Rais Samia: Dunia kwa sasa inakabiliwa na tatizo jipya la Usalama (Ugaidi)

Rais Samia amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na tatizo jipya la Usalama (Ugaidi). Ameeleza hayo katika Ufunguzi wa Kikao cha Mkuu wa Majeshi kinachofanyika Ngome ya Lugalo

Ameeleza, "Kwa hulka ya Ugaidi, Mtu yeyote bila kujali Rangi, Dini, Umri, Itikadi, Kipato au Uraia anaweza kuwa mhanga wa Ugaidi. Mifano ipo nanyi mnaijua"

Rais ameongeza kuwa, "Mapambano dhidi ya tishio la Ugaidi si suala la Vyombo vya Ulinzi na Usalama peke yenu, bali linahitaji ushirikiano kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo Vyombo vya Habari na Asasi za Kiraia"

View attachment 2011253
.....atoaye pumzi amemsikia, na anajua ujumbe wake ulimaanisha nini
 
===
Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kikao cha Mkuu wa Majeshi CDF, Chief of defence Forces General Venance Mabayo na makamanda wengine wa vikosi mbalimbali vya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam,

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amevalia Sara za Jeshi la JWTZ kama amiri Jeshi mkuu wa majeshi yote Tanzania alionekana kuvutia na kushawishi wengi hasa kutokana na ujasiri na ukakamavu wake aliouonesha kabla,wakati na baada ya kikao kile kwani alifanya kikao kingine Ikulu Jijini Dar es salaam na mwakilishi wa Bank ya dunia ( WB )

Rais Samia Suluhu Hassan amewashukuru na kuwapongeza askari wote wa majeshi yote kwa namna wanavyoendelea kuitunza na kuilinda amani ya Taifa letu la Tanzania kwa ustadi na umahiri mkubwa huku wakitanguliza wivu na Uzalendo kwa Taifa,

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza lazima amani ya Taifa letu ilindwe kwa "gharama yeyote" kwani amani ndio msingi wa maendeleo yote ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisayansi,hakuna amani hakuna maendeleo hakuna Taifa,

Rais Samia Suluhu amesema hakuna mwekezaji yoyote awe wa nje au wandani anaweza kuwekeza mtaji wake mahali pasipokuwa na "amani " kwani amani ndio kigezo namba moja cha kukuza uwekezaji katika nchi yoyote ile hapa Duniani,Hakika hakuna kama Samia,
 
Attachments

  • VID-20211115-WA0058.mp4
    23.6 MB
===
Amiri Jeshi mkuu na mkuu wa majeshi yote bara na Visiwani Mhe Samia Suluhu Hassan,

IMG-20211115-WA0053.jpg

IMG-20211115-WA0051.jpg

IMG-20211115-WA0050.jpg

IMG-20211115-WA0049.jpg

IMG-20211115-WA0042.jpg
 
===
Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kikao cha Mkuu wa Majeshi CDF, Chief of defence Forces General Venance Mabayo na makamanda wengine wa vikosi mbalimbali vya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam,

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amevalia Sara za Jeshi la JWTZ kama amiri Jeshi mkuu wa majeshi yote Tanzania alionekana kuvutia na kushawishi wengi hasa kutokana na ujasiri na ukakamavu wake aliouonesha kabla,wakati na baada ya kikao kile kwani alifanya kikao kingine Ikulu Jijini Dar es salaam na mwakilishi wa Bank ya dunia ( WB )

Rais Samia Suluhu Hassan amewashukuru na kuwapongeza askari wote wa majeshi yote kwa namna wanavyoendelea kuitunza na kuilinda amani ya Taifa letu la Tanzania kwa ustadi na umahiri mkubwa huku wakitanguliza wivu na Uzalendo kwa Taifa,

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza lazima amani ya Taifa letu ilindwe kwa "gharama yeyote" kwani amani ndio msingi wa maendeleo yote ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisayansi,hakuna amani hakuna maendeleo hakuna Taifa,

Rais Samia Suluhu amesema hakuna mwekezaji yoyote awe wa nje au wandani anaweza kuwekeza mtaji wake mahali pasipokuwa na "amani " kwani amani ndio kigezo namba moja cha kukuza uwekezaji katika nchi yoyote ile hapa Duniani,Hakika hakuna kama Samia,
Picha ya Rungwe imeingiaje hapo?
 
Rais Samia amepozi kama vile ni askari mzoefu jeshini
 
Akili za Viongozi wa Tanzania, ukiwasikia "tutailinda amani kwa gharama yoyote ile" basi wanamaanisha "dhidi ya wapinzani" na wala sio dhidi ya maadui kutoka nje!!
 
Kwani Wapinzani ndio mnataka kuivuruga amani yetu?
 
Kauli kama hizi kuna watu hawapendi kuzisikia, hongera sana mama amani yetu ndio kila kitu.
 
Kwa hiyo Samia alikwenda Ngome jana kutangaza kwamba anawapeleka vijana vitani dhidi ya ugaidi.
Na sisi tunadhani she was just basking in military uniform.
"Nia tunayo,uwezo tunao,sababu tunayo," speech .
 
Back
Top Bottom