#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

Walishaanza kutapanya pesa za msaada toka kwa Mabeberu kuhusu korona, Naona wameanzisha tamasha ili kuwahadaa mabeberu kuwa pesa walizopata za IMF wanachukua hatua

Danganya toto Jinga


Sasa mbona jambo la kitaifa na la kiserikali limegeuzwa la chama

Haya mambo yanachekesha sana na yanarudisha nyuma sana hamasa na maendeleo

Meza zimewekwa bendera ya CCM na baadhi ya watu wamevaa sare za ccm

Kuna watu wakisikia neno ccm wanazima TV na kuondoka, Hawaitaji porojo na uwongo wa ccm

Unapohimiza mambo ya kitaifa kama chanjo, Kampeni za malaria, Kampeni za watu kuwa matajiri, Au kampeni za elimu yakupasa kusimamia Sera za Taifa

Watu ambao hawana chama ni wengi kuliko wana ccm au Chadema


CCM walisema tuchape kazi Corona hakuna na waliwacheka Chadema waliohimiza kuwa corona ipo na itaondoka na watu ikiwemo viongozi


Leo ccm inapiga kampeni ya chanjo ni wajinga waliopindukia na watu wasiojitambua wanaweza Sikiliza ujinga huu


Nashauri viongozi waombe radhi wananchi kwa kuwajaza upepo kuwa korona hakuna na ni kama mafua ya ndege


Humprey Polepole bado anahubiri hakuna korona na amesimama na msimamo wa ccm


Sasa Je Pesa za IMF zimetumikaje?

Mtuambie pesa mlizopata za IMF mmeajiri madaktari wangapi kama mkataba unavyotaka


CCM wanahubiri mapambano ya corona, Pathetic

CCM mlikuwa wapi mmesubiri mpaka watu wameondoka, Mlihimiza Bunge liendeleee na waliotoka bungeni wakatwe pesa
Kama umewahi kufanya kazi taasisi za kimataifa
Inauguration ni kitu kinachopewa kipaumbeke na huwa na bajeti yake
Kinachofanyika ni public advocacy ambacho ni kitu muhimu sana
Kila activity huwa na budget cost kwaio wako ndani ya bajeti
 
Inapelekea huu mkutano wa Leo uzinduzi wa kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 umetumia fedha nyingi sana. Nikifuatilia utangulizi wake utangamua Hilo kwa idadi kubwa ya waalikwa
 
Ndio nauliza kweli tupo serious kabisa tunapambana nao ? Au tunafanya sarakasi ili kukidhi matakwa ya kupokea misaada ? Vyombo vya usafiri vinajaza nyomi kama kawaida, viwanja vya michezo, kkabu,bar...sioni mtu anayehangaika na UVIKO-19 kwa sasa

Hivi kweli cccm wanadhani watanzania vyote vichwa vyetu ni urembo tu si vya kufikiri? Punguzeni huo ujinga wenu japo kdg jamani.
 
Unalakubadilisha au unatuita ili tupige udaku kwa pesa waliotumia wakubwa..?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo 10 Oktoba 2021.​

Fuatilia matangazo hapa


Rais Samia huwa anaswali lini na wapi? Kuuliza sio ujinga​

 
Mama ameamua wajameni sasa ni mwendo mdundo, haya ndio maendeleo ya kwelii.

#UTAIFA MBELE
#TWENDE NA MAMA
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo 10 Oktoba 2021.​

Fuatilia matangazo hapa


Kwa nilichokisikia kwa Waziri wa Fedha mama ameifanyia sekta ya Afya overhal ,haijawi kutokea hii.

Maji saizi ni kila sehemu,madarasa 18,000 ..ma Veta,noma sana nchi nzima itakuwa construction site safi Sana Mungu ambariki.

Nchi hii imekopa pesa miaka mingi ila tija yake hajakuwa kubwa sasa,sasa Tilioni moja imeibadili sekta ya Afya,elimu na maji kuwa yenye tija kwa umma.
 
Back
Top Bottom