Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Ila Samia hapaswi kumsema vibaya hata kama walipishana'
Mkuu mama Samia ndiye mwenye mpini sasa hivi na alikuwa msaidizi wake hivyo wacha atupatie madhaifu ya mtangilizi wake.
 
Wacha tuujue udhaifu wa jiwe kama mbwai wacha iwe mbwaaiiii
 
Hakika Mungu hamfichi mnafiki
 
Mama kakata tamaa ya kura za kanda ya ziwa iwapo akigombea 2025!!Labda kama hatogombea na anajua hatogombea!!!
 
Kwa nini hamtaki kusikia ukweli??
 
Ni heshima hiyohiyo ya uoga ndiyo inamfanya hata CAG aatamie madudu ya awamu hii.

Muda ukifika na yeye atanangwa hivihivi.
 
Kama ile ilikuwa nidhamu ya uoga kwa sababu ya simba wa yuda basi tutamkumbuka sana tena sana. Yeye anayetaka nidhamu ya moyoni atuonyeshe achievements...
Nakubali the end justifies the means.
Akituletea nidhamu kubwa zaidi with different approach she will be my hero
 
Sawa boss
 
Hakika Mkuu kama kumchafua mzee wameshamchafua sana,hakuna jipya tena ni mipasho inaendelea
 
Nidhamu ya woga afadhali kuliko uhuru wa kuiba.



Sitetei wizi wa mali za Umma la hasha!

Lakini wacha nikuulize Mpendwa ;

Kwani wakati ule hakukuwa na wizi?

Kumbe sababu ya kumsakama CAG ilikuwa ni nini?
 
Hajui maana ya uongozi alio nao, hataki kumsimamia mtu yeyote ila anataka kila kitu kiende vizuri. Kuongoza bila kusimamia ni kuweka maji kwenye dema. Kikwete aliongoza bila kusimamia wakati Magufuli aliongoza kwa kusimamia: tufauti zinajulikana. Hakuna binadamu aliye malaika kiasi kuwa ukimteua tu basi atatekeleza mambo yote perfectly, lazima asimamiwe.

Serikali siyo chombo cha kubembeleza kinachotegemea hiari ya mtu, bali serikali ni chombo cha mabavu kichoendeshwa kwa kufuata sheria kikiwa kinatoa adhabu kwa kila asiyefuata sheria hizo. Inabidi rais asimamie wateule wake, ambao pia watawasimamia walioko chini yao, na msululu unaendelea hadi ngazi ya chini kabsa ya serikali.
 
Ina maana hivi vyuo kabla ya awamu hii vilikuwa vinafundisha madudu gani?

Sasa baada ya hivi vyuo kufanya marekebisho hayo, mitaala yao itakuwa pia ikionyesha "kula kwa urefu wa kamba za wahitimu wa vyuo hivyo?

Na je, makaratasi watakayokuwa wanapewa (mavyeti), sasa yatakuwa na thamani na kuwawezesha kufanya kazi?

Maswali yangu kwa sasa ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…