Rais Samia, hii kauli ya kuwaruhusu Mawaziri wajipimie, wasivimbiwe itolee ufafanuzi tena

Walewale wa kujipimia hakuna cha kiunguja nani hajui kuvimbiwa..? Nani hajui kujipimia..?
 
... ile ilikuwa kauli ya ovyo kabisa kuwahi kutolewa na kiongozi kwa anaowaongoza! Ufisadi unatakiwa ukemewe kwa nguvu zote popote na yeyote; sio kuurembaremba kwa maneno ya ajabu ajabu sijui mle kwa urefu wa kamba zenu; mara msivimbiwe! Dah!

Anyway, the former CCM Secretary General aliwahi kunukuliwa live akisema, "Neno ufisadi halipo kwenye kamusi ya CCM", na hadi leo kauli ile haijawahi kukanushwa na yeyote!
 
Walewale wa kujipimia hakuna cha kiunguja nani hajui kuvimbiwa..? Nani hajui kujipimia..?
Ndugu zangu kiswahili cha ZNZ na huku kwetu ni tofauti kabisa.

Tuendelee jifunza hizi 'regional dialects'. Mama atakuwa Mwalimu mzuri sana.
 
duh! kikulacho ki nguoni mwako.
 
alafu supika anaweza kuchukua mzee vijisenti msomi harvard...
tutafika mbinguni tumechoka sana.
 
alafu supika anaweza kuchukua mzee vijisenti msomi harvard...
tutafika mbinguni tumechoka sana.
Nakumbuka jinsi alivyokuwa anatetea ile takrima wakati wa uchaguzi kwenye jumba la sheria....Mungu mwenyewe aingilie kati
 
Hakuna ambacho hakijaeleweka hapo.

Kwenye hii video ndefu anasimulia jinsi miradi inavyokwama kukamilika kwa sababu ya upigaji na ametolea mfano wa mradi wa meli.

Anasema kabisa kuwa miradi inakuwa compromised(kukwama) kwa sababu ya watu kupiga sana na akaiita hii hali kuwa ni watu kula hadi kuvimbiwa na anaomba watu wapige kwa kiasi(wajipimie).

Sasa hapo ni kitu gani hujaelewa?!Wewe kinachokusibu ni kwamba huamini anachosema Samia lakini huo ndiyo msimamo wa Samia na Serikali yake.
Your browser is not able to display this video.
 
Na alipostaafu alikabidhiwa V8 mpya kabisa
 
Pale Taifa linapokuwa fucked up!🤡🤡🤡

Imagine hapo mawaziri wana-take notice kabisa kumbe wanaandika mambo ya kipumbavu ya 'kujipimia' katika diary zao🤡🤡🤡
Your browser is not able to display this video.
 
Hii kauli ni kati ya kauli ya hovyo iliyotolewa bila tafakuri ya kina. Huo ulaji ni wizi, ufisadi na uchafu wa kila namna unaohamasishwa kwa mgongo wa vyeo. Aliyetoa hii kauli yapaswa atoke hadharani na aitengue.
 
Mtunga-sheria ndiye mwenye haki ya kuitafsiri sheria husika. Au siyo?
 
Huyo mama yenu yupo yupo tu hapo ofisini na nimegundua hakuna kitu kinamtatiza kama namba.
 

Mkisikia ^kula^ tu mnajua ni ufisadi? Najua fika kwamba utawala huu ni ponga katika suala la matumizi ya mali za umma na udhibiti wa pesa, kuliko ile ya JPM, lakini hapa Bi Mikopo anamaanisha matumizi ya mamlaka. Watendaji wake wasiingiliane na kugombana katika kutekeleza majukumu ya ^sirikali.^

Don't be so closed-minded. Anyweiz, politics inatendensi ya kukapitolaizi kwenye mambo tata na seemingly negative.
 
Huduma za jamii zitakuwa shida kupata kwa Sasa dhuruma kwa wanyonge itakuwa kubwa sana. Ukienda ofisini lazima utowe kianzio la sivyo hupati huduma, eg hospital office za serikali etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…