Hakuna Rais aliyekuwa hana miradi. Tuache dharau.
Daraja la wami Hilo hapo. Kajengewa hukumbuki tu. Na liko hapo mtaani kwake alikuwa hakumbuki kuna Tatizo la daraja na mamia kwa marefu walifia wami.
 

Attachments

  • 4084756A-0AD6-4A46-B665-50B7A65FEE46.jpeg
    334.3 KB · Views: 6
Kwa hiyo wameona kumtaja john pombe magufuli kama ndiye muasisi wa ujenzi wa hiyo ikulu ni nuksi au?
 
Ni kweli. Mama anapambana sana kuona hii miradi inakamilika. Ila kutoona kazi ya mtangulizi wake nayo pia ni dhihaka.
Kuna awamu nyingine watu walikuwa busy kulamba asali. Maendeleo kidogo tu. Tusisahau hilo pia. Watanzania wa leo sio wa juzi
Watanzania ifike hatua muache ujingaujinga, kwenye mradi wowote ule wanaotajwa wakati wa ufunguzi ni taasisi na mkuu wa taasisi wa wakati huo.

Tukitaka kuwataja watu kwa majina walioshiriki itabidi muwataje wakuu wa taasisi walioshiriki tokea awali pamoja na mawaziri na makatibu wakuu waliokesha usiku wakihakikisha kazi ya ujenzi inaanza na kutekelezwa ipasavyo wengine walishaondoka kwenye hizo nyadhifa zao. Kazi walizotekelezwa watapata pongezi internally ndani ya taasisi zao.

Punguzeni ujuaji, hii inaleta picha kuwa hakuna kiongozi anaweza kuanzisha mradi utakaomalizika baada ya miaka 40 kisa tu Jina lake halitatajwa wala yeye kunufaika. Ujinga mtupu.
 
Wewe ndio utumie akili. Watu wakuogope halafu waminye kukupa heshima yako?. Yani wakatae kukupa unachostahili?. Hapo wamemdharau makubwa maana waliona Kama hastahili kutajwa hata kidogo.
Wao ndiyo wanamdharau je wananchi kwa ujumla wao nao wanamdharau jpm ? ....ndiyo maana nikakuambia wanaogopa
 

Kama tunataka taasisi ndio iheshimiwe, basi tuache kuingiza siasa kwenye miradi ya umma. Ukianza kutaja majina, hakikisha majina sahihi yanatajwa.
Hii nchi kupewa uongozi toka lini imeacha kuwa ni dhamana na sio kuwa special talent or person?
 
Yaani Wote hawakutambua chochote kuhusu Magufuli kwenye ujenzi wa Ikulu ya DODOMA , ila mwishoooni Kwenye hitimisho Rais Samia ndio kafurukuta kumtaja, japo kwa taabu !
Hata wewe usiyempenda Magufuli imekushangaza eeh?! Ndiyo maana waswahili walisema ukistaajabu ya Musa utaona ya filauni.
 
Leo historia imeandikwa, na imeandikwa kwa wino wa dhahabu. Hili ni jingo ambalo tumelijenga wenyewe. Wataaalamu wetu walichora. Wakasanifu. Tumetoa pesa zetu wenyewe kujenga na leo limekamilika.
Hii ndiyo 'audacity'/uthubutu wa kipekee kabisa ambao ungetakiwa kujengewa heshima kuu na kila kiongozi wa nchi hii.

Isiwe ni maneno tu ya kusema mbele za watu, na tukitoka hapa tunakwenda kulialia kwa kila jambo dogo kutafuta tusaidiwe.

Hii ndiyo tabia inayotakiwa kujengeka ndani ya nchi yetu. Tabia ya kuamini "TUNAWEZA".
 
Kama tunataka taasisi ndio iheshimiwe, basi tuache kuingiza siasa kwenye miradi ya umma. Ukianza kutaja majina, hakikisha majina sahihi yanatajwa.
Hii nchi kupewa uongozi toka lini imeacha kuwa ni dhamana na sio kuwa special talent or person?
Nadhani upo sahihii, mfano mimi ningeshiriki hapo kwa kutoa technical advice...je na mimi nitajwe Jina? Jibu ni hapana bali itajwe taasisi iliyoniteua kufanya hiyo kazi. Then ndani ya taasisi ndiyo zawadi itakuja kwangu, tuacheni kujenga taswira ya majina ya watu kisa wanasiasa...inavunja moyo wale watekelezaji.

Nchi zilizoendelea hawakuendelea kwa kufanya haya mnayoyashabikia...Kuna mabwawa ya kuzalisha umeme zilichukua zaidi ya miaka 20 kujengwa lakini hawakuhishania kuongozi flani ametenda zaidi ya mwingine.

Tukiacha sisi waendesha ushabiki ata hao wanasiasa wataacha tu...make wanaenda na ngoma zetu wapiga kura.
 
Pongezi kwako mzalendo Magufuli na vijana wa jkt japo kuwa chawa wa mama wanapindisha ukweli ili mama aonekae kaijenga yeye.
Sio tu kupindisha ukweli, huyo muhuni wa Msoga anasema ni yeye ndio alipanga yote na huyo mpango wake wa kando ndo kakamilisha? Au nimesoma vibaya?
 
Wakristo tuna visa kwerikweri 😂😂
 
Nimechelewa kwenye huu mjadala ila nina maswali mengi kuhusu hii Ikulu. Kwanza nnauliza, Ikulu ya Dodoma inazinduliwa mara ngapi? Mbona kumbukumbu zangu zinaniambia ni zaidi ya mara moja shughuli kama hii imeshafanyika na pia leo ni kama ni uzinduzi wa JENGO kwa maana hiyo inawezekana kukawa na uzinduzi mwingine siku za mbele.
 
Majengo yanaonekana vizuri mahali wanapokosea ni ile barabara ya njia Moja kuingia na kutoka! Je hiyo nafasi yote wameacha ya Nini? Kwa Nini wasingeliiweka pana walau mbili kuingia mbili kutoka!
Haya ndio makosa ya kutokuwa na mpango wa miaka 50 mbele!
Wabunifu hakuna.
 
Siku zote jua halijawahi kudanganya kazi yake kubwa ni kueneza mwanga, si jukumu la jua kujisemea kazi yake, huwezi kumulika au kuwasha taa kwenye mwanga.

Siku zote giza linafukuzwa na mwanga, ukitaka kujua utamu wa muwa kutana na pingili...

Asante kwa viongozi kuzindua ikulu ya Dodoma, ninaamini isingekuwa kamba kufungwa vizuri kwenye kishina huenda mzigo ungelemea kamba na kukatika na kiukweli mzigo ungepolomoka.
 
Kwa jinsi mambo yalivyo, sidhani kama kuna uelewa huo.

Dhamana ya uongozi ni tofauti na huu mrizamo uliopo. Ndio maana hata haya mambo yanayotusaidia sisi sote na watoto wetu, inapnekana kama vile ni zawadi ambayo kiongozi anaamua aitoe. Hivyo kutajwa ni lazima.
mimi sifagilii kabisa hayo. Ukweli utuweke sote huru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…