Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Huwezi kupendwa na wote na huwezi kuchukiwa na wote !! That's life !!
 
Kwani kasema uongo?
 
Haya mambo yanasikitisha sana ila Pumzika kwa amani JPM, najua utakumbukwa kwa mengi mazuri.
 
Kwa mtu ambaye anapenda na kuzingatia siasa za kistaarabu, haki, kiutu na maelewano, atauelewa kwa urahisi sana mtizamo wa kiungozi wa Rais SSH. Lakini wale kwangu pakavu tia mchuzi bado vichwani mwao wamebakia na kumbukumbu za siasa za kiharamia za awamu iliyopita.

Wakati msimamo wa Madam President ni kurithi na kuyaendeleza mazuri yote ya awamu zilizopita, baadhi ya wanufaika wa awamu iliyopita wanatamani ayaendeleze na mabaya yake pia.

Toka mwaka 2016 walijawa na dhihaka, majivuno na kejeli nyingi pale Watanzania wenzao walipipitia katika madhila makubwa. Waliwabeza na kuwasimanga, huku wakisema kila zama ina msahafu wake.

Wamekuwa wepesi wa kusahau na wagumu wa kuelewa zama zimebadilika ijapokuwa zilikuwa ni fupi ama zilifupishwa. Ni dhahiri sasa ni kuwa ukishindwa kukabiliana ama kupambana nao, ni vyema ukaungana nao.

Mwenye akili na busara anamuelewa sana Madam President, wewe ni nani ambaye huoni aibu ya kulazimisha vitu vilivyopuuzwa, kusahaulika na kutupiliwa mbali!?
 
Kwa hiyo sasa wana ufanisi?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Huyu ni ndumilakuwili,mbona aku step down

Tuseme tu ukweli umejaribu kwenda kwenye taasisi za serikali ukaona huduma zao zikoje ukifananisha na simba wa chato huduma ilikuaje.
Anatikisa tu wezere lake hana lolote
 
SIMBA WA YUDA NI YESU, jamani, acheni kufananisha na Magufuli.
 
Hata iweje hakutakiwa kumuongelea kihivi, kwa sababu Wananchi wengi akili zimefunguka kupitia awamu ya 5. Inashangaza ila inasikitisha sana kiongozi wetu kumtamka aliyekuwa yeye msaidizi. Wanafikiri watanzania ni wale wa kabla ya JPM

Duh!
Anafikiri kwa kusema mabaya ya mzee kutafanya wananchi wasione mazuri aliyoyafanya,
 
Basi hujui kuongoza kama hutaki kuogopywa. Hakuna kiongozi mzuri asiyeogopwa, na iwapo una kiongozi wa namna hiyo basi hatekelezi majukumu yake. Hata dini zinatufundisha kumuogopa Mungu anayetuongoza.
 
Sio vizuri kumsema marehemu coz hawezi kujitetea, ila moyo wa mtu kichaka
 
Kundi lote la sukuma gang wameishiwa pumzi sasa kazi yao ni kutukana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…