kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema anatambua kundi la vijana waliojiajiri kupitia bodaboda na yuko tayari kwenda nao mpaka 2025. Rais Samia Suluhu alizungumza hayo aliposimama kuzungumza na wakazi wa Usa River wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Vijana hao wa Bodaboda walionyesha kumuunga mkono Rais Samia na kusindikiza Msafara wake kuelekea Usa River kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri.
Aidha madereva bodaboda wamesisitiza kazi yao sio ya laana lakini pia wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuwapa mikopo inayowawezesha kuwekeza kwenye shughuli nyingine kama kilimo na biashara.