Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumzia mauaji yaliyotokea Mtwara ambapo maafisa wa Jeshi la Polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara Mussa Hamisi ambapo Jeshi limeunda kamati kuchunguza tukio hilo.
Rais amesema haiwezekani Jeshi kutuhumiwa kisha liunde kamati ya kujichunguza lenyewe, hivyo amesema amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aunde kamati nyingine kuchunguza tukio hilo.
Amesema taarifa ya kamati ya polisi inayochunguza tukio hilo, italinganisha na taarifa ya kamati huru itakayoundwa na Waziri Mkuu.
Ameyasema hayo akiwa njiani akielekea Mwanza.
=======
Pia soma:
Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (25/01/2022)
Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022 (26/01/2022)
Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi (25/01/2022)
Iundwe Tume Huru kuchunguza suala la Hamza kuua Polisi
Ukifuatila kwa ukaribu suala la mauji alofanya Hamza kisha nae kuuwawa unabaki na maswali mengi kuliko majibu. Nmesoma gazeti la mwananchi tangu kutokea kwa tukio hili kuna vitu vingi ni ambiguous, kwa mfano majirani zake wote waliohojiwa wanasema jamaa alikua mstaraabu na mpole ukienda chunya...