Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Acha roho mbaya ndugu yangu.
 
Mkuu suala hili no complex ,tumshukuru tu Mama kwa Hilo ,hapoilipo umehudumiwa na watu wengi Sana was Aina hiyo!inawezekana hata aliy3msaidiaa mama yako kujifungua. Alikiwa na Vyeti Feki!
Acha walipwe Manisha yaendelee!
 
Kuwarudisha kazini ni kuwakatili vijana walioko mitaani bila ajira ambao wamehitimu kwa mujibu wa sheria, na pia kuhamasisha uvunjaji sheria kwenye sekta ya elimu(kugushi).

Kuwasaidia, wangewalipa mafao yao yawe kama mtaji wa kujiajiri ili vijana ambao hawana mtaji wala ajira wachukue hizo nafasi zao.
Hapo wangeua ndege wawili kwa jiwe moja.
 
Rais ndiye mkuu wa utumishi nchini na ana mamlaka ya kuajiri yeyote anayemtaka

Kama hilo hutaki nenda kadai katiba mpya ili imuondolee rais mamlaka hayo
 
Hata kama kughushi cheti ni kosa kisheria, DPP ana mamlaka ya kuipeleka kesi mahakamani au hata kutoipeleka. Au hata akiipekeka ana mamlaka ya kuachana nayo akiamua. na DPP ni mteule wa rais

Kama hupendi mfumo huo wa ssa wenye loopholes nyingi kwenye kutekeleza sheria ungana na wanaodai katiba mpya ili hilo liwezekane
 
Magufuli angekuwa hai angekuuliza utamlipaje stahiki mtu aliyeidanganya serikali na kujipatia ajira na mshahara kiudanganyifu?

Kama unataka kutekeleza sheria basi inabidi uwe bandidu kotekote yaani, hakuna mafao wala kurudishwa kazini.

Ila wewe ukiona bora alipwe mafao tu, mwingine ansona bora arudi kazini tu

Ni mtizamo tu wa kila mmoja
 

Kama una umri angalau miaka 45 utaelewa kuwa mfumo wa zamani wa ajira ulichukua drs la saba wengine mpaka darasa la nne.

Baadae wakawalazimisha waendelee na hapo sasa mtu ana miaka 40 hawezi kwenda shule kumkariri grasshoper na matundu yake ndo mambo ya kununua majina, kufoji n.k yakaingia.

Lile tukio ilikuwa ni kubana matumizi ya serikali, inawezekana hata yeye hakupenda ila alilazimika ndo maana hapakuwa na mpango wa replacement kuziba nafasi.

walipowaondoa maofisini waliobaki walijiongeza wakiendelea kuwasiliana na waliofukuzwa wakitafuta ushauri wa nini wafanye wapi na kwanini.

Ukiachana na udaktari, hizi field nyingine nyingi experience ni kila kitu kwenye kazi. Huwezi ondoa mtu ana experience ya 20 years or more kazini eti ana cheti feki halafu umlete graduates hapo afanye kazi zake. Ndo maana jeshi halikuguswa. Huwezi mtoa mhasibu mkuu wa kikosi ulete graduate afanye kazi zake.

Kuna watumishi walioitumikia hii nchi kama tutabadilishana na graduates watahitajika graduates 20 kujaribu kuufikia utendaji wa mtu mmoja na hawatoufikia.

Kwa sasa serikali idhibiti mfumo wa ajira wanaostaafu wawapishe wenye elimu sahihi ila kuwaondoa lilikuwa kosa.
 
Inaonyesha mambo mengi labda alikua hakubaliani nayo, alikua anatetea ugali wake, who will blame her?
Nje ya siasa, hakuwa na taaluma nyingine? Kama huwezi kusimamia haki kwenye level ya chini, unaweza kusimamia haki ukipewa mamlaka yote ya nchi? Kulikuwa na madhara gani kutoka siasani kwa ground za kutokukubaliana na uonevu na udhalimu unaofanywa, au hata uvunijfu wa sheria?

Wanasema, kutokujua sheria hakukuondolei kosa! Anakubali kuwa watumishi hao wameghushi nyaraka za serikali?

Ni lini imehalalishwa kughushi nyaraka za serikali?

Kati ya watumishi 4000 waliofukuzwa, wangapi wamefungua kesi kudai kuonewa? Ziwe zimesikilizwa au hazikusikilizwa, ngapi zimesajiliwa?

Tuishie kusema, TAKUKURU na POLISI hawatoshi, hawana meno. Genge la mahamakama na wanasheria ni wachumia tumbo kama aliyelinda ugali wake!

Nitaamini kuwa HAKI imetendeka/inatendeka ikiwa Seth, Rugemalira, Maimu na wapigaji wengine wakifungua kesi dhidi ya serikali kwa udhalilishwaji waliofanyiwa, uonevu, kunyimwa uhuru na yafananayo, wadai na fidia.

Msiba amedhalilisha watu, anapaswa kulipa watu mabilioni, serikali imedhalilisha watu na wengine kufungwa bila kosa, wahanga kimya!

Bado nipo nipo sana.
 
Ninapendekeza lazima kila mtu yeyote atakyetaka kugombew nafasi yoyote kuwe na kipimo cha utimamu wa akili..

Hii nchi imechezewa sana
 
Elimu yenyewe haina maana!cheti kina maana gani sasa!!kama form six leaver anaweza fundisha vizuri tu kuliko hata mhitimu wa chuo cha ualimu!!!!Hata form six failure anaweza kufunzwa udaktari tu na akawa deep tu bila kujali ufaulu wake!!?
 
Hongera sana mama Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…