Rais Samia ingia mtandaoni umsikilize Tundu Lissu kuhusu yanayoendelea Ngorongoro

Rais Samia ingia mtandaoni umsikilize Tundu Lissu kuhusu yanayoendelea Ngorongoro

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mhe. nakushauri uingie mariaspace muda huu (kama haujaingia) umsikilize Lissu akichambua yanayoendelea na ambayo yamekuwa yakiendelea huko Ngorongo na nakushauri usome na kitabu chake alichoandika kuhusu Ngorongoro.

Ukikosa nafasi, basi sikiliza hotuba yake ambayo bila shaka itapatkana ikiwa ni recorded (kumbuka amefanya utafiti katika eneo hilo).

Mama, Lissu atakusaidia sana katika hili jambo na tusingekuwa na mahusiano mabovu ya kisiasa, Lissu alipaswa kuwa mmoja wa washauri wako juu ya kutatua huu mgogoro wa Ngororo unaotokota chini chini kwa chini au tuseme unaotaka kuibuka.

Kama alivyomshauri Magufuli kwenye madini na akapuuzwa, ndivyo unaweza kufanya wewe, ila sidhani kama na wewe utakwepa yale matokeo yaliyomkuta mtangulizi wako katika ule mgogoro.
 
kwenye madini binafsi sikukubaliana na JPM kwenye baadhi ya mambo lakini TL hakuna lamaana aliloshauri zaidi ya makelele na baadaye nilihisi ana maslahi na Acacia kupitia watu fulani.

Ngoringoro its either Masai waondoke na Ngorongoro ibaki au Masai wabaki na Ngorongoro ipotee. Mwaka 1950 kulikuwa na Masai wangapi Ngorongoro na leo 2022 kuna Masai wangapi Ngorongoro...? Ukubwa wa Ngorongoro ni ule ule au umeongezeka..
 
Wamasai wamejaa nchi nzima na ngo'mbe zao. Yani vurugu mechi. Ila tunaishinao hivyo hivyo. Leo tunacheka kesho tumenuniana. Ila inaonekana wao sehemu moja tu ndo. ......wakiondoka huko ndo itakuwa kama. .labda wote watakufa.

Hakuna mtu asiejua umuhimu wa sekta yautalii katika nchi yetu.

Sawa la pale ni rahisi sana. It's not rocket science. Wanyama watabaki hapo hapo. Itolewe namba ya wamasai watakao baki hapo. Hilo jukumu wapewe wazee wakimasai wenyewe wachaguane nani wakubaki, nani wakuondoka. Na tunawapa mwezi mmoja tu.

Hao wamasai wasitake kutuchanganya vichwa. Sio kwamba labda wao tabaka Lao ni la juu kuliko watanzania wengine. Hii nchi yetu sote. Lazima wote tuwajibike.
 
Wamasai wamejaa nchi nzima na ngo'mbe zao. Yani vurugu mechi. Ila tunaishinao hivyo hivyo. Leo tunacheka kesho tumenuniana. Ila inaonekana wao sehemu moja tu ndo. ......wakiondoka huko ndo itakuwa kama. .labda wote watakufa...
Unamchukia masai ila unapenda nyama na maziwa? We vipi, huna msimamo! Kuwa rasi ule malalio ya nyoka mpaka unye bluu
 
Nilimuona Tundu Lissu siku moja enzi za ujana wake kwenye BBC documentary akihojiwa kama conservationists na mtaalamu wa maeneo hayo akiwaelezea nadhani historia ya Olduvai George na mambo ya symbiotic relation kwenye hayo maeneo alikuwa young kweli na mwajiriwa wa serikali.

Sikuamini nilichokiona binafsi tangia siku hiyo nilianza kumchukulia kama nyoka na hawa wanasiasa watanzania sio watu wakuwaamini 100% sikumbuki title ya ile documentary vinginevyo ningechukua screen shot.

So nakubali kabisa mtu akiniambia Tundu Lissu anauelewa mpana wa hayo maeneo na siasa zake. Ajabu hiyo historia ya maisha yake imefutwa na aipo kwenye CV yake wakati at one point Lissu worked in conservation areas as a government officer.
 
Daah ila ndo chawa wa mama aka TISS wanabutua kinoma yaani Lissu anakatika katika vibaya sana.
Kabisa, hapa kwenye Kama dk 5 zilizopita ilizimwa kabisa. Ila tumerudi tena. Lema anaongea.....
 
Tundu Lisu hamzidi Maulid Kitenge kwa uelewa wa mambo ya Ngorongoro!
20220208_000817.jpg
 
Back
Top Bottom