Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Lakini hii serikali inatuonaje sisi wavuvi kata ya Kalya tulichomewa nyavu zetu na kuchukuliwa machine zetu za boat kimakosa kabisa tunalipwa lini tutendewe haki
Wavuvi hawana umoja. Mara nyingi miongoni mwao kuna wasaliti
 
4100 hawakufiji vyeti bali waliingia bila kukidhi vigezo vya ajira mfano mtu darasa la saba aliajiriwa na baadae kujiendeleza hadi kufika form four, huyu anastahili kurudishwa kwa kua hakufoji vyeti na hakuna jinai kwake
Uanapotosha makusudi magufuli wakati anahutubia watumishi kule bandarini aliwaambia kama wee ni lasaba ni umejaza lasaba hamna mwenye shida naye ila mtu la saba anafoji ni form four uki mwambia alete cheti cha form anaruka ruka
 
Kati ya 4000+ waliojiendeleza kielimu watakuwa wangapi? Waliofika mda wa kustaafu niwangapi?na zile stress mtu atajiendeleza kweli?

Wanasiasa wana udanganyifu sana
Si wamesema 4100
 
Kati ya 4000+ waliojiendeleza kielimu watakuwa wangapi? Waliofika mda wa kustaafu niwangapi?na zile stress mtu atajiendeleza kweli?

Wanasiasa wana udanganyifu sana
Hiyo kitu nimejiuliza sana!!
 
Rais achunguzwe pengine na yeye ni cheti feki. Kama umesota hadi kupata cheti kwa vyovyote huwezi kuoneo huruma mtu aliyefoji cheti kama chako na kupata faida kama uliyopata wewe au uliyokosa wewe kwa yeye kutumia cheti cha kufoji. Cheti feki wanastahili kua jela sio kurejeshwa kazini. Kwanza unawarejesha kwenye kazi gani maana hawakua na sifa kuajiriwa kwenye hiyo kazi?
Unachosema ni kweli mama nasikia ana vikozi vya kuunga unga balaa ndo maana naye anashadadia ujjnga .mtu anafoji chei then anarudishwa
 
Elimu yenyewe haina maana!cheti kina maana gani sasa!!kama form six leaver anaweza fundisha vizuri tu kuliko hata mhitimu wa chuo cha ualimu!!!!Hata form six failure anaweza kufunzwa udaktari tu na akawa deep tu bila kujali ufaulu wake!!?
Una uhakika na hiki
 
Ni wazi kabisa mtu akifoji kitu official huyu ni mualifu na adhabu yake inaweza kuwa kifungo mpaka miaka7.

Hamna kitu kinasikitisha kama mtu unahangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote unakomaa, halafu ajira aje kupewa mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ya kufoji vyeti, hii haiko sawa.

Nilitegemea Hawa watu wawe mfano wa onyo la kughushi vyeti lakini ndio kwanza wanarudishwa kazini, ni sawa na mtu aliefungiwa account yake benki alipokamatwa akingiza noti feki ila sasa anasamehewa na zile noti feki zinahesabiwa kuwa orijino.

Vijana kibao wapo mitaani wamesoma kwa shida ili kumaliza degree / masters, kiukweli hawatendewi haki hawa vijana, Binafsi sikuwa fan wa magufuli lakini kuna mambo machache sana aliyoyafanya nilikuwa upande wake likiwemo hili swala la kuchomoa wanao ghushi vyeti,

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora imetangaza kuwarejesha kazini Wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4000+) ambao waliondolewa kazini kutokana na kugushi vyeti katika maeneo mbalimbali lakini sasa kwa huruma ya Rais Samia watarejeshwa kazini kwa sharti la kuwa wawe wamejiendeleza kielimu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mohamed Mchengerwa amesema "wale walioweza kujiendeleza ambao ni zaidi ya 4100 tayari wamerejeshwa kazini, pia tunao Watumishi 1150 ambao hawakufanikiwa kujiendeleza maana yake hawana sifa za kutosha kuendelea kuitumikia Serikali japo walikua ni Watendaji wazuri”

Rais Samia alishatuagiza kwamba hawa 1150 kutokana na utendaji wao uliotukuka Watumishi hao wote walipwe haki zao na stahiki zao kama vile wapo kazini kwahiyo watalipwa"
Kosa la kimfumo lilishafanyika...siyo sahihi kuwatesa wa upande mmoja.....Mama anajaribu kufanya balance of nature
 
kwa sharti la kuwa wawe wamejiendeleza kielimu.
Hapa ndio mtego ulipo

Una masters ila ulifoji cheti cha 4m4 unajiendelezaje? Kuna ambao vigezo vitawatema ngoja tusubiri WARAKA tuone vigezo walivyoweka. USIAMINI saana maneno ya wanasiasa
 
Harafu wangetanabaisha kuwa watawalipa lin watu wajue si tu kuwa tutawalipa je ikifika 2025 au ndio wasubili? MATESO JE WALIO JINYONGA NA JE WALIO KUWA MUDA WAO WA KUSTAFU UMEFIKA JE NAO ITAKUWAJE WAACHA SIASA KILA KITU WAO WANAWAZA KUCHEZA NA AKILI ZETU
 
Kwa hiyo Kugushi cheti ni haki yao, kazi kweli kweli mwizi anapokuwa huru ingawa mmemkamata na vizibiti.
 
Back
Top Bottom