Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Wamejiendeleza vipi kielimu?
Mtu alitumia jina la ndugu yake akapata kazi sasa leo hii amejiendeleza vipi kupata hivyo vigezo. Au ambaye alikosa cheti cha Form 4 alienda kuwa private candidate akafanya NECTA na kufaulu. Na kwa muda gani imefanyika hiyo wakati SSH hana hata mwaka. Na walijuaje kwamba watarudishwa mpaka wakaenda kusoma ndani ya miezi 6 hii.
JK anarudisha watu wake,haiingii akilini eti watu 4000 walijiendeleza,wataje vyuo walivyosoma kujiendeleza tuone.

Halafu wamehitimu wote Mara tu Hangaya alipokuwa rais?

na wale waliofikia umri wa kusitafu?
 
Ni wazi kabisa mtu akifoji kitu official huyu ni mualifu na adhabu yake inaweza kuwa kifungo mpaka miaka7.

Hamna kitu kinasikitisha kama mtu unahangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote unakomaa, halafu ajira aje kupewa mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ya kufoji vyeti, hii haiko sawa.
Tutakuwa tunakosea sana kama tunafanya vitu kupendeza wananchi na si kufuata sheria. Mtu aligunduliwa ana cheti cha kugushi akafukuzwa kazi. Hilo halina mjadala. Kama cheti kilidhaniwa kuwa cha kugushi wakati ni halali, na sasa imekuja kuthibitishwa kwamba kweli ni cha halali, hapo sawa.

Mtu huyo anahitaji kurudishwa kazini na kulipwa fidia kwa muda wote aliokuwa nje ya kazi. Kudai kwamba watu zaidi ya elfu nne wamejiendeleza kimasomo ndani ya miezi 6 ya Rais mpya ni 'danganya toto'. Haiwezi kuaminika kwamba mtu alishindwa kujiendeleza miaka yote ya nyuma aje afaulu kufanya hivyo ndani ya miezi sita tu! Aidha, kama waliofukuzwa wangeambiwa wakijiendeleza watarudishwa, baadhi wangeweza kufanya hivyo ingawa si ndani ya muda mfupi wa miezi 6.

Mwezi Marchi mtu angeweza kujiandisha kufanya mtihani wa Kidato cha 4; mwisho wa mwaka akaufanya huo mtihani na majibu yakatoka mwanzoni mwa mwaka kesho. Hivyo si chini ya mwaka mmoja mtu kusemekana amejiendeleza. Hali halisi ilivyokuwa ni kwamba wahusika wala hawakuambiwa wakijiendeleza watarudishwa. Ni ajabu ilioje kusikia watu zaidi ya elfu nne walikurupuka tu kujiendeleza na wakafaulu. Natofautiana kabisa na hili.
 
Watanzania huwaga siwaelewi kabisa kipindi cha jiwe alipowafukuza watu walishangilia ooh walikuwa wamezidi kwanini wanakua na vyeti feki, ooh mara walikua wanaziba nafasi za wenye vyeti , sasa hivi ooh mama ana huruma , mama ni binadamu yaani kwa ufupi hatujui hata tunataka kitu gani sisi
 
Sijaelewa vizuri ,waliofukuzwa vyeti feki walikuwa zaidi ya elfu 10 ,criteria gani iliyotumika kurudisha 4100? Kama ni kweli basi Mama SSH anazidi kuupiga mwingi ,vipi hao elfu 6 waliobaki stahili/stahiki zao watapata?
Itakuwa walikosea kuwafukuza. Nitashangaa MTU afoji Cheti arudishwe kazini.
 
Hakuna alosema walofoji vyeti warudi kazini bali wale darasa la saba na baadae wakajiendeleza ndo wanarudi kazini.

Acha kuwatia viongozi maneno mdomoni
Wale wa la saba waliingiaje kazini kama sifa walijkuwa hawana bila kufoji sifa husika!?
 
Ni wazi kabisa mtu akifoji kitu official huyu ni mualifu na adhabu yake inaweza kuwa kifungo mpaka miaka7.

Hamna kitu kinasikitisha kama mtu unahangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote unakomaa, halafu ajira aje kupewa mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ya kufoji vyeti, hii haiko sawa.
Rais achunguzwe pengine na yeye ni cheti feki. Kama umesota hadi kupata cheti kwa vyovyote huwezi kuoneo huruma mtu aliyefoji cheti kama chako na kupata faida kama uliyopata wewe au uliyokosa wewe kwa yeye kutumia cheti cha kufoji. Cheti feki wanastahili kua jela sio kurejeshwa kazini. Kwanza unawarejesha kwenye kazi gani maana hawakua na sifa kuajiriwa kwenye hiyo kazi?
 
Hata kama kughushi cheti ni kosa kisheria, DPP ana mamlaka ya kuipeleka kesi mahakamani au hata kutoipeleka. Au hata akiipekeka ana mamlaka ya kuachana nayo akiamua. na DPP ni mteule wa rais

Kama hupendi mfumo huo wa ssa wenye loopholes nyingi kwenye kutekeleza sheria ungana na wanaodai katiba mpya ili hilo liwezekane
Kwani Katiba ya sasa inasemaje kuhusu DPP?
 
Elimu yenyewe haina maana!cheti kina maana gani sasa!!kama form six leaver anaweza fundisha vizuri tu kuliko hata mhitimu wa chuo cha ualimu!!!!Hata form six failure anaweza kufunzwa udaktari tu na akawa deep tu bila kujali ufaulu wake!!?
Basi sawa
 
Safi sana mama umeonyesha maana halisi ya uongozi na utu umeitendea haki imani yako.
 
Labda wamedushwa wale waliotolewa kimakosa na drs la 7

Maan mimi bado sijamuona alie rud kzn hadi sasa.
Labda wawabadilishe vituo vya kazi ndio warudishwe. Maana waliondoshwa kwa kudhalilishwa hivyo wakirudi bado kisaikolojia hawatakuwa sawa.

Mimi ningependa kusikia wanalipwa mafao tu kwa kipindi walichotumikia tu kisha nafasi zao waajiriwe wapya waliopo mtaani.
 
Lilikuwa ni zoezi la uonevu kisa tu hisia eti wafanyakazi walimpigia kura Lowasa. Kama ishu ilikuwa ni vyeti mbona majeshini akuwagusa na huko ndo vimejaa.Hizi dabo standard hazifai
 
Labda wawabadilishe vituo vya kazi ndio warudishwe. Maana waliondoshwa kwa kudhalilishwa hivyo wakirudi bado kisaikolojia hawatakuwa sawa.

Mimi ningependa kusikia wanalipwa mafao tu kwa kipindi walichotumikia tu kisha nafasi zao waajiriwe wapya waliopo mtaani.
Hapana hata wenzao watafurahi kuungana nao
 
Watanzania huwaga siwaelewi kabisa kipindi cha jiwe alipowafukuza watu walishangilia ooh walikuwa wamezidi kwanini wanakua na vyeti feki, ooh mara walikua wanaziba nafasi za wenye vyeti , sasa hivi ooh mama ana huruma , mama ni binadamu yaani kwa ufupi hatujui hata tunataka kitu gani sisi
Wana Siasa ili kuongeza thamani yao huwa wanatengeneza tatizo kisha wao wenyewe wanakuja kutatua tatizo ili waonekane wamefanya vizuri. Hii ndio mbinu ya kisiasa.
 
Kuna watu walikuwa wanafyatua vyeti kule kariakoo walikamatwa na mashine zao je wameachiwa na mashine zao na mihuri? Maana nahitaji cheti cha form four
 
Huyu maza hakuna kitu, baadae watajumuisha waliorudishwa kwenye takwimu za Ajira mpya

Unajiendeleza vipi ikiwa huna sifa pumbav sana siasa
 
Hizo ni siasa hakuna mtu aliyejiendeleza popote, acheni undezi.....nyie semeni tu mmeamua kufunika kombe mwanaharamu apite.
 
Ni wazi kabisa mtu akifoji kitu official huyu ni mualifu na adhabu yake inaweza kuwa kifungo mpaka miaka7.

Hamna kitu kinasikitisha kama mtu unahangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote unakomaa, halafu ajira aje kupewa mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ya kufoji vyeti, hii haiko sawa.
SITETEI KUFOJI VETI, LAKINI
Kuwatoa watumishi wenye vyeti FEKI yalikuwa ni maamuzi ya KINYAMA sana kutoka katika Nchi yetu.

Magufuli mwenyewe alimuuwa Ben Saanane kwa vile alimhoji uhalali wa THESIS yake ya PhD ambayo inasemekana ali PLAGIARIZE kutoka kwa Dr J Y Phillip ambaye alisimamiwa na Prof Buchwashaija wa UDSM kama yeye mwenyewe Magufuli.

Magufuli aliwaacha akina Makonda waliofoji vyeti vya Form IV wakiwa Wakuu wa Mikoa, au Prof Kabudi aliyekuwa Waziri wa Sheria, lakini akawafukuza MADREVA na matarishi waliofoji vyeti vya Form IV.

Asante Rais SSH kwa kuwatetea Watanzania wenzetu, waache wapate haki zao kwa vile siyo vyeti ndiyo vilikuwa vinafanya kazi bali ni nguvu zao za kimwili na akili.
 
Watanzania huwaga siwaelewi kabisa kipindi cha jiwe alipowafukuza watu walishangilia ooh walikuwa wamezidi kwanini wanakua na vyeti feki, ooh mara walikua wanaziba nafasi za wenye vyeti , sasa hivi ooh mama ana huruma , mama ni binadamu yaani kwa ufupi hatujui hata tunataka kitu gani sisi
Wabongo hasa Chaggadema ni genge la watu wapumbavu.

IMG_20211103_093523.jpg
 
Back
Top Bottom