Rais Samia: Hakuna atakayeuza Tanzania. Sitaki Shida nataka Watanzania Waishi Maisha mazuri

KWA Nini unaumiza Watanzania wenzako.?Utajibu Nini mbele za Mungu?
 
Huyu MAMA akili kisoda hizi R ameshindwa kusimamia Hata hiyo moja kwa mfano ili watu waige kutoka kwake badala yake anawapa watu wakasimamie kwa ajili yake yeye anaingia ndani kupakaa hina ,kweli
 
Yaani umewafanya watu mateka, wamechukuliwa utumwani kwenye kuta za gereza kwa sababu ya wajomba zako, kwa mkataba wa kimanguno, ili wapate rasilimali za watanganyika, ukaiacha zanzibari ikiwa huru na rasilimali zao sababu wewe watokea huko, umeshirikiana na wazanzibari wenzako kwenye uuzaji wa bandari zetu, leo unasema hutaki kunyanyasa watu, wakati ndugu zetu wanalala polisi pasipo stahiki zozote, kisa wamehoji mkataba mbovu wamekuwa wahaini,

ujinga mtupu, tutakusikiliza baadae
 
Hizo R nne ndio zipi?
 
Anajua kilichomo kwenye IGA, au anajisemea tu mambo kama kawaida yake bila kuelewa anachozungumzia?

Lazima wananchi wakusute, kwa sababu huna unalolijua.

Unafanya maksudi mazima kupitisha kiujanjaujanja IGA Bungeni, halafu sasa unakuja hapa na kutoa vistori?

Tokea mwanzo wa mchakato wa haya mambo ya bandari, alama zote zinaonyesha uhusika wako katika kuhujumu nchi. Umeweka watu wako kila mahali wasukume jambo hilo la Bandari bila pingamizi, sasa unakuja na visababu huwezi kuuza Tanzania?

Kama wewe huwezi kuuza Tanzania ni nani mwingine mwenye uwezo kama huo, kwa maana umejipambanua waziwazi kwamba huna uchungu kabisa na mambo ya nchi hii.

Hakuna kiongozi yeyote, aliyewahi kuwa katika nafasi hiyo uliyopo sasa, ambaye alikosa huruma na nchi hii na watu wake kama ulivyo wewe.
Hata wakoloni kidogo walijali koloni walilolikalia kuliko unavyoonyesha wewe.

Maslahi yako yako kwingine kabisa.
 
Speech ya mtu wa kawaida kabisa.
 
Hii ndio speech ya mkuu wa nchi kweli?
 
Mtu hawezi jibu kitu ambacho haelewi
 
Mkuu wa nchi hana tofauti ya wewe na mimi mradi afuate katiba ya nchi
Mkuu wa nchi hawezi kulingana na mimi wala wewe.
Speech yake inaandaliwa na jopo la wasomi wazuri kadhaa na inafanyiwa mapitio.

Kauli ya rais ni kauli ya nchi, sio mipasho mipasho kama ya Kopa anayejitungia ashki zikimshika
 
Haiauzwa imegawiwa bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…