [emoji108][emoji108][emoji108]

The world is dynamic because of advanced changes in technologies!

The world is not static!
 
Kama aliona mongela ana uzoefu,amemuhamisha kutoka mwanza wa nini? Angembakisha huku huku mwanza.
 
Mwenye CV ya SSH tafadhali
 
Hapana mkuu, mama na Magu ni watu tofauti, kwani we huoni kelele hizi zinzopigwa humu ili kupinga mama wasifanane kwa lolote na Magu?

Hiyo inajulikana, kila mmoja ameumbwa kwa jinsi tofauti na mwenzake. Ila kama kuna mazuri aliyofanya mwendazake, si vyema kuyaacha yaende na mwendazake, mwendazake aende na maovu na mabaya yake, mazuri yabaki.

Kwangu umeme, barabara na kutodhurumiana ardhi natamani kuona tukiendeleza alipoishia jamaa.
 
Tatizo mnataka mama acopy na kupaste kwa Magu. Ni kitu hakiwezekani. Hii ni awamu yake anatakiwa aongoze anavyoona yeye. Likiharibika jambo ni yeye ndo atasemwa na sio Hayati. Kama Kuna mahali makosa yalifanyika mama afanye masahihisho mapema. Na watu wakubali KILA nafsi itaonja mauti. Magufuli amefariki na hatarudi tena. Alifariki Nyerere na tukasonga mbele, hata hii ya Magu tutasonga mbele. Mama amronesha dira nzuri na wananchi huku nje wanamuunga mkono sana
 
Amehofia huyo Kafulila angeirudisha Chadema madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao, au!

Kwa hali hii, Katiba Mpya haikwepeki! Yaani unamteua mtu leo, kesho unamtengua/kumhamisha juu kwa ju, na hakuna wa kukuhoji!!

Only in Tanzania!!
Katiba mpya italishughulikiaje hilo? Tufafanulie - maana katiba mpya inaongelewa kana kwamba ina miujiza!
 
Akizungumza leo katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa mikoa ,
Spika wa Bunge la JMT, Mh. Job Ndugai, kwa masikitiko makubwa amesema (Nanukuu) ' kumekuwa na uonezi na maonezi makubwa Sana katika taasisi ya TAKUKURU, ni vizuri mkajiangalia upya, sisi ambao tunawakilisha wananchi tunaona, Si mahali pa kusemea lakini Waziri na wenzake watawasaidia kwa upande mwingine, Si vizuri kuonea watu, haipendezi hata kidogo' alisisitiza zaidi Bw. Job Ndugai!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Katiba mpya italishughulikiaje hilo? Tufafanulie - maana katiba mpya inaongelewa kana kwamba ina miujiza!
Katiba Mpya itapunguza mamlaka ya Rais katika uteuzi kwa kuhusisha pia mamlaka nyingine kama Bunge na Mahakama!

Na pia Rasimu ya Katiba Mpya ya Wananchi, ilifuta hivi vyeo vya Wakuu Mikoa na Wilaya! Maana havina tija yoyote ile, zaidi tu ya kuongeza matumizi ya fedha serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…