Rais Samia aweka rekodi ya Dunia. Tuna uwezo wa kuzalisha umeme hata mvua isiponyesha miaka 3. Lita bilioni 2 za maji bwawa la Nyerere zakusanywa

Rais Samia aweka rekodi ya Dunia. Tuna uwezo wa kuzalisha umeme hata mvua isiponyesha miaka 3. Lita bilioni 2 za maji bwawa la Nyerere zakusanywa

Uongo wa mchana kweupeee; si tupo Tanzania hi hi tupo. Nambie, kiwanda gani kikubwa kilianzishwa baada tu ya Kalemani kutumbuliwa?
Kuna waziri flani wa viwanda alisema ukiwa na cherehani 10 na kuajiri mafundi 10 wa kushona ni kiwanda.
 
Hivi ni serikali imeweka historia au ni Mama Samia?
Mbona neno Serikali sasa limekufa na limebaki la mama tu?
Mnajua hii ni aibu sana enyi watu?
 
Mchina ameleta generator za solar za KV 1000 na anauza bei ndogo mno.Hiyo inatosha kuendesha miji midogo,ndio maana generator za mafuta zimeshuka bei.Huu umeme wa maji tuendelee kuombeana akili zaidi,huenda kukawa na kilio
Hakuna kilio kitakacho tokea zaidi ya furaha na tabasamu kwa watanzania
 
Hivi ni serikali imeweka historia au ni Mama Samia?
Mbona neno Serikali sasa limekufa na limebaki la mama tu?
Mnajua hii ni aibu sana enyi watu?
Ni Maono ,akili ,maarifa, dhamira , ujasiri na uthubutu wa Rais Samia ndio umewezesha mambo haya makubwa kukamilika
 
Mwenye Bwawa lake anajulikana; Afrika; Uarabuni na dunia nzima inamfahamu. Mwenyezi Mungu amrehemu
Yule mzeee hata maadui zake sasahivi wanamshukuru ndo wanaanza kumuelewa ahaaa ahaaaaa , ni binadamu alikuwa na mapungufu yake machache lakini kaacha alama kuliko watangulizi wake wote
 
Hahaha rekodi ya Dunia nenda China kaone hizo Dams zikoje ,,, baada ya kuvunja record kwa bwawa kubwa la kuzalisha umeme Duniani wanavunja rekodi yao wenyewe tena wanajenga lingine...hapo kumbukaa lile la kwanza lime impact adi mzunguko wa Dunia ...usisahau wametengeneza tayari jua Lao ambalo ni zaidi ya jua hili halisi
 
Mradi Ni wa shujaa JPM Na mvua Ni ya Mungu hayo mengine Ni mapambo ya sanamu
Huu ni mradi wa serikali na ulikuwepo toka enzi ya mwl. Nyerere. JPM alianza utekelezaji wake kama rais aliyepewa dhamana na wananchi wa JMT. Tujifunze kutofautisha vitu binafsi navya serikali.Kumekuwa na slogan Rais Samia katoa pesa billion kadhaa badala ya kusema serikali imetoa.
 
Julius Nyerere Hydro power itabaki daima kuwa legacy ya Magufuli, Samia hahusiki aje na yake, matundu ya choo ile ni aibu na upotevu wa pesa
 
Back
Top Bottom