Rais Samia hajaonekana kwenye Sherehe za Mei Mosi, yuko wapi?

Ficha upumbavu wako.Yaani hivyo viwanda viwili vinaacha uzalishaji siku ya Mei 1 ili kuhudhuria uwanjani?
Miaka yote walikuwa wanakuja "kujaza" uwanja.
Njoo na sababu nyingine.Tunaoishi Arusha tunajua hamasa ilikuwa kubwa Mei Mosi na sababu kubwa ni uhamasishaji uliofanywa na Makonda.
 
Naunga mkono hoja,alijua itakuwa kama ya sherehe za Uhuru,afukuze kazi washauri wake
 
Vipi KIKOKOTOO
 
Nauona mzigo mkubwa wa maswali magumu kutoka kwa mtu mwenye kujenga hoja na maarufu sana nchini, bwana Tundu lissu, watu wa mjini Kimara huku tunadiriki kumwita Toto tundu kuwaelemea kina Nape na vijana wa CCM

Kwa wanaomfahamu vizuri Mh Lissu, naamini watakubaliana nami kwamba, kosa lililofanywa na washauri wa mh Rais, ni kosa la kiufundi

Kukosa huko kwenye kujumuika na wafanyakazi nchini kuzungumza nao hata kama ni kwa ahadi, kunampa turufu kubwa mh Lissu kuichachafya tena CCM

Yetu macho!
 
Habarini Wadau,

Leo tarehe 1/5 ni siku ya maadhimisho ya sherehe za Wafanyakazi maarufu kama Mei Mosi. Kitaifa Sherehe hizi zimefanyikia Jijini Arusha

Katika Maadhimisho haya Rais wa Nchi (Samia Suluhu Hassan) ambaye kimsingi alikuwa na taarifa zote na maandalizi ya kutosha na hata alishatengenezewa ratiba ya kuhudhuria

Lasivyo angetoa hudhuru, lakini hajafanya hivyo, kwakuwa hajafanya hivyo na anajua alipaswa kufanya hivyo maana yake ni kwamba amefanya makusudi

Aidha, alijua hana la kuwaahidi Wafanyakazi au ameona hata asipohudhuria hakuna umuhimu

Watanzania Wafanyakazi wa nchi hii wanazidi kumuona Mama kuwa Msanii na Mwenye ahadi za uongo zisizotekelezeka

Kwanini Hakufika?
Kwanini Hakuomba udhuru?
 
Rais akuombe ushuru wewe kama nani? Boss wako ofisini Huwa anakuomba ushuru anapotoka?
 
Siku ya meimosi hajaipa umuhimu. Ratiba ya raisi inapangwa muda mrefu sana.
Ndio siku pekee watumishi wanaomsaidia kazi wanataka wamsikilize
 
Nawaza tu, 🤔 sherehe za mei mosi kama zingepangwa kufanyika kitaifa Honolulu mwendo wa masaa 10+ angani .... Mgeni rasmi angeacha kwenda? 💬
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…