Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Ni sawa tu..kupanga bajeti Ni kuonesha umuhimu....kutumia kwa.shughili maalum Ni kutoa zwadi ka Umma badala yankuzila
 
Lilia Katiba mpya utapata na bando la muungano ndani yake
 
Hapa ndipo anapofeli na wajanja wamepata nafasi ya kupiga, SSH kusema kweli atapata taabu sana naona wapigaji wakiongezeka kwa speed ya Jobo

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
TRA haihusiki kabisa kule Zanzibar.

Zanzibar wanna taasisi yao ya kukusanya mapato
... futeni hilo neno Tanzania kwenye kirefu cha TRA tujue moja kwamba ni ya Tanganyika pekee. Huu muungano ni kizungumkuti sana.
 
Haya mambo ya kubadili matumizi kwa kidinguzio cha kubana matumizi ni jambo la kushangaza sana.
Bajeti ya sherehe za Muungano imepitishwa mwaka huu wa fedha na sasa rais anataka atuaminishe kuwa ndo amejua kuwa hazikustahili kutengwa!!!
Na je mwakani watatenga tena au ndo sherehe zisahaulike chini ya utawala wake???
Haya mabo ya kuona karibu ndo yana angamiza taifa letu na kulifanya kuwa na watu maskini wa kutupwa.
Hivi kweli ndani ya mwaka mmoja unabadirisja matumizi ya mambo muhimu kama sherehe ya Muungano na hata Uhuru atafuta!
Mpango wa 2025 je!!
Kazi bado ipo japo wanasema iendelee

landson Tz
 
Bado sielewi Zanzibar wapewe hizi pesa kwa utaratibu upi? Zilipatikana kwa utaratibu upi? Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi. Wanakusanya wanatumia kwao. Kwa nini kodi zetu nao wapewe?
 
Acha nao wafaidi kutawaliwa na mkoloni mweusi....acha jahazi lisonge
 
Ni kwa utaratibu ule ule ambao ulitumika kwa Chato. Mama SSH keshasema yeye na mwendazake ni kitu kimoja. Sasa umeshaonyeshwa mkia wa nyani ulipo sasa naniliu yake unataka kuitafutia wapi?
 
Pesa zigawanywe pande zote mbili kivipi sasa kwani kuna serikali ya Tanganyika pia?
 
Mama kaanza kuyumba. Sometimes Magufuli alikuwa sawa na ile style yake ya kutoa directions bila chenga.

Sasa hii ya Mama ya kusema eti hela zigawiwe sawa na kila upande ujue nini cha kufanyia ni udhaifu. Next year ni bora wasitenge pesa yoyote ili kuepuka mambo ya kipuuzi kama haya
 
Bado sielewi Zanzibar wapewe hizi pesa kwa utaratibu upi? Zilipatikana kwa utaratibu upi? Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi. Wanakusanya wanatumia kwao. Kwa nini kodi zetu nao wapewe?

Hakuna cha utaratibu ili mradi yeye ni rais na hizo pesa zinaenda Tanzania hiihii. Magufuli alikuwa anajichotea tu na kupeleka atakapo, na utetezi ilikuwa huko anakopeleka kwa upendeleo ni Tanzania pia. Hivyo mama aachwe apeleke chochote atakacho Zanzibar maana ni Tanzania pia.
 
Hii ni bajeti ya Mwaka 2020/2021 Ilishapitishwa kuwa kutakuwa na sherehe hizo. Mama kaamua kuondoa acha ujuaji
Kwanini hakushauri fedha hizi zisiwekwe kwenye hiyo budget mapema?

Yeye ofisi yake kipindi hicho (vice president) ndio walikuwa wahusika.

Anatafuta kiki tu kama alivyokuws akifanya Jiwe.

Maana Jiwe kuna bajeti nyingi tu katia sahihi then siku ya sikukuu anatangaza kuaghirisha sherehe then nyie wajinga mnamsifia
 
Kwa ufupi kila zama na mambo yake.... mwache aijenge zanzibar. Ni sebemu ya Tanzania 🇹🇿. Namsapoti asilimia 100%. Tuache unafki, mpenda kwao hutunzwa, waswahili walisema hivo.

Mbona tunasahau mapema sana ule usemi"Chato ni sehemu ya Tanzania" !?
 
Kwani tumeshindwa kuelewa kwamba kuna watanzania bara wanaishi visiwani Zanzibar na hizo hela za muungano zitawasaidia hata hao! Hapo hapo kuna wazanzibari wanaoishi bara, ni wafanyakazi, ni wafanyabiashara nao wanachangia katika kapu la TRA. Hii ni nchi moja, Zanzibar ni kama Chato au Tandahimba, period!
 
Pesa za sherehe za Muungano zipo kisheria na Bunge wamepitisha hiyo bajeti sielewi Rais anatumia sheria ipi kuzitumia tofauti na makusudio yake lini amerudi Bungeni kuomba kubadilisha matumizi hayo na CAG atakagua vp mahesabu hayo tunarudi kule kule kwa Mwendazake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…