#COVID19 Rais Samia: Ilikuwa ni vigumu kwangu kufanya kazi na Hayati Magufuli hasa alivyokuwa anakabiliana na suala la Covid -19

Amejibu vizuri ....yeye ndio alikuwa anaujua ukweli kuwa magufuli alikuwaje kiutendaji.

Yawezekana hata hilo jibu angeweza kulitoa hapa nchini, tatizo waandishi wa habari wa hapa nchini wakialikwa ikulu na kupewa nafasi ya kuuliza swali hawahoji maswali fikirishi.


Kazi kubwa ya waandishi wetu na vyombo vya habari ni kusifia wakubwa.
 
Rais Samia amewambia wamarekani kuwa ilikuwa ni vigumu kwake kufanya kazi na Magufuli.

Na alikuwa ana tofautiana nae sana kwenye mambo mengi hasa jinsi alivyokuwa ana kabiliana na swala la UVIKO-19.

View attachment 2188625
Kwa nini hakuachia ngazi? Makamu wa Rais ndiye mshauri mkuu wa Rais. Unaonekana kwenye video ukisifia juhudi kumbe rohoni una yako. Huo ni unafiki usiokubalika.
 
Anachosahau ni kwamba, yeye atanangwa akiwa hai baada kumaliza muda wake.
Karma is real...

Naomba uzima niione hii siku, natamani Rais atakaeingia atoe general amnesty ya walau mwaka mmoja kwa raia yeyote atakaemsema huyu mama asishtakiwe kokote.
 
Mtangulizi wake mwenyewe kwa nyakati tofauti aliwahi kukiri ni kichaa hata baadhi ya watu waliomfahamu kwa karibu kuanzia TANROADS
View attachment 2188891

walishangaa kuona jamaa wamempa ofisi kubwa kama ile.


“You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness. In this case, it comes from nonconformity, the courage to turn your back on the old formulas, the courage to invent the future. Besides, it took the madmen of yesterday for us to be able to act with extreme clarity today”- Thomas Sankara

JPM is one of those madmen and history will surely absolve his presidency.
 
Rais Samia amewambia wamarekani kuwa ilikuwa ni vigumu kwake kufanya kazi na Magufuli.

Na alikuwa ana tofautiana nae sana kwenye mambo mengi hasa jinsi alivyokuwa ana kabiliana na swala la UVIKO-19.

View attachment 2188625
huyu mama dishi limeyumba! Hajielewi! Hajitambui! Anajipendekeza kwa mabeberu ili apate nini? Kaporomosha uchumi na kurudi umasikini! Ombaomba! Mtangulizi wake kapambana na kupewa bigup jinsi alivyohandle covid ndani na nje! Sasa anaongea nini?
 
Tunatakiwa kutunza kumbukumbu ya kila kauli ya kipuuzi anayotoa huyu mama na Mungu amjalie uzima siku moja akishaondoka azitolee maelezo zote.
 
Kwenye Jambo la Uviko 19 nakubaliana kabisaa na Rais Samia.

Hayati JPM alikosea jinsi ya kukabiliana/kupambana na Janga hili tangia mwanzo.....hakuna cha kuficha kwenye hili.
Hata Kanisa lilitofautiana naye Jinsi Hayati JPM alivyo shughulikia Janga la Uviko19.

Covid19 ilikuwa ni janga la Dunia lkn Hayati alilichukulia kinyume kabisa na kuifanya TZ kama kisiwa na hivyo kuzua mgogoro na mataifa mengine kutokana na msimamo wake.

Pongezi kwa Rais Samia Jinsi alivyo lishughulikia janga la Covid19 mara tu alipo chukua Nchi.

Kila mwenye macho na akikili aliona.
 
Umeandika ujinga.Huyo Mungu alikua tanzania tu.Corona haikua tishio kivile kama nchi za ulaya kwahiyo kutokua na vifo vingi sio kwasababu hakukua na lockdown au tulimwomba sana Mungu.Na ziko nchi nyingi tu za afrika nao hawakuathirika sana na covid.Tumia kichwa chako kufikiri sio kukaririshwa.
 
Kuna unafiki sana kwenye siasa, ahsante kwa kuliona hili maana hata mie nilitaka kuandika kuhusu uvaaji wa barakoa maana mtu unakuwa mnafiki mpaka kwenye afya yako yaani unaogopa ugonjwa alafu huvai barakoa kisa utaonekana upo kinyume na maonoya Rais.

Mwingine aliekuwa anavaa barakoa alikuwa Rais Mstaafu wa Zanzibar Karume
 
Ila mpagani bado anaishi
 
This is not presidential at all. Mama anapaswa kufanya yake tu sasa bila kumtajataja marehemu

Collective responsibility holds. Otherwise angeachia ngazi those days
Huyu mwanamke hafai kuwa Rais, hakutakiwa kwenda kinyume na kiapo chake.
Aliapa hatatoa Siri za Yale atakayoyajua kwenye utumishi wake. Sasa amekuwa kama lissu tuu anabwatuka hovyo.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kwani kafanyaje? Kusema walitofautiana mawazo na Mwendazake au? Kwamba hili ni kosa au?

VP sio mtu mdogo,Tzn ina umuhimu gani hadi Biden iwe lazima kuongea na Rais?
Kwani North Korea 🇰🇵 inaumuhimu gani mpaka wa mfate Singapore 🇸🇬
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…