Rais Samia, hii kauli ya kuwaruhusu Mawaziri wajipimie, wasivimbiwe itolee ufafanuzi tena

Rais Samia, hii kauli ya kuwaruhusu Mawaziri wajipimie, wasivimbiwe itolee ufafanuzi tena

Serikali inaongozwa na MWANADAMU na si MUNGU......


Mwanadamu huyo anawakumbusha WATENDAJI KUSIMAMIA VIAPO VYAO vifuatavyo........

1)Kutoingiliana katika majukumu ya mipaka ya kazi zao....kazi yoyote ina maslahi binafsi na Yale makuu zaidi(kutoa huduma kwa jamii)

2)Kutochafuana ,kubagazana na kufitiniana kwa kiongozi mkuu(kwenda kusema kwa mama)

Mh.SSH amefafanua vyema tu ila baadhi yetu tumeamua kufanya UPOTOSHAJI WA MAKUSUDI.....

#Siempre JMT🙏
Hivi unakumbuka Kikwete au mwinyi Kama sikosei aliwahi kulisema neno Hilo,na unajua Nini kilitokea baada ya hapo? Mh subiri matokeo ya hiyo kauli utaniambia.
 
Ndio maana mzunguko huwa ni uleule ili waendelee kutafuna! Hii nchi hovyo kabisa!
Wanasiasa hawapo kwa ajili ya maslahi ya wananchi bali wapo kwa maslahi ya kwao binafsi, mama namuelewa sana anajaribu kutuweka wazi ili tuelewe tabia za watawala wa kisiasa walivyo akiwamo na yeye maana kajiwekea wigo wa upigaji kwa kurudisha wezi madarakani.
 
Inasikitisha sana!
Means hakuna anayeweza kufanya lolote...What kind of mentality is this? Dola ina levya watu hivi?
Wana polisi, wana jeshi, usalama wa taifa. Huwezi kuiondoa CCM kwa kura za uchaguzi. Ingekuwa kura zinaondoa CCM ingekuwa chama pinzani miaka mingi
 
Rais Samia, jana akiongea na mawaziri aliwaambia wajipimie ila wasivimbiwe tena mbele ya TV ya umma. Nilipigwa na butwaa ila nikahisi mambo yafuatayo.

1. Rais hajui kwamba mali anazowaambia mawaziri wajipimie ni za wananchi wanao msikiliza na kwamba wananchi wanataka alinde mali zetu kama kiapo kinavyomtaka?

2. Rais anajua hawezi shitakiwa hata kama atafanya lolote; hivyo kalewa madaraka.

Ushauri kwa rais; Hii kauli itolee ufafanuzi, huku mtaani kishanuka mno.

Hata hivyo mawaziri wapiga deal wanajulikana.

VEDIO HII HAPA
Mimi naona Mh.Raisi yuko sahihi.
Kosa ni kuitoa hii kauli kwa Wananch.
Ikulu wajitokeze haraka kusafisha hali ya hewa.
 
Je unadhani Watanzania wote ni la Saba C???
Miaka 60 hakuna maji wala umeme, huduma za afya ni kwa msaada wa wafadhili, barabara tumejengewa kwa msaada au mikopo, niliwahi sikia hata nyumba kuu pale Dom ni kwa msaada wa mchina.
Hata uwe na proposal nzuri kiasi gani au hata aje nayo mmarekani; bila ya 10% hakuna kigogo anayetia sahihi.
Kuna mtu aliwahi sema kuwa CCM ni sawa na ukoo wa panya.
Mama ametukumbusha ukweli kuwa ukiona mradi unasusua jua w
akubwa wajipimia zote.
 
Lilikuwa ni onyo la tabia za kifisadi zilizoshamiri tangu 2010 to 2020 ambazo hazijawahi kuachwa. 2015 to 2020 hazikuzungumzwa tu ila zilikuwepo za kibabe.

Hata hivyo ametoa onyo very weak, ukisha amua kuweka udhaifu wa mtendaji wazi ni umemshtaki kwa jamii basi unatakiwa umuwajibishe, kinyume na hapo muite faragha muonye. Sasa hapa tunajua kuwa kuna mawaziri walafi ila wanatakiwa wajipime wenyewe.

Tunahitaji mpango mkakati bora wa kudhibiti utendaji wa serikali.
Tena wale jamaa wa msoga kawapa wizara zenye kamba refu. Bure sana huyu mama. Utakaaje na mawaziri wamevimbiwa kwa upigaji. Kiapo cha urais sio mzaha. Haiwezekani kuendesha nchi kimzahamzaha.
 
Back
Top Bottom