Rais Samia azindua daraja la Selander (Tanzanite), ataka liwekewe nembo ya Tanzanite sio Mwenge

Wazee wa propaganda wa Sisiemu wanafeli sana...

Rais kila siku yuko kwenye runinga.
 
Maamuzi ya hovyo ya serikali ya awamu ya tano. Utajengaje barabara ya kilomita moja kwa sh, 243 Bilioni katikati ya nchi maskini km Tanzania ambapo bado mikoa na wilaya karbu zote ni barabara ya vumbi eti unapendezesha mji wa DSM? Ni sawa na mradi wa daraja la Kigogo-Busisi unaogharimu zaidi ya Bilioni 700 kwa urefu wa k 3.2 tu! Kisa viongozi wao wanaishi katika hiyo miji mikubwa. Huu ni ubaguzi na unyanyasaji mkubwa kwa watanzania. Hebu angalia mji kama wa MBULU ULIOJENGWA MWAKA 1905 mpaka leo haufikiki kwa barabara ya lami ni umbali wa km 75 tu, gharama yake haifiki hata Bilioni 100. Nenda kaangalie vumbi liliko meneo km Loliondo, Kiteto, Simanjiro utafikiri ni maeneo ambayo bado hajapata Uhuru. Rais pekee nitakayemkumbuka ktkt maisha yangu ni JAKAYA MRISHO KIKWETE. HUYU MZEE HAKUONESHA HATA TONE LA UBAGUZI WA AINA YEYOTE. HAYATI MAGUFULI NDIO MUASISI WA HUU UBAGUZI NA MAMA BILA KUSTUKIA ANAUENDELEZA. SUBIRINI MTASTUKIA MMESAGAWA NCHI. MSIJEFIKIRI WA TANZANIA WANAOTAABIKA KTK BARABARA ZA VUMBI TANGIA NCHI IPATE UHURU WANAFURAHIA KUSHUDIA MAENEO MENGINE ZINAJENGWA BARABARA JUU YA BAHARI NA MAZIWA. HUKU NI KUWADHARAU, KUWAPUUZA, KUWABAGUA NDANI YA NCHI YAO. HT MRADI WA SGR UNA MSAADA MDOGO SANA KTK NCHI HII. NI MRADI UNAOPITIA KTK MIKOA MICHACHE SANA WAKATI HUKU MAENEO MENGI YA NCHI HII WANANCHI WAKITAABIKA NA VUMBI NA MATOPE NYAKATI ZA MVUA
 
Nilikuwa nawaza
Nilikuwa nawaza ule mwenge pale darajani una maana gani.
 
Hongera sana, huo ndio ubunifu wenye tija, sio kila siku majina ya viongozi tuuuu,
Mfano hiyo tanzanite daima itajulijana na kila ajaye,
Ila jina la kiongozi baada ya muda linakuwa jina tu ila athari yake haipo,
Kama ambavyo watoto wa siku hizi wasivyojua viongozi waliopita
 
Haikuwa Mingi kama Ya Jpm Tena Ukilinganisha na Mtu alokaa Madarakani

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni kenge,unaweza nipa idadi ya miradi aliyozindua Samia na mimi nikupe ya Mwendazake.

Mwendazake hadi baada ya miaka 3 alikuwa anazindua miradi iliyokamilika enzi za JK tena miaka Zaidi ya 3 mbele tofauti na Samia anaekamilisha yeye nakuizindua.

Kiufupi yule mtu wenu hakuna mradi alikamilisha kwa miaka 6 yote.
 
Wazee wa propaganda wa Sisiemu wanafeli sana...

Rais kila siku yuko kwenye runinga.
Akisafiri mnasema,akienda kuzindua mnasema.

Kwanza naunga mkono hoja Rais azindue miradi mingi kadiri inavyowezekana ila tunaomba aje na mikoa mingine.

Kwa mda sasa amekuwa akitembelea Dar,Dom,Kaskazini , Lake zone na Zanzibar.

Kusini,magharibi na Nyanda za Juu sijamuona.
 
Sensa imewekwa mwezi wa kumi tena. So necta na tamisemi wajiandae kurekebisha ratiba zao??
 
Hii inamantiki, ahsante mama kuliona hilo
 
Spesho = maalum?
 
Leo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassana amefanya uzinduzi wa Daraja la Tanzanite .

Katika uzinduzi huo Mhe Rais. amesema mradi huo unagharimu zaidi ya Dola za za kimarekani 123 .

Aidha Mhe Rais amesema kukamilika mradi huo pamoja na miradi mingine itapunguza kero ya msongamano kwa kiasi kikubwa ambapo kutachochea ukuaji wa uchumi na biashara .

Mhe Rais aliwataka wizara wahakikishe wanakarabati madaraja "Wizara wahakikishe barabara na madaraja yanafanyiwa matengenezo stahiki kwa Muda muafaka na sisi serikali tutafanya jitihada za kutafuta fedha za kutosha kwa ajili ya matengenezo ya barabara zetu zote Nchi nzima." Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan

Mhe Rais alitoa ushauri juu ya uwekwaji wa umbo la Tanzanite katika daraja "Ushauri nilioupata Kwa wananchi daraja hili tunaliita daraja la Tanzanite, lakini alama tuliyoiweka ni alama ya mwenge ni tunu yetu adhimu wananchi wangependa sana kuona umbo la Tanzanite pale ulipo mwenge Ili kukamilisha jina la daraja hili." Mhe Samia Suluhu Hassan.

#AlipoMamaVijanaTupo
#2022JiandaeKuhesabiwa
#KaziIendelee
 

Na akija nyanda za juu tutasema pia,, Binadamu hatuwezi acha kusema,, tumeumbwa kusema na midomo hio ndio kazi yake.

Ujumbe wako tutafikisha kwa Rais, na hivi karibuni atakuja na huko mikoani kwenu..

Just Relax.
 
katika uzinduzi wa daraja la Tanzanite mama amesema kuwa WATANZANIA WANATAKA daraja liwe na alama ya tanzanite kama lilivyo jina lake.
swali la msingi hao watanzania waliosema wanataka hvyo ni kundi lipi ? Kundi la wamtandaoni au wasio wa mtandaoni?
Kundi la wanachama au kundi la wasio wanachama?

Ukifungua kila mtandao wa kijamii utakutana na takwa la watanzania kwa wingi wao.
Ukizungumzia mambo ya uzalendo au siasa au vyama vya siasa bila mtandao utakutana na takwa kubwa la watanzania

Kwasasa watanzania wamenyamaza kuhusu kupandishwa vyeo , kuhusu kuongezwa mishahara , kuhusu uhuru wa kuongea
sasa hivi mambo makuu ambayo wananchi zaidi ya robo 3 wanahtaji kujua ni
1, HATMA YA KUPANDA KWA BEI ZA BIDHAA MUHIMU.
2. KATIBA MPYA
Kusema kuwa wanamchi wanataka alama za tanzanite kwenye daraja hapo ni kuwadanganya watanzania hao hao ambao hawawezi kudanganyika kwa kuwa hizo alama hazitapungu mafuta lita moja kuuzwa 8000.
mama sema na ufanye kile wananchi wanataka kusikia na si kuwapeleka kwenye matakwa yako
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…