Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Ikulu mpya iliyopo Makao Makuu ya Nchi, Dodoma, leo tarehe 20 Mei, 2023.
HUSSEIN MWINYI, RAIS WA ZANZAIBAR
Nampongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mafanikio haya ya ujenzi wa majengo mapya ya Ikulu ambayo ni miongoni mwa hatua za kuendeleza dhamira za Baba wa Taifa, hayati Mwl. Julius Nyerere kupitia chama cha TANU mwaka wa 1973 ya kuweka azimio la kutaka Dodoma iwe Makao Makuu ya Serikali.
Hivi sasa sote tunashuhudia mafanikio ambayo tumeweza kuyapata katika utekelezaji wa mpango huo, ikiwemo leo katika ufunguzi wa Ikulu hii mpya hapa Chamwino jijini Dodoma.
Natumia fursa hii kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuipatia Serikali ya Mapinduzi Zanziba eneo hapa jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zake. Naahidi kuwa sisis nasi tutajenga ofisi za SMZ hapa Dododma ili kuwawezesha Watumishi wetu kupata mazingira bora ya kufanyia kazi.
Nikushukuru Mheshimiwa Rais kuwa katika Ikulu hii pia kumetengwa nafasi, au tuseme Ofisi ya Rais wa Zanzibar.
DKT. PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA
Mh. Rais, Ikulu ulioizindua ni lulu ya Tanzania. Ni jingo lenye hadhi ya nchi yenye kipato cha kati. Nami naona ni taa ya kuipeleka nchi yetu ndani ya kipato cha juu ndani ya kipindi kifupi.
Ikulu hii ni kazi ya vichwa vya Watanzania. Ni kazi ya mikono ya Watanzania. Ni kazi ya kodi za Watanzania. Kwahiyo hongereni sana kwa kazi nzuri ya kupata Ikulu mpya yaChamwino.
Nawaomba (Watumishi wa Ikulu) jengo lile liheshimiwe. Na jingo lile litunzwe vizuri.
SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA TANZANIA
Tukio hili ni adhimu na kuleta faraja kwani kwa mara ya kwanza Watanzania tumeweza kujenga Ikulu yetu kwa kutumia rasilimali zetu na kutumia wataalamu wetu wa Kitanzania. Hii ni tofauti na Ikulu yetu ya Dar es Salaam ambayo ilielezwa vizuri hapa.
Sasa ndugu zangu, katika mchakato huu ni nguvu za awamu zote ziliingia katika mchakato wa kuifanya Dododma kuwa Makao Makuu yay a Serikali na kuwa Mji Mkuu wa nchi yetu. Ni ngu za awamu zote. Kabla sijaendelea nimkaribishe Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.
JAKAYA KIKWETE, RAIS MSTAAFU WA TANZANIA
Leo historia imeandikwa, na imeandikwa kwa wino wa dhahabu. Hili ni jingo ambalo tumelijenga wenyewe. Wataaalamu wetu walichora. Wakasanifu. Tumetoa pesa zetu wenyewe kujenga na leo limekamilika.
Tukio hili umuhimu wake ni kuwa linahitimisha dhamira ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu kutoka Dar es Salaam kuyaleta katikati ya nchi hapa Dododma. Uamuzi ulifanyika mwaka 1971 lakini leo Mama yetu, umekamilisha.
Kilele cha uamuzi ule ni Rais kuhamia Dododma. Na si kuhamia Dododma kwa kupita tu, lakini Rais kuwa na ofisi yake Dodoma. Katika kila awamu kuna yaliyofanyika.
Katika kipindi change uamuzi wa msingi tulioufanya ni kuamua kwamba Ofisi ya Rais na makazi ya Rais yatakuwa hapa Chamwino. Wazo lililokuwepo mwanzoni ni kwamba pale Chimwaga ndipo yatakapokuwa makao makuu ya TANU na makao makuu ya Serikali.
Mimi nilipokuja nikaamua pale tujenge chuo kikuu. Kulikuwa na mjadala, mawazoo yalikuwa mengi lakini nikasema tutajenga chuo kikuu Dododma.
Baada ya kuwa pale tumepatumia kwaajili ya chuo kikuu, Tulifanya mkutano na CBA. Mh. Lukuvi alikuwa Waziri wa Ardhi. Nikamwambia Ofisi ya Rais na Makazi ya Rais yajengwe Chamwino. Na ofisi za mawaziri zijengwe karibu na hapo.
Niliwaamba waende Kuala Lumpur. Kuala Lumpur, Malaysia wamejenga makao ya Serikali. Na kule walipojenga makao ya Serikali ndipo yalipo makazi ya Waziri Mkuu, ya Mfalme, huko huko. Nikawaambia nendeni mkaone. Na wamejenga vizuri. Unapita majengo ya ofisi za mawaziri halafu juu yake mwishoni ndiko ofisi ya Rais. Wamekwenda wamefanya hiyo kazi na ndiyo hii tunaiona sasa.
Rais wa Awamu ya Tano ndiyo ametoa msukumo mkubwa wa ujenzi.