Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Ila kama Serikali haina mpango wa kuadhimisha Sherehe za Muungano, kwanini wanatenga bajeti yake kila mwaka!?

Kwanini fedha hizo in a first place zisipangiwe shughuli za maendeleo badala ya kuja kuzibadilishia gia angani ilhali kuna vifungu vingi tu vya muhimu vinakosa bajeti katika wakati wa kupanga.
Ni sawa tu..kupanga bajeti Ni kuonesha umuhimu....kutumia kwa.shughili maalum Ni kutoa zwadi ka Umma badala yankuzila
 
Lilia Katiba mpya utapata na bando la muungano ndani yake
Hili litam - cost..

Viongozi wetu hawa hawajui kuwa Wa - Tanganyika tulio zaidi ya 55,000,000 ukilinganisha na Wazanzibari wasiozidi 2,000,000 hawaoni mantiki ya kuongozwa na Rais raia toka taifa jingine dogo kabisa...

Huu muungano HAPANA. Binafsi mimi huwa sielewi huu ni muungano wa aina gani. Ni muungano wa kulazimishana...

HAYA MAMBO SIYO KABISA. Si ajabu hili lika - speed upya na haraka HISIA ZA UBOVU/KASORO za muungano huu...

I predict kuwa, mambo haya yanayoonekana kuwa madogo dogo, tutambue kuwa, yanaweza ku - speed mwisho wake kabla ya 2025...

Ajifunze kwa marehemu Magufuli. He was selfish President, si msikivu, aliyejidhania ni mtakatifu kuliko Mungu, mwenye kiburi, aliyejiona ana akili kuliko watanzania wote..

Mwisho wake, akafa kifo cha ajabu na çha kusikitisha...

Samoa jifunze kwa tukio hili. Go and follow the right path. I see her, she is almost going through the same way...

Tatizo la viongozi wetu ni ugumu wao au pengine hawataki kusikiliza na pengine kupokea ushauri wa watu "wadogo" na "wapumbavu" kama sisi...
 
asiishia hapo tu, tunataka kujua hizo pesa zimefanya shughuli gani, kipindi cha jpm tumeona hosptali ya ya uhuru dodoma, barabara za morocco- mwenge etc. samia amefeli kusema zikafanye shughuli zingine. ingekuwa jjpm angeshazialocate kabisa hizo hela zikafanye nini.
Hapa ndipo anapofeli na wajanja wamepata nafasi ya kupiga, SSH kusema kweli atapata taabu sana naona wapigaji wakiongezeka kwa speed ya Jobo

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
TRA haihusiki kabisa kule Zanzibar.

Zanzibar wanna taasisi yao ya kukusanya mapato
... futeni hilo neno Tanzania kwenye kirefu cha TRA tujue moja kwamba ni ya Tanganyika pekee. Huu muungano ni kizungumkuti sana.
 
Haya mambo ya kubadili matumizi kwa kidinguzio cha kubana matumizi ni jambo la kushangaza sana.
Bajeti ya sherehe za Muungano imepitishwa mwaka huu wa fedha na sasa rais anataka atuaminishe kuwa ndo amejua kuwa hazikustahili kutengwa!!!
Na je mwakani watatenga tena au ndo sherehe zisahaulike chini ya utawala wake???
Haya mabo ya kuona karibu ndo yana angamiza taifa letu na kulifanya kuwa na watu maskini wa kutupwa.
Hivi kweli ndani ya mwaka mmoja unabadirisja matumizi ya mambo muhimu kama sherehe ya Muungano na hata Uhuru atafuta!
Mpango wa 2025 je!!
Kazi bado ipo japo wanasema iendelee

landson Tz
 
Bado sielewi Zanzibar wapewe hizi pesa kwa utaratibu upi? Zilipatikana kwa utaratibu upi? Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi. Wanakusanya wanatumia kwao. Kwa nini kodi zetu nao wapewe?
 
Acha nao wafaidi kutawaliwa na mkoloni mweusi....acha jahazi lisonge
 
Labda niulize kuwa pesa za gharama za Muungano huwa zinatoka wapi au kwa utaratibu gani.

Pili je Zanzibar kuna pesa ambayo wanachangia kwenye Muungano kusema sasa warudishiwe sehemu?

Kinyume na hapo Tanganyika haipaswi iendelee kuifadhili Zanzibar. Otherwise tuambiwe kuwa nao Zanzibar kuna pesa huwa wanachangia huku kwetu.

Mh Rais asitake sasa kuwa nyonya wabara kwa jasho lao kupafaidisha kwao. Haya ndo madhara ya kuwa na Rais kutoka Zanzibar. Kama kuna sehemu anaona Zanzibar wananyonywa aseme wazi na hiyo mianya izibwe.

Lakini siyo sisi huku tupigike halafu jamaa wawe wanakula tende na urojo tu mwisho wa siku wapate pesa zetu.
Ni kwa utaratibu ule ule ambao ulitumika kwa Chato. Mama SSH keshasema yeye na mwendazake ni kitu kimoja. Sasa umeshaonyeshwa mkia wa nyani ulipo sasa naniliu yake unataka kuitafutia wapi?
 
Labda niulize kuwa pesa za gharama za Muungano huwa zinatoka wapi au kwa utaratibu gani.

Pili je Zanzibar kuna pesa ambayo wanachangia kwenye Muungano kusema sasa warudishiwe sehemu?

Kinyume na hapo Tanganyika haipaswi iendelee kuifadhili Zanzibar. Otherwise tuambiwe kuwa nao Zanzibar kuna pesa huwa wanachangia huku kwetu.

Mh Rais asitake sasa kuwa nyonya wabara kwa jasho lao kupafaidisha kwao. Haya ndo madhara ya kuwa na Rais kutoka Zanzibar. Kama kuna sehemu anaona Zanzibar wananyonywa aseme wazi na hiyo mianya izibwe.

Lakini siyo sisi huku tupigike halafu jamaa wawe wanakula tende na urojo tu mwisho wa siku wapate Kwa
Pesa zigawanywe pande zote mbili kivipi sasa kwani kuna serikali ya Tanganyika pia?
 
Mama kaanza kuyumba. Sometimes Magufuli alikuwa sawa na ile style yake ya kutoa directions bila chenga.

Sasa hii ya Mama ya kusema eti hela zigawiwe sawa na kila upande ujue nini cha kufanyia ni udhaifu. Next year ni bora wasitenge pesa yoyote ili kuepuka mambo ya kipuuzi kama haya
 
Bado sielewi Zanzibar wapewe hizi pesa kwa utaratibu upi? Zilipatikana kwa utaratibu upi? Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi. Wanakusanya wanatumia kwao. Kwa nini kodi zetu nao wapewe?

Hakuna cha utaratibu ili mradi yeye ni rais na hizo pesa zinaenda Tanzania hiihii. Magufuli alikuwa anajichotea tu na kupeleka atakapo, na utetezi ilikuwa huko anakopeleka kwa upendeleo ni Tanzania pia. Hivyo mama aachwe apeleke chochote atakacho Zanzibar maana ni Tanzania pia.
 
Hii ni bajeti ya Mwaka 2020/2021 Ilishapitishwa kuwa kutakuwa na sherehe hizo. Mama kaamua kuondoa acha ujuaji
Kwanini hakushauri fedha hizi zisiwekwe kwenye hiyo budget mapema?

Yeye ofisi yake kipindi hicho (vice president) ndio walikuwa wahusika.

Anatafuta kiki tu kama alivyokuws akifanya Jiwe.

Maana Jiwe kuna bajeti nyingi tu katia sahihi then siku ya sikukuu anatangaza kuaghirisha sherehe then nyie wajinga mnamsifia
 
Kwa ufupi kila zama na mambo yake.... mwache aijenge zanzibar. Ni sebemu ya Tanzania 🇹🇿. Namsapoti asilimia 100%. Tuache unafki, mpenda kwao hutunzwa, waswahili walisema hivo.

Mbona tunasahau mapema sana ule usemi"Chato ni sehemu ya Tanzania" !?
 
Kwani tumeshindwa kuelewa kwamba kuna watanzania bara wanaishi visiwani Zanzibar na hizo hela za muungano zitawasaidia hata hao! Hapo hapo kuna wazanzibari wanaoishi bara, ni wafanyakazi, ni wafanyabiashara nao wanachangia katika kapu la TRA. Hii ni nchi moja, Zanzibar ni kama Chato au Tandahimba, period!
 
Dodoma!

Akizungumza Leo katika kongamano la Muungano jijini Dodoma, Makamu wa Raisi Dr . Philip Mpango amesema Raisi Samia Suluhu Hassan ameelekeza Fedha zilizotakiwa kutumika katika shughuli za maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zigawanywe pande hizo mbili (Tanganyika na Zanzibar) ili zikafanye shughuli za maendeleo!...
Pesa za sherehe za Muungano zipo kisheria na Bunge wamepitisha hiyo bajeti sielewi Rais anatumia sheria ipi kuzitumia tofauti na makusudio yake lini amerudi Bungeni kuomba kubadilisha matumizi hayo na CAG atakagua vp mahesabu hayo tunarudi kule kule kwa Mwendazake
 
Back
Top Bottom