Covid-19,imesababisha uchumi wa dunia kusinyaa,kwa hiyo IMF kwa kuliona hilo, ndiyo iletenga mabillions ya dola ili kusaidiwa mataifa yenye uhitaji kupambana na COVID-19,ili mataifa hayo yarejee kwenye uzalishaji.
Mashariti ya mkopo ilikuwa kupambana na kutokomeza covid-19,(Chanjo,vifaa tiba na miundo mbinu ya afya), mataifa mengi yaliyotangulia kuchukua mkopo huu,wao walenga kutimiza sharti hili la IMF.
Lakini Tanzania, ndiyo wakajenga hoja kuwa,ili kutokomeza covid-19,ni dhana Pana,siyo kununua chanjo na vifaa tiba (mitungi ya gesi).bali linaanzia na wafunzi wa Shule za msingi na sekondari ambao,wanabanana madarasani au kukaa sakafuni,au kupanda daladala kila siku kwa ukosefu wa mabweni,Ni vema wakapata madarasa ya kutosha, madawati na mabweni na vitanda,kwa kufanya hivi,tutakuwa tunapambana na maambukizo ya covid-19.
Serikali iliona kuwa ili kupambana covid-19,inahitaji maji tiririka,kwa kwa kuwa Tanzania,miji na vijiji vingi havina maji safi,kwa hiyo walio Ni busara sehemu ya fedha hizo zielekezwe kwenye maji Safi.
Mwisho, ndiyo mapambano halisi ya covid-19,kwa kujenga vituo vya afya,magari, mitungi ya gesi, mitambo ya kupima maradhi nk.
Kwa kuwa Tanzania,ilifanyia maboresho ya mashariti ya mkopo,ilibidi Mtukufu Rais akutane na Rais wa IMF na Rais wa IMF Kanda ya Africa,kuwashawishi,na hatimae kuridhia kufanya marekebisho ya mashariti ya mkopo.
Ushauri
(1). Pamoja na IMF kuridhia maboresho ya mashariti ya mkopo Ni vema serikali,ikatimiza madhumuni ya mkopo,kutokomeza covid-19,ili dunia ianze uzalishaji
(2). serikali Ni vema ikaajiri watumishi wa kutosha kwenye hivyo vituo vya afya na hospital, watakao toa huduma hizo, vinginevyo Ni kazi bure,kuna Upungufu wa madaktari na wauuguzi,na watalaam wengine,lakini wataalaam hao wako madaktari wote watakao maliza intern waajiriwe Mara moja,Kama ilivyo kuwa mwaka 1978, wakati wa vita ya Uganda, wanafunzi ambao walikuwa JKT kwenye mafunzo na mgambo walikwenda mstari wa mbele.
(3). Serikali iwalipe posho ya majanga (risk allowance) wafanyakazi wa sekta ya afya,wanao fanya kwenye kitengo Cha magonjwa ya milipuko.
(4).Tunatahadharisha,hayo majengo na mashiñe zisije kuwa mapambo, badala ya kufanya kazi iliyokusudiwa.