Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Rais Samia: Inashangaza kifo cha Kibao kimeibua wimbi kubwa, hii sio sawa, kifo ni kifo

Wanaoua watu makusudi ili kumwondoa huyu mama,tafadhali waache....mama atamaliza wakati wake ataondoka .....msiue watu wasio na hatia jaman...siyo vizuri kiukweli
 
Hi kauli kuwa kifo ni kifo tu inazidi kutupa uchungu watanzania.

Kama huyu mzee angekufa kwa kifo cha kawaida. Nani angelaani?

Sasa hili la kusema kifo ni kifo tu linatoka wapi? Panick au kujisahau?
Pia amefananisha kifo cha mzee Kibao na vifo vingine tu mfano wanaohisiwa kuwa wachawi, albino nk.

Nimemshangaa sana rais sikuamini masikio yangu. Tuko nyuma sana.
 
Huyu rais bana, anadhani hatujui tofauti za vifo vya huko, achia mbali hatua zinazochukuliwa na wahusika kupatikana. Haya mauji na utekani wa sasa wa wapinzani, serekali yake ndio wahusika namba moja, na watu wote wenye akili timamu wanajua serekali yake ndio wahusika wakuu. Hiki kifo cha Ali Kibao kimekuja kuondoa shaka ya wale waliokuwa wanadhani vyombo vya dola sio wahusika. Hii hotuba yake lazima angeitoa hivi hivi maana yeye ndio muhusika, hivyo lazima avitetee vyombo vya dola.

Uzuri pamoja na geresha zake za kitoto, bado hajafanikiwa kubadilisha ukweli uliopo kwenye akili za wananchi walio wengi, wala kurejesha imani kwa vyombo vya dola na serekali yake.
Lucas Mwashambwa Tlaatlaah ChoiceVariable
ukweli ni kwamba,
ni Muhimu Zaid kuiombea Chadema imalize Uchaguzi wake wa ndani salama, maana joto na baridi ya nafasi za uongozi wa juu linafahamika kwa waTanzania, na ndio hasa chanzo cha huo unyama walomfanyia kiongozi mwenzao Mzee wa watu mpooleee sana kamanda Ally Mohamed Kibao...

watu wengine wanatamaa na uchu wa madaraka mbaya sana,
sasa mtu huna uhalali, huna hoja, hukubaliki, wajumbe na wanachama wamekuchoka unang'ang'ania hadi unaua wenzio kweli?

inatia uchungu sana..
Nawatakia Uchaguzi mwema kwa sehemu na nafasi za juu za uongozi wa chadema zilizosalia 🐒
 
Hata mtu mzima mpumbavu naye huzeeka.

Hivi Mwanasiasa, na Tena wa CHAMA kikubwa, Tena katika Nchi iliyoingia mikataba ya kimataifa kuhusu Siasa ,, AUWAWE, yaan ichukuliwe kua ni Kifo Cha kawaida tu??.

Mpumbavu anatolea mfano Trump, Trump si Dunia nzima kila Chombo Cha habari kilisimama kazi zake na kuanza kufatilia habari za Trump?.kwann wasingempuuza tu kua ni mtu wa kawaida??.

Anashangaa nini Kwa Mzee Kibao??.

Kwann Mataifa yasiingilie Kati katika bara hili la kijinga ambalo víongozi ni madikteta?.
Nimecheka Sana hii nchi ina vituko sana Jambazi atoke huko na VX na Bunduki ablock gari mchana mweupe kwenye gari kuna trafic afike ajitambulishe yeye ni Askari anapingu ambebe mtu mchana kweupe kama tumefika hatua hiyo Majambazi kuchukua watu mchana kweupe tena kublock gari ni hatari kwa Taifa ila najua hatujafika Uko je hao ni Wakina nani maana Police wanakataa
 
Unamaanisha wanaoua wana nguvu kuliko yeye na serikali yote?
Yaan daa,yaan mwee....yaan hata sielewi yaani....kwamba anaagiza mkuu? Mi sitaki kuamini hilo mbona hafananii😓
 
Maza kwa speech yake leo kachanganya mambo mazima,ilibidi atoe speech ya kuponya mioyo ya wananchi walio katika hofu

Khaa
 
Back
Top Bottom