Rais Samia: CCM inawachama milioni 13 yoyote anayefikiria kukipasua chama hiki ajifikirie mara mbili mbili

Kwanini hataki na hawataki mabadiliko ya kweli kwenye katiba mpaka kwenye tume huru ya uchaguzi aone cha moto.
 
Hayo yote hayana shida. CCM ina wanachama wengi na ina uhakika wa kushinda, kwa nini mnaogopa reforms? Kwa nini mnaogopa uchaguzi huru na haki? Kama kweli mnakubalika na mna wapiga kura wengi, mtashinda tu
 
Kila kijiji na kila mtaa Tanzania nzima kuna ofisi ya CCM. Nenda kaulize ofisini kwao au kwa mjumbe yeyote wa nyumba kumi atakuambia
Sasa million 13 uoga unatoka wapi wa kuweka tume huru isiyochaguliwa na Rais au 13 ni wa kupika?
 
kingekuwa na wanachama wote hao tume ya uchaguzi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa isingejaza makada wake tupu na kwanini inaogopa uchaguzi huru na inamamilioni ya wanachama mbona wanajidanganya wenyewe sasa
 
sasa kwanini mnaogopa uchaguzi huru na wa haki wakati mna kura 13M za uhakika?
 
Kila kijiji na kila mtaa Tanzania nzima kuna ofisi ya CCM. Nenda kaulize ofisini kwao au kwa mjumbe yeyote wa nyumba kumi atakuambia
Sasa kwa nini mnaogopa uchaguzi wa uhuru na haki,na kalibu kila uchaguzi lazima mreta fingusi za kuiba kura
 
Tatizo sio kupasua, hamna mwenye mpango huo. Swali hapa je kwanini kinapgopa mabadiliko?
 
Kama ni wanachama zero brain sawa...ila wale wanaojielewa sidhan kama wanafika hata 20🤣🤣
 

..akawaombe msamaha GenZ wa Kenya.

..Watanzania tumechoka mitandao kufungiwa wakati ugomvi hatukuuanzisha sisi.
 
Sahihi kbs, sasa mbona ccm yenye mamilioni ya wanachama haitaki uchaguzi ulio huru & haki...inaogopa nn wakati uhakika wa kushinda wanao?!.

Ccm hamna akili kuanzia mwenyekigoda hadi chawa!
Sumu haionjwi my friend
 
Hao ni wasindikizaji, CCM inawenyewe
 
kuwa na kadi sio kwamba watu ni wanachama in the heart, bali hiyo kadi wengi wanayo kama kinga, ili pakitokea fursa iwe kama kilainishi cha kufanikisha mambo yako binafsi kutokana na hali halisi on the ground . Imagine,wengi wana hii notion kwamba ili upate ajira serikalini basi uwe cadre wa ccm sasa unatarajia nini ,ili ukodi chumba katika majengo ya chama basi uwe mwanachama wa CCM, ukikamatwa polisi alafu huna kadi ya chama ,hupati zamana au utapata mbilingi mbilingi, ukifaulu chuo bila kadi ya chama hupewi mkopo ,what are you expecting under this situation?
 
Sawa hatukatai,sasa wekeni tume huru kweli kweli tushuhudie mpambano halisi
 
Robo ya watanzania siyo? Hongereni
 
Kati ya hao mmewalazimisha wafanyakazi wa umma wote nchini wawe na kadi za CCM na wahakikishe wanazilipia - mnafikiri hatujui. Kwa mfano wafanyakazi wa halmashauri zote nchini ni lazima wawe wana CCM kama.unaipenda ajira yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…