#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

Mama ameamua wajameni sasa ni mwendo mdundo, haya ndio maendeleo ya kwelii.

#UTAIFA MBELE
#TWENDE NA MAMA
Noma sana saizi hata ukienda hospital una uhakika wa vifaa tiba.

By mwaka ujao wa fedha yaani bajeti ijsyo nakwambia wonders hasa kwenye ajira.

Watu waliosoma sekta ya Afya na elimu waandae vyeti
 
Ahahahaaha yaani nyie watu,hayo yote si ni matamanio tu,shida ni utekelezaji,shida yetu kama Taifa ni usimamizi wa matamanio yetu
 
Watu wa pwani wanapenda sana sherehe,ila Mkapa hakuwa mtu wa Pwani,haya mambo wangeweza kufanya tokea ikulu na mawaziri wachache tu
Nyie tukiwazoea,ni historian hiyo ndio maana inakuwa sherehe..MRI machine 29 kutoka 2 wewe unaonaje hapo?
 
Wakati Corona inatafuna watu na kuwaondoa ndugu zetu mliaminisha UMMA kwamba haipo sasa hivi imesubside (tuliobaki tumepata immunity nayo) mnaanza kuitafuta.... Madhara ya Siasa kwenye vitu muhimu ni makubwa sana..., alafu wanashangaa credibility yao / Uamifu kwa wananchi ukipungua...

Lets always call a Spade a Spade vinginevyo ni kuwachanganya wananchi na siku kweli wakihitaji ushauri / mkiwashauri huenda wasiufuate... (Na hio ni Hatari Sana)
 
wale waliokuwa wanabeza safari za mama waje hapa
Wameaibika,afu Waziri kasema Wengine wamekopeshwa kwa riba kubwa sisi ni pesa za bure na mkopo wa riba ndogo.

Kuna zingine za kuimarisha reserves za forex ya nchi zinakuja tril.2.2 hivi maana Hali ya Uchumi ilianza kuanguka..

Juzi tuu Sida wamemwaga mabilioni yaani saizi nchi yote ni site ya Ujenzi..

Bajeti ya Mwaka ujao itakuwa kubwa Sana hasa kwenye miundombinu,maji,ajira nk Kwa sababu mzigo mkubwa utakuwa umepunguzwa mwaka huu
 
Hayo yote aliyoyasema Waziri wa Fedha yatatekelezwa. Hizo fedha zitatosha kweli???

Au kuna fungu lingine tofauti na hilo.
 
Naona wameandaa na nyimbo za kusifu.
Ni siasa tu[emoji706].
 
Hayo yote aliyoyasema Waziri wa Fedha yatatekelezwa. Hizo fedha zitatosha kweli???

Au kuna fungu lingine tofauti na hilo.
Mkuu sh Til 1.3 less bil 130 ya Zanzibar unabakia na karibu 1.17 T,,hapa pesa za ufuatiliaji na utawala ni hizo bil 170 ,kwa hiyo Til.1 ni bil.1,000 ni pesa mingi Sana.

Kwenye afya ni bil 460,Maji bil.102,Elimu bil.200 hizo zingine huko kuliko Baki kwa hiyo pesa inatosha Sana mkuu.
 
Yaleyale ya Mquere!!!

Kilimo kwanza😆😆😆
Big results now😂😂😂
Tanzania Beyond Tomorrow🤣🤣🤣
 
Naendelea kufatilia tukio hili ambalo liko Mbashara.

Maeneo yaliyonufaika na fedha hizi ni Huduma za jamii i.e Afya, Maji na Elimu. Licha ya kuwa fedha hizi zitakwenda kuhudumia maeneo hayo matatu lakini ni matumaini yangu fedha hizi zitakwenda kuongeza mzunguko wa fedha mtaani. Tunajua ukata uliopo mtaani, hivyo kupitia shughuli za Ujenzi wa Vyumba vya madarasa, vituo vya afya, miradi ya Maji n.k iwe kupitia Ukandarasi, Uzabuni, Local Fundi fedha hizi zitakuja mtaani

Kiukweli nitumie jukwaa hili kumpongeza Mhe. Rais kuhusu mgawanyo wa fedha uliofanyika hasa maeneo ambayo zimeelekezwa.

Wahandisi, MaQS let's join hata kuwa Local Fundi kupiga hizo deal za Ujenzi
 
Yaleyale ya Mquere!!!

Kilimo kwanza😆😆😆
Big results now😂😂😂
Tanzania Beyond Tomorrow🤣🤣🤣
Tulia sindano za Samia zikuingie,Samia ndio ataweka historia kubwa nchi hii..

Magu alikopa na kupewa msaada bil.600 za covid,kaulize sasa zilikoenda kama utapata majibu..

Mungu alituona akamuwahisha haya sasa ndio matokeo kwa hiyo wivu utakuua.
 
Wizara ya Fedha na BoT wajitahidi kudhibiti mfumuko wa bei maana hii ni Neema kwa watu wa sekta ya ujenzi,manunuzi,zabuni nk..
 
kuongoza Tanzania n kazi watu wanamuonea wivu hadi Rais wa nchi
 
Kuzindua kampeni ya maendeleo ndo kitu gani??
Mama anatapatapa au hana washauri wazuri
 
Naona Mpoto anapokea mahela tu hapa et tusisubiri Chanjo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…