Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Toka kipindi kile alishauriwa awe anaweka namba ya simu kwenye nyuzi zake za kichwa jamaa alikazana sana na baadaye zilipotoka teuzi ni kama alikatishwa tamaa.

Leo Rais kasema huwa anapita pita humu mimi nlishaona ID flani na nliambiwa niiangalie kwa utulivu. So sasa nadhani dogo atapambana sana naye atoke juani maana anapambana sana humu kuchawia halafu vyeo wanapata wengine ambao hata hawamo humu.
 
Ni ushauri aliotoa Kikwete kwa Kagame ukataka kuwaka moto
 
Mama Samia anaijuwa Jamii Forums kabla haijawa Jamii Forums.
 
Ni lazima TISS wawe na jicho huku kama kweli wapo serious..

JF ni chombo muhimu.
 
Yupo mitandao yote ya kijamii kuanzia Facebook, Instagram, Twitter nakadhalika.

Kwahiyo kama ni kuwaheshimisha basi amewaheshimisha hadi watumiaji wa Facebook nakadhalika.
Mtu akiwa JF kuna namna fulani huwa namheshimu..tofauti na Facebook na Twitter.

Mama kusema anapita humu Jf ni kitu poa sana.
 
Mama with all due respect tukumbuke sisi watoto wako na ajira, tuko mtaani toka 2015 tuna majukumu, mpaka tunakufuru
 
Kumbe hua ana comment, ana like, ana bishana na kukosoa kwenye ule uzi wa kimashihara.

Inabidi nianze kwenda PM randomly naweza kuangukia popote. mara pa Ultimate magogoni
Tokea mama awe rais hivi ushawahi kuona Faiza fox kucomments??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…