Rais Samia bado anapotoshwa, hajapata washauri wenye weledi

Baada ya Rais Magufuli kufariki, Tanzania tumepoteza mwelekeo tulitegemea mama atakuwa kiongozi ila nimeshangaa nae kawa mwanasiasa anafanya maamuzi kufikiria uchaguzi wa 2025.
Chini ya Magufuli tulikuwa tunaelekea shimoni sasa hivi haieleweki tunaenda wapi ?
 
Kwahiyo wewe ndio unajua kuliko wataalamu wote serikalini ????

Wabongo bana.
Mkuu hao wataalamu serikalini ndiyo walioshauri serikali kuweka tozo kubwa kwenye miamala ya simu?
 
Covid-19,imesababisha uchumi wa dunia kusinyaa,kwa hiyo IMF kwa kuliona hilo, ndiyo iletenga mabillions ya dola ili kusaidiwa mataifa yenye uhitaji kupambana na COVID-19,ili mataifa hayo yarejee kwenye uzalishaji.
Mashariti ya mkopo ilikuwa kupambana na kutokomeza covid-19,(Chanjo,vifaa tiba na miundo mbinu ya afya), mataifa mengi yaliyotangulia kuchukua mkopo huu,wao walenga kutimiza sharti hili la IMF.
Lakini Tanzania, ndiyo wakajenga hoja kuwa,ili kutokomeza covid-19,ni dhana Pana,siyo kununua chanjo na vifaa tiba (mitungi ya gesi).bali linaanzia na wafunzi wa Shule za msingi na sekondari ambao,wanabanana madarasani au kukaa sakafuni,au kupanda daladala kila siku kwa ukosefu wa mabweni,Ni vema wakapata madarasa ya kutosha, madawati na mabweni na vitanda,kwa kufanya hivi,tutakuwa tunapambana na maambukizo ya covid-19.
Serikali iliona kuwa ili kupambana covid-19,inahitaji maji tiririka,kwa kwa kuwa Tanzania,miji na vijiji vingi havina maji safi,kwa hiyo walio Ni busara sehemu ya fedha hizo zielekezwe kwenye maji Safi.
Mwisho, ndiyo mapambano halisi ya covid-19,kwa kujenga vituo vya afya,magari, mitungi ya gesi, mitambo ya kupima maradhi nk.
Kwa kuwa Tanzania,ilifanyia maboresho ya mashariti ya mkopo,ilibidi Mtukufu Rais akutane na Rais wa IMF na Rais wa IMF Kanda ya Africa,kuwashawishi,na hatimae kuridhia kufanya marekebisho ya mashariti ya mkopo.

Ushauri
(1). Pamoja na IMF kuridhia maboresho ya mashariti ya mkopo Ni vema serikali,ikatimiza madhumuni ya mkopo,kutokomeza covid-19,ili dunia ianze uzalishaji
(2). serikali Ni vema ikaajiri watumishi wa kutosha kwenye hivyo vituo vya afya na hospital, watakao toa huduma hizo, vinginevyo Ni kazi bure,kuna Upungufu wa madaktari na wauuguzi,na watalaam wengine,lakini wataalaam hao wako madaktari wote watakao maliza intern waajiriwe Mara moja,Kama ilivyo kuwa mwaka 1978, wakati wa vita ya Uganda, wanafunzi ambao walikuwa JKT kwenye mafunzo na mgambo walikwenda mstari wa mbele.
(3). Serikali iwalipe posho ya majanga (risk allowance) wafanyakazi wa sekta ya afya,wanao fanya kwenye kitengo Cha magonjwa ya milipuko.


(4).Tunatahadharisha,hayo majengo na mashiñe zisije kuwa mapambo, badala ya kufanya kazi iliyokusudiwa.
 
Unahaki ya kuwa na maoni hayo ila ni vyema kufahamu kwamba maamuzi ya serikali mara nyingi hufanywa baada ya mchakato mrefu unaohushisha watu wengi. Siamini kwamba kila kitu kinafanywa kiurahisi kama mtoa mada alivyo eleza
 
S Samahani mkuu hivi za madarasa sio zile za matozo Tena??? Eeeh eeeh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…