Rais Samia azindua daraja la Selander (Tanzanite), ataka liwekewe nembo ya Tanzanite sio Mwenge

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Agakhan - Upanga jijini Dar Es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua daraja la Selander (Tanzanite) na barabara unganishi leo tarehe 24 Machi 2022.

===
Rais Samia Suluhu Hassan ametaka alama ya Mwenge katika Daraja la Tanzanite iondolewe na iwekwe alama ya Tanzanite ili watu waione inafananaje. Rais amesema Mwenge ni tunu ya nchi, lakini wananchi wametaka Tanzanite ili kukamilisha jina la Daraja hilo

Pamoja na hayo Rais ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika Oktoba 2022
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Agakhan - Upanga jijini Dar Es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua daraja la Selander (Tanzanite) na barabara unganishi leo tarehe 24 Machi 2022.

Hua nchi zingine wanaposema Rais wao yupo kwenye ziara flani, wanataja na chama anakotoka? achilia mbali wadhifa yake ndani ya chama.

Hii tabia ipo Tanzania tu, sometimes mnashusha sana hadhi ya Rais wa nchi kwa kutajataja Mambo ya uchama ndani yake.
 
Ila Kwa kupendezesha mji sawa,ila Kwa msaada sidhani,añgekuwa anazindua leo Jangwani hapo nadhani ingekuwa fahari zaidi ya kule salenda
Inchi nyingi zilizoendelea lazima ziwe na barabara zaidi ya moja ya kuingia mjini.

Hvi Mfano daraja la salender lingekuwa halipo,

Leo watu wangekwendaje mjini na jangwani kumejaa maji?

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Ila Kwa kupendezesha mji sawa,ila Kwa msaada sidhani,añgekuwa anazindua leo Jangwani hapo nadhani ingekuwa fahari zaidi ya kule salenda
Ila ninachopendea siku za uzinduzi miradi, ni kwamba huwa ni siku za kutoa ahadi na matamko mapya yenye manufaa baadae

Inawezekana kabisa leo akaahidi na kutoa tamko kuwa ujenzi wa daraja la jangwani uanze maandalizi mara moja. Inawezekana kabisa.
 
Mbeleni itachosha kumwona Rais kila siku kwenye headlines.

Ikifika 2025 atakuwa hana jipya, hana upya, hana mvuto. Ni jambo la kufikiria.

Kwamba ni miradi ya awamu ya 5, yeye alikuwa sehemu muhimu ya urais tena kikatiba "presidency " kwa hiyo tusimtenganishe.

Tumpe haki anayostahili.
 
Wanataka kumnyanyapaa na kumbagua kila wanapoishiwa hoja za msingi za kujadili.
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Agakhan - Upanga jijini Dar Es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua daraja la Selander (Tanzanite) na barabara unganishi leo tarehe 24 Machi 2022.

Huu sio uzinduzi bali ni kampeni za 2025. Mama hajiamini ila ana uchu wa madaraka
 
Back
Top Bottom